SABABU YA PUA KUWASHA NA TIBA YAKE
Tatizo hili huweza kuwa kero kubwa kwa mhusika kila mara, na huweza kutokea kwa muda mfupi kisha kutulia yaani acute au likawa tatizo la muda mrefu yaani Chronic.
Na kwa baadhi ya watu,shida hii huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile kukohoa,kupiga chafya sana n.k
SABABU YA PUA KUWASHA NI PAMOJA NA;
- Kushambuliwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa puani kama vile Virusi au kwa kitaalam Viral Infection mfano INFLUENZA n.k
- Tatizo la Mzio au Allergy, Kinga ya Mwili wako huweza kurespond kwenye vitu mbali mbali kama vile Vumbi,chemicals zenye harufu flani n.k
- Maambukizi ya Fangasi Puani yaani Fungal Infection, na wakati mwingine huweza kutokea mdomoni kwenda puani
- Kuota nyama ndani ya Pua yaani Nasal Polyps
- Uwepo wa Environmental Irritants ambapo huweza kupenya Puani, kama vile moshi,chemical products n.k
- Shida ya Sinusitis,ambapo huweza kuwa acute au Chronic, na wakati mwingine huambatana na matatizo mengine kama vile kupata shida ya kupumua,kuchoka sana,maumivu karibu na macho n.k
- Kutumia CPAP Machines,mashine hizi hutumika kwa wagonjwa lakini pia huweza kuchangia tatizo la kuwashwa Puani
- Shida ya ukavu puani yaani Dry Nose, hii hutokana na sababu mbali mbali kama vile; hali ya hewa ya joto sana,kutokunywa maji ya kutosha,Matumizi ya baadhi ya dawa,kupenga sana pua n.k
- Tatizo la Nasal Tumor ambapo kwa wakati mwingine huweza kuwa shida ya kansa au uvimbe tu puani ambao hauna uhusiano wowote na kansa.
MATIBABU YA TATIZO LA KUWASHWA PUANI
• Tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,mfano; kama chanzo ni Fangasi,Basi mgonjwa atapewa dawa za fangasi,kama ni allergic reaction mgonjwa atapewa dawa za allergy n.k
Pia mgonjwa hushauriwa matumizi ya maji mengi angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa siku, Pamoja na matumizi ya Dietary Supplements mbali mbali.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!