Ticker

6/recent/ticker-posts

P2 INAFANYA KAZI MUDA GANI



 P2 INAFANYA KAZI MUDA GANI

Hizi ni emergence contraceptives ambazo ni maarufu sana kwa jina la P2,

Dawa hizi hutumika Kuzuia mimba kwa dharura kama hujapanga kubeba Mimba,

Hata hivo matumizi ya mara kwa mara ya P2 sio salama kwako,ndyo maana zinaitwa emergence contraceptives,

ila sio njia ya uzazi wa mpango ya kudumu kama wengine wanavyofanya.

P2 INAFANYA KAZI KWA MUDA GANI?

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba; P2 itakukinga na Kubeba Mimba kwa asilimia 85%,

  •  P2 itakukinga na Mimba kwa asilimia 95% endapo umewahi kutumia ndani ya masaa 24 ya kwanza
  •  Uwezo wa P2 huanza kupungua mpaka asilimia 58%  kama umezitumia kati ya masaa 48 na 72 baada ya kufanya tendo la ndoa.

JE MADHARA YA KUTUMIA P2 NI YAPI?

➡️ P2

P2 ni dawa ya dharura (emergency contraceptive),inazuia mtu asipate Mimba kwenye mazingira ambayo umefanya sex pasipo kupanga na upo siku za hatari,

au umelazimishwa kufanya sex au umebakwa,ili kuzuia mimba zisizotarajiwa unalazimaka Kunywa hizi dawa.

Ni Dawa iliyotengenezwa kutumiwa mara chache tu,inapokulazimu,Sio dawa unayotakiwa kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Kuna wanawake humeza p2 kila mwezi,hii haitakiwi, Katika mazingira ya kawaida,haipaswi kumezwa zaidi ya mara 3 kwa mwaka.

Kuendekeza kila mwezi kunywa hizi p2 sio sahihi,Unatakiwa uende hospitali ili upate njia sahihi ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Baadhi ya Side effects/madhara ni ya matumizi holela ya dawa hizi ni 

  1. Unaweza kujisikia kichefuchefu au kutapika baada ya kumeza,
  2. Maumivu ya tumbo
  3. Matiti kuuma na kujaa
  4. Pia hedhi zako zinazofuata zinaweza zikawahi au zikachelewa au zikatoka nyingi sana( ukiona zimezidi siku 8 fika muone daktari) au ukawa unapata hedhi nyepesi sana,au pia haupati hedhi kabisa (amenorhoea)
  5. Kichwa kuuma na kizunguzungu
  6. Mabadiliko ya Ute ukeni (change in cervical secretion,hapa unakuta Ute wa ovulation mtu hapati).
  7. Kupata maambukizi ukeni,vaginal infections
  8. Hatari ya kupata PID
  9. Maumivu wakati wa sex(dyspareunia)
  10. Mama anakuwa hatarini kutungisha mimba nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy.
  11. Lakini pia kuna wanawake hupata Ovarian cyst,vivimbe kwenye mfuko wa mayai.

Kuna sababu hapo juu kama PID,kutopata UTE,infections kwenye uke hizi zinakuja athiri mwanamke anakuwa anapata taabu kwenye Kupata mimba

Kama hujapanga kupata mimba,tafadhari fuata njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu inayokufaa,achana na kumeza p2 kila mwezi.

HAYO NDYO MAELEZO MAFUPI KUHUSU P2 NA MATUMIZI YAKE.





Post a Comment

0 Comments