Mambo 5 ya kujua kuhusu Nimonia au homa ya mapafu
Pneumonia ni maambukizi kwenye mapafu. Mara nyingi husababishwa na bakteria au virusi. Ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa kupumua.
Watoto lakini pia watu wazima wanaweza kuugua ugonjwa huu. Kwa mujibu wa shirika la afya duniani, Watoto 740,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wamefariki kutokana na homa hiyo ya mapafu mnamo 2019. Kila Novemba 12 ulimwengu huadhimisha “Siku ya kimataifa ya kupambana na Pneumonia”.
Pneumonia au homa ya mapafu ni nini?
Kwa lugha nyepesi, ni maambukizi yanayotokea katika mfumo wa kupumua. Na mara nyingi maambukizi haya hutokana na virusi, bakteria au hata kuvu(fangasi).
Maambukizi yakitokana na bakteria, maji na usaha hukusanyika katika eneo linalofanya kazi kuchuja hewa ya oxygen na carbon dioxide wakati tunapopumua.
Hivyobasi kufanya upumuaji hewa kuwa vigumu, hatua inayosababisha pia kiwango cha oxgen kupungua katika damu mwilini.
Maambukizi yanaweza kuwa mepesi au mara nyingine husababisha hata kifo kwa muathiriwa.
Dalili za homa ya mapafu ni zipi?
Mtu yoyote anaweza kuugua homa ya mapafu. Dalili zake ni pamoja na
• Kupata matatizo ya kupumua
• Kuongozeka kwa mapigo ya moyo
• Joto mwilini
• Kutetemeka, kutokwa na jasho mwilini
• Kukohoa
• Maumivu kifuani
• Kuumwa na kichwa, kuhisi kutapika, kutapika, kuharisha n.k
Wataalamu wanasema ni muhimu kutambua aina ya homa ya mapafu kwa kufanyiwa utafiti wa maabara au Vipimo na kupata matibabu.
Shirika la afya duniani linasema kwamba iwapo maambukizi yametokana na bakteria au virusi madhara yake yako sawa. Hatahivyo dalili hutofautiana kidogo.
Iwapo homa hiyo imetokana na maambukizi ya virusi basi baadhi ya dalili anazokuwa nazo mgonjwa ni pamoja na;
- kikohozi,
- joto mwilini kuwa juu,
- mafua
- Pamoja na kupata matatizo ya kupumua.
Vipi unaweza kutambua mtoto anaugua homa ya mapafu ?
Joto mwilini
Watoto wanaweza kupata joto mwilini kwa sababu tofuati. Mara nyingi joto mwilini hutokea wakati mwili unapambana na ugonjwa. Lakini iwapo joto ni jingi sana au halishuki hata unapompatia mtoto dawa, ni lazima umfikishe mtoto kwa daktari. Matatizo ya kupumua
Upumuaji wa watoto huwa tofuati kila saa mchana. Wao hupata matatizo ya kupumua wanapopata maambukizi ya homa ya mapafu. Baadhi hutoa sauti kama firimbi kuashiria ugumu wanaopata kupumua. Hapa mzazi unahitaji kuwa na uangalifu mkubwa.
Uchofu.
Mapafu hujaa maji kutokana na homa hii. Na ndicho kinachosababisha shida ya kupumua. Mtoto anahisi kuchoka. Iwapo mtoto wako anaonekana kuchoka saa zote, basi ni muhimu apate ushauri wa daktari haraka iwezekanavyo.
Je homa ya mapafu inatibiwa vipi?
Ni muhimu kuzitambua dalili na mapema. Ni rahisi kutambua homa ya mapafu kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Anapopata matatizo ya kupumua ni muhimu kumfikisha hospitalini haraka iwezekanavyo.
Virusi ndani ya mapafu vinaweza kuchukua siku kadhaa hadi wiki kusambaa mwilini.
Maambukizi ya bakteria yanaweza kutibiwa kwa dawa za antibiotics.
Hatahivyo iwapo maambukizi ni makali huenda mgonjwa akahitaji kulazwa hospitalini.
Wataalamu wanashauri kwamba wagonjwa wanaweza kupoa haraka kwa kuchukua hatua kama vile kupumzika na kunywa maji mengi.
#SOMA ZAIDI hapa Kuhusu Ugonjwa wa Nimonia,chanzo,dalili na Tiba
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!