MTOTO MCHANGA KUKOJOA DAMU,CHANZO NA TIBA YAKE
Kwenye wiki ya kwanza baada ya mtoto kuzaliwa,
Mama huweza kuona vidamu damu kwenye diapers wakati anamsafisha mtoto,
Lakini mara nyingi sio kwamba mtoto kakojoa damu ila ni mkojo ambao ni High concentrated ambao unaweza kusema ni damu.
Kwa watoto wakike unaweza kuona kama mtoto mdogo ila kaanza Blid, hii hutokana na mtoto kuwepo kwenye mazingira ya vichocheo au hormones kwenye tumbo la uzazi la mama yake kwa muda mrefu,
hali ambayo hupelekea mtoto kuanza kupata blid, ila baada ya kukaa kwenye mazingira ya Nje, hali hii hupotea yenyewe.
ANGALIZO: Endapo mtoto wako anakojoa damu na kupata dalili zingine kama vile;
- Maumivu makali ya tumbo
- Kutonyonya kabsa au uwezo mdogo sana wa kunyonya
- Mtoto kulegea
- Mtoto kutapika,kuharisha n.k
- Mtoto kupata homa au joto la mwili kuwa juu sana.
Mkimbize mtoto hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu ya haraka.
BAADHI YA VITU VINGINE AMBAVYO HUWEZA KUSABABISHA HALI YA KUKOJOA DAMU NI PAMOJA NA;
• Maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
• Maambukizi kwenye Figo
• Kiwango kikubwa sana cha Calcium na madini mengine kwenye mkojo
• Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo au UTI
• Kupata majeraha kwenye njia ya mkojo,figo au kibofu cha mkojo n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!