MADHARA YA MWANAMKE KUMEZA SHAHAWA
Wakati wa kufanya mapenzi,kuna mambo mengi huweza kufanyika kwa lengo la kuleta raha na msisimko zaidi wa tendo la ndoa,Wapo watu ambao hufanya mapenzi mpaka kwa njia ya mdomo yaani Oral sex, na wapo baadhi ya wanawake kufikia mpaka hatua ya kumeza shahawa za wanaume, je kuna madhara yoyote kwenye hili?
MADHARA YA MWANAMKE KUMEZA SHAHAWA NI YAPI?
- Kujiweka katika hatari ya kupata magonjwa mbali mbali ya zinaa yaani sexual transmitted diseases(STD's)
Kama ilivyo aina zingine za ngono zisizosalama,kumeza shahawa humuweka mwanamke kwenye hatari ya kupata magonjwa mbali mbali ya zinaa kama vile;
magonjwa ya zinaa yanayotokana na mashambulizi ya bacteria(Bacterial infection) mfano Kisonono(gonorrhea) pamoja na Chlamydia ambapo huweza kuathiri eneo la kooni kwa Mwanamke,
au magonjwa yanayotokana na mashambulizi ya virusi kwenye ngozi(skin viral infection) mfano herpes ambapo mtu huweza kupata baada ya kutokea mgusano wa ngozi pamoja na magonjwa mengine kama vile Kaswende(syphilis),maambukizi ya Human papilloma virus(HPV), Trichomoniasis n.k
Ushauri: Unashauriwa kujihusisha na ngono kwa njia ya mdomo au Oral sex endapo tu mtu unafanya naye kitendo hiki amepimwa magonjwa yote ya zinaa na imeonekana hana
- Pia mda mwingine mwanamke kumeza shahawa huweza kuwa chanzo cha kupata maambukizi ya fangasi maeneo ya mdomoni,kwenye ulimi au kooni,endapo shahawa zikaenda pamoja na vimelea vya ugonjwa wa fangasi kutoka kwa mwanaume
- Mwanamke kupata tatizo la Mzio au allergic reaction mwilini kutoka na kumeza shahawa hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Seminal plasma hypersensitivity,
Baadhi ya wanawake wana allergy na Shahawa au huweza kupata allergic reaction mwilini kutokana na kumeza shahawa, na matokeo yake wakaanza kupata madhara mbali mbali baada ya kumeza shahawa kama vile;
• Mwili kuanza kuwasha sana au kupata miwasho maeneo mbali mbali mwilini ikiwemo eneo la sehemu za siri
• Ngozi ya mwili kuanza kutengeneza wekundu zaidi kuliko kawaida kwenye baadhi ya maeneo
• Kupata maumivu makali ya viungo au misuli ya mwili
• Kuvimba kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama vile kwenye Lips za mdomo n.k
• Na hata baadhi ya wanawake kupata shida zaidi mpaka kwenye swala la upumuaji
- Hii hutegemea na mtu,ila baadhi ya wanawake baada ya kumeza shahawa na ladha mdomoni hubadilika kabsa, na kuona kila kitu akila ni kichungu kwenye mdomo wake,
Kumbuka kumeza shahawa wakati wa kufanya mapenzi sio swala la lazima,hivo unashauriwa kupima faida na hasara zake wewe mwenyewe kabla ya kufanya kitendo hiki,ila kwa kifupi hizo ndyo baadhi ya athari ambazo mwanamke huweza kupata baada ya kumeza shahawa.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!