Mtoto kutapika baada ya kula,chanzo na Tiba yake
Baadhi ya watoto wanapata shida hii ya kutapika kila wakipewa maziwa au chakula,lakini hawana shida nyingine yoyote kama vile Homa n.k
Je hali hii husababishwa na Nini? Soma hapa kujua baadhi ya Sababu zinazochangia uwepo wa tatizo hili kwa Watoto.
CHANZO CHA MTOTO KUTAPIKA MARA BAADA YA KULA
1.Mtoto kujifunza kula, Kama ulikuwa hujui Watoto wanajifunza kila kitu kutoka mwanzo, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kula au kumeza maziwa mara baada ya kuzaliwa,
Pamoja na kutema mate, mtoto wako anaweza kutapika mara kwa mara baada ya kulishwa. Hii ni kawaida zaidi katika mwezi wa kwanza mara baada ya mtoto kuzaliwa.
Inatokea kwa sababu tumbo la mtoto wako bado linazoea kusaga chakula. Pia wanapaswa kujifunza kutomeza maziwa haraka sana au kulishwa kupita kiasi.
Kutapika baada ya kulishwa kwa kawaida hukoma baada ya mwezi wa kwanza. Kama mtoto wako ana shida hii, Usimpe maziwa mengi kwa wakati mmoja,ila Mpe mtoto wako maziwa kidogo kidogo mara kwa mara au karibu karibu ili kusaidia kukomesha kutapika.
Lakini mjulishe daktari wako wa watoto ikiwa mtoto wako hutapika mara nyingi au kwa nguvu sana.
2. Tatizo la gastroenteritis ni miongoni mwa sababu kwa watoto wachanga na watoto kuanzia mwezi mmoja na kuendelea kutapika. Mtoto wako anaweza kuwa na mizunguko ya kutapika ambayo huja na kuondoka kwa takriban masaa 24.
Dalili zingine kwa watoto zinaweza kudumu kwa siku 4 au zaidi:
- kinyesi chenye majimaji au kuharisha kidogo
- Mtoto kutokutulia na kulia mara kwa mara
- Mtoto kukosa kabsa hamu ya kula
- Kupata maumivu ya Tumbo,
Na wakati mwingine shida hii inaweza kusababisha Homa ila mara nyingi sio kwa watoto wadogo.
Kwa watoto wachanga, gastroenteritis kali inaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini. Mpeleke mtoto hospital haraka ikiwa ana dalili za upungufu wa maji mwilini ikiwemo:
- ngozi kuwa kavu, mdomo au macho
- usingizi usio wa kawaida
- kilio dhaifu
- kulia bila machozi kutoka n.k
3. Tatizo la acid Reflux au GERD kwa watoto wachanga
Kama vile watu wazima wa umri wowote wanavyoweza kupata acid reflux au GERD, baadhi ya watoto wanapatwa pia na tatizo hili. Hii inaweza kusababisha kutapika kwa mtoto katika wiki za kwanza au miezi ya kwanza.
Epuka kumlisha mtoto kupita kiasi kwa wakati mmoja, badala yake mlishe kidogo kidogo ila mara kwa mara.
4. Mafua na kikohozi, Watoto hupata mafua kwa urahisi kwa sababu wana mifumo mipya ya kinga ambayo ingali inakua na mafua hutokea sana hasa kipindi cha baridi.
Kamasi nyingi kwenye pua huweza kusababisha mtoto apate shida ya kupumua, pia kutokuwa na hamu ya kula,
hali hii pamoja na mtoto kukohoa sana wakati mwingine husababisha kutapika kwa watoto baada ya kula.
5. Maambukizi ya sikio(Ear infection), Maambukizi ya sikio ni tatizo lingine ambalo huwapata sana watoto wachanga na watoto kuanzia mwezi mmoja na kuendelea.
Hii ni kwa sababu mirija ya masikio yao iko mlalo badala ya wima kama ilivyo kwa watu wazima.
Ikiwa mtoto wako ana maambukizi ya sikio, anaweza kuwa na kichefuchefu na kutapika bila homa. Hii hutokea kwa sababu maambukizi ya sikio yanaweza kusababisha kizunguzungu na kupoteza usawa. Dalili zingine za maambukizi ya sikio kwa watoto ni pamoja na:
• maumivu katika sikio moja au yote mawili
• sikio kutoa maji maji au usaha
• kusikia kwa shida n.k
Maambukizi mengi ya sikio kwa watoto huisha yenyewe bila matibabu. Hata hivyo, ni muhimu kuonana na daktari wa watoto ikiwa mtoto wako atahitaji antibiotics ili kuondoa maambukizi haya.
6. Kuzidisha joto, Kabla ya kumvalisha mtoto nguo nyingi angalia kwanza halijoto ya nje na nyumbani kwako.
Ingawa ni kweli kwamba joto lina umuhimu mkubwa kwa watoto, Ila wanaweza kupata joto zaidi kwa haraka katika hali ya hewa ya joto au katika nyumba yenye joto sana.
Hii ni kwa sababu miili yao midogo haina uwezo wa kutoa joto kwa urahisi kupitia kuvuja jasho. Kuongezeka kwa joto kunaweza kusababisha kutapika na upungufu wa maji mwilini.
Hivo unashauriwa kupunguza nguo mara moja na umlinde mtoto wako kutoka kwenye jua au chanzo chochote cha joto kali. Jaribu kunyonyesha kidogo kidogo ila karibu karibu au mara kwa mara, na pia unaweza kumpa mtoto wako maji kidogo ikiwa ana miezi 6 au zaidi. Pata matibabu ya haraka ikiwa mtoto wako harudi kama kawaida yake.
7.Tatizo la Motion sickness,Kwa kawaida watoto walio chini ya umri wa miaka 2 hawapati ugonjwa huu wa mwendo au motion sickness wakati wanasafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa gari,
lakini baadhi ya watoto wanaweza kuugua baada ya kupanda gari au kuzungushwa huku na huku - hasa ikiwa wametoka kula muda huo huo.
Ugonjwa wa mwendo unaweza kumfanya mtoto wako apate kizunguzungu na kichefuchefu, na kusababisha kutapika.
Kuna uwezekano mkubwa wa kutokea ikiwa mtoto wako tayari kashiba sana au ana shida ya tumbo kuvurugwa kutokana na kuvimbiwa, gesi, n.k
Harufu kali na barabara zenye upepo au zenye matuta zinaweza pia kumfanya mtoto wako apate kizunguzungu,kichefuchefu n.k.
Kichefuchefu huchochea mate zaidi na kisha kumfanya mtoto wako kutapika.
Unaweza kuzuia tatizo hili kwa kusafiri wakati mtoto wako yuko tayari kulala au ni rahisi zaidi kutokutokea kwa hali hii ikiwa mtoto wako anapenda kulala wakati wa safari.
Pia unashauriwa kuepuka kupanda gari Muda huo huo mara tu baada ya mtoto wako kutoka Kula.
8. Tatizo la Milk intolerance
Aina adimu ya hali hii ya kutovumilia maziwa inaitwa galactosemia. Inatokea wakati watoto wanazaliwa bila kimeng'enya fulani kinachohitajika kuvunja sukari kwenye maziwa. Baadhi ya watoto walio na hali wanapata shida hata kwenye maziwa ya mama.
Inaweza kusababisha kichefuchefu na kutapika baada ya kunywa maziwa au aina yoyote ya bidhaa za maziwa.
Galactosemia pia inaweza kusababisha upele wa ngozi au kuwasha kwa watoto na watu wazima.
HIZO NDYO BAADHI YA SABABU AMBAZO HUWEZA KUSABABISHA TATIZO LA MTOTO KUTAPIKA BAADA YA KULA.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!