Magonjwa haya yaongoza kusababisha VIFO DUNIANI

TAKWIMU:Orodha ya Magonjwa 10 yaliyoongoza kusababisha Vifo Duniani

“Mnamo 2021, sababu 10 kuu za vifo zilisababisha vifo milioni 39, Sawa na asilimia 57% ya jumla ya vifo milioni 68 ulimwenguni kote. Hii ni kwa mujibu wa Takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO).

Sababu kuu za vifo ulimwenguni, kulingana na jumla ya idadi ya watu waliopoteza maisha, zinahusishwa na mada mbili pana:

  • Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu/cardiovascular kama vile; (ugonjwa wa moyo wa ischemia, kiharusi n.k)
  • Pamoja na matatizo kwenye mfumo wa upumuaji ikiwemo (COVID-19, ugonjwa sugu wa mapafu au chronic obstructive pulmonary disease, pamoja na maambukizi kama vile lower respiratory infections)

Vitu hivi  vyaibuka kama sababu kuu za vifo duniani. katika Takwimu hizi Tatizo la Ischaemic heart disease limeshika namba Moja kwa Vifo ikifuatiwa na maambukizi ya Uviko 19(Covid-19).

Sababu za Vifo zinaweza kugawanywa katika makundi matatu:

  1. Magonjwa ya kuambukiza (magonjwa ya kuambukiza na ya vimelea na hali ya uzazi, uzazi na lishe),
  2. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza (sugu)
  3. na majeraha,ajali,Kuumia n.k.

Sababu kuu za vifo ulimwenguni
Katika kiwango cha kimataifa;

Sababu 7 kati ya 10 zinazoongoza za vifo katika mwaka 2021 zilikuwa za magonjwa yasiyoambukiza, ambayo yalisababisha asilimia 38% ya vifo vyote, au asilimia 68% ya visababishi 10 Vikuu.

Sababu kuu za vifo mnamo mwaka 2021 ulimwenguni”(Leading causes of death in 2021 globally)”

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!