MKOJO KUTOKA KIDOGO KIDOGO
Hali hii huhusisha mtu kukojoa kiwango kidogo sana cha mkojo na wakati mwingine huweza kuwa kidogo kidogo ila mara kwa mara au karibu karibu,
Kwa kawaida asilimia kubwa ya watu wazima hutakiwa kutoa mkojo yaani Adult urine output isiokuwa chini ya 500mls ndani ya masaa 24(kwa siku),
Lakini ukiwa unakojoa kiwango kidogo zaidi ya hichi huenda kukawa na sababu zingine za kiafya.
BAADHI YA SABABU ZA TATIZO LA KUKOJOA KIDOGO KIDOGO NI PAMOJA NA;
- Maji kupungua mwilini kutoka na sababu mbali mbali kama vile;
1. Kutokunywa maji ya kutosha
2. Kutapika sana
3. Kuharisha
4. Homa kali ambayo huweza kupelekea joto kuwa juu sana mwilini,kutoa jasho sana n.k
- Sababu nyingine huweza kuwa shida ya kuziba kwa njia ya mkojo kutokana na sababu mbali mbali kama vile kukua kwa tezi dume(enlarged prostate) n.k
- Mashambulizi kwenye njia ya mkojo kama vile UTI n.k ambapo hapa huweza kuambatana na maumivu wakati wa kukojoa
- Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile Anticholinergics pamoja na antibiotics zingine
- Pia kwa asilimia ndogo shida ya kuishiwa na damu yaani Blood loss/Anemia, huweza kuchangia tatizo hili
- Maambukizi makali(severe infection) ambayo huweza kusababisha Shocks n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!