Magonjwa yasiyoambukiza tishio Temeke

Magonjwa yasiyoambukiza tishio Temeke

IDADI ya wagonjwa wanaoumwa magonjwa yasiyoambukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke 2022/23 imeongezeka kutoka 9566 mwaka 2022/2023 hadi 11,175  kwa mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 14.4

Akikabidhi  jengo la kutolea huduma za kusafisha damu katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda amewataka wahudumu wa afya kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na magonjwa yasiyoambukiza huku jamii ikitakiwa kuzingatia mtindo bora wa maisha .

Akitoa taarifa ya Hospitali hiyo mganga Mkuu Dkt Joseph Kimaro amesema mwaka 2023/24 Hospitali ilipokea takribani wagonjwa 412 waliohitaji huduma za usafishaji damu ambao walipatiwa rufaa hivyo kuanzishwa kwa huduma hiyo kutasaidia kusogeza huduma hizo karibu na wananchi.

Kwa upande wake Mwakilishi  wa TPA  Abeid Galus amesema TPA itaendelea kushiriki katika miradi mbalimbali ya kijamii ambapo kwa sasa imetoa Shilingi milioni 251.26 kwa ajili ya maboresho ya jengo hilo pamoja na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi Milioni 10.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!