Metronidazole inatibu magonjwa gani

Metronidazole inatibu magonjwa gani

Katika Makala hii tumechambua baadhi ya magonjwa ambayo hutibiwa kwa kutumia dawa ya Metronidazole na hivo kujibu swali la "Metronidazole inatibu magonjwa gani?" .

Metronidazole ni dawa jamii ya antibiotic ambayo hutumika kutibu aina mbali mbali za maambukizi,

Dawa hii ya Metronidazole hujulikana kwa jina Maarufu kama vile "FLAGYL"

Metronidazole inatibu magonjwa gani

Metronidazole inatibu maambukizi ya magonjwa kwa kuzuia ukuaji wa vimelea mbali mbali vya magonjwa ikiwemo;

  • bacteria
  • pamoja na parasites.

Kumbuka: Dawa jamii ya antibiotic hutibu baadhi ya maambukizi yanayotokana na mashambulizi ya bacteria pamoja na parasite pekee, Dawa hizi haziwezi kufanya kazi dhidi ya maambukizi yanayotokana na mashambulizi ya virusi kama vile kwenye tatizo la genital warts n.k

Je,Metronidazole inatibu magonjwa gani?

Metronidazole inaweza kutumika kutibu magonjwa mbali mbali ikiwemo;

- Ugonjwa wa amoeba,

- Pia huweza kutumika na dawa zingine kwa mtu mwenye aina flani ya vidonda tumboni au kwenye utumbo(stomach/intestinal ulcers) ambavyo husababishwa na bacteria kama vile H. pylori.

- Metronidazole inatibu maambukizi mbali mbali kwenye ngozi, mdomoni n.k

- Metronidazole huweza kusaidia kama una maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama bacteria ndani ya Fizi zako

- Metronidazole inaweza kusaidia kama umepata shida ya jibu kwenye eneo la jino au meno(dental abscesses).

- Metronidazole inatibu matatizo kama vile;

  • bacterial vaginosis
  • pamoja na pelvic inflammatory disease(PID).

- Metronidazole ni dawa nzuri kutumika kuzuia Ukuaji wa bacteria au kutibu na kuzuia maambukizi ya bacteria pamoja na parasite kwa mtu mwenye vidonda mbali mbali ikiwemo;

  • Sehemu ambapo umeng'atwa na wadudu(insect bites)
  • Vidonda kwenye ngoz(skin ulcers),
  • Vidonda vinavyotokana na mgonjwa kulala kwa muda mrefu(bed sores)
  • Pamoja na aina nyingine za vidonda.

- Metronidazole inatibu maambukizi ya bacteria kwenye maeneo mbali mbali kama vile;

  • Ukeni
  • Tumboni,
  • Kwenye Ini
  • Kwenye ngozi
  • Kwenye joints
  • Kwenye ubongo
  • Kwenye uti wa mgongo
  • Kwenye mapafu
  • Kwenye Moyo
  • Kwenye damu(bloodstream) n.k.

- Metronidazole inatibu magonjwa ya Zinaa kama vile trichomoniasis,

Ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na mashambulizi ya parasite

TAHADHARI(Warnings)

Tahadhari juu ya Matumizi ya dawa aina ya Metronidazole;

1. Epuka matumizi ya metronidazole kutibu tatizo lolote ambayo halijafanyiwa uchunguzi na wataalam wa afya

2. Epuka kabsa Matumizi ya Pombe kama unatumia dawa ya Metronidazole

3. Epuka matumizi ya metronidazole kama umetumia disulfiram (Antabuse) ndani ya wiki mbili zilizopita.

4. Epuka kunywa Pombe au kutumia vyakula au dawa zenye propylene glycol ndani yake wakati unatumia dawa ya Metronidazole

5. Omba kwanza Ushauri kutoka kwa wataalam wa afya kabla ya kutumia metronidazole endapo una matatizo kama vile;

6. Usitumie Metronidazole kutibu magonjwa yanayotokana na mambukizi ya Virus kama vile tatizo la mafua,genital warts n.k.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!