Connect with us

magonjwa ya watoto

Shingo ya Mtoto Kulegea(chanzo Chake)

Doctor Ombeni

Published

on

🩺
Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician.
254 Views
0 Comments

Shingo ya Mtoto Kulegea(chanzo Chake)

Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto huanza kuimarika na kuwa na nguvu ya kutosha ili kuweza kuinua na kusupport kichwa chake.

Uwezo huu wa shingo huimarika kabsa na kuwa na nguvu inayotakiwa kuweza kusupport kichwa cha mtoto(full control) kwenye miezi sita ya Mwanzo.

KUMBUKA; Sio lazima iwe hivo kwa kila mtoto, kuna baadhi ya watoto shingo inakuwa imekaza toka mwanzoni, na wengine huchelewa zaidi kujenga misuli Imara shingoni na kuifanya iwe STABLE.

Ili kujua kwamba baada ya mtoto kuzaliwa misuli yake ya shingoni(neck muscles) sio imara na haina nguvu,utaona akijaribu kuinua kichwa chake kinashuka chenyewe,

Hii ina maana misuli hii ya shingoni sio imara na haina nguvu ya kuweza kusupport kichwa chake.

Hivo basi katika kipindi hiki utatakiwa kumsupport mtoto kichwa chake pamoja na shingo yake kwa kutumia mikono yako.

MWEZI MMOJA MPAKA MIEZI MIWILI

– Kwa baadhi ya watoto mwishoni mwa mwezi wa Kwanza,wanaanza kujaribu kuinua kichwa, na pia wanaweza kupeleka kichwa kidogo upande mmoja kabla ya kichwa kurudi kilipokuwa.

WIKI NNE MPAKA WIKI 12

– Mpaka kufikia kipindi cha Wiki 12, Kwa baadhi ya watoto wanakuwa tayari wana uwezo wa kuinua kichwa vizuri bila shida yoyote.

NB: Uwezo wa mtoto kwenye ukuaji wake huweza kuwa tofauti na mwingine(Babies develop skills differently), Baadhi ya watoto huwahi zaidi kwenye hatua hizi na wengine huchelewa zaidi.

Lakini kama Mtoto wako anazaidi ya Miezi 5 mpaka 6 bado shingo haina dalili yoyote ya kukaza na hawezi kudhibiti kichwa chake vizuri unaweza kuongea na wataalam wa afya kwa ajili ya ushauri zaidi.

FAHAMU: Kama mtoto wako kazaliwa kabla ya Wiki 37 za Ujauzito anaweza kupata shida hii ya shingo kuchelewa kukaza pamoja na kuchelewa kwenye hatua zingine za ukuaji wake(development milestones).

Hapa nazungumzia hatua kama vile;

  • Mtoto kuanza Kukaaa
  • Mtoto kutambaa
  • Mtoto kusimama
  • Mtoto kutembea
  • Mtoto kuongea n.k

Hakikisha Unaongea na Wataalam wa afya Kwanza;

Au KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Sababu Za Shingo ya Mtoto Kulegea au Kuchelewa Kukaza

Kama tunazungumzia shingo ya mtoto kulegea na kushindwa kuishikilia vizuri,hapa tunazungumzia hali ambayo mara nyingi huitwa hypotonia (low muscle tone). Inaweza kuwa ya muda mfupi au ishara ya tatizo linalohitaji uchunguzi wa daktari.

Sababu zinazoweza kufanya shingo ya mtoto kulegea

1.Ukuaji wa kawaida kulingana na umri wake
Mtoto mchanga huwa bado hajajenga nguvu za misuli ya shingo. Hata hivyo, kadiri anavyokua, uwezo wa kushikilia kichwa unapaswa kuongezeka.

Lakini kama Mtoto wako anazaidi ya Miezi 5 mpaka 6 bado shingo haina dalili yoyote ya kukaza na hawezi kudhibiti kichwa chake vizuri unaweza kuongea na wataalam wa afya kwa ajili ya ushauri zaidi.

2.Mtoto Kuzaliwa kabla ya Wakati(Premature)

Hapa nazungumzia Watoto njiti(Premature),moja ya changamoto kubwa ambayo huweza kukutana nayo ni baadhi ya hatua za ukuaji kuchelewa ikiwemo hii ya kukaza shingo.

Kama mtoto wako kazaliwa kabla ya Wiki 37 za Ujauzito anaweza kupata shida hii ya shingo kuchelewa kukaza pamoja na kuchelewa kwenye hatua zingine za ukuaji wake(development milestones).

3.Ugonjwa uliopata wakati wa kuzaliwa au Baada ya kuzaliwa

Mfano,Mtoto mwenye tatizo la upungufu wa oksijeni wakati wa kuzaliwa (birth asphyxia),au kuugua magonjwa mengine kama Ugonjwa wa manjano n.k baada ya Mtoto kuzaliwa,inaweza kuchelewesha hatua za ukuaji kwa Mtoto huyo.

4.Tatizo la Hypotonia (misuli kuwa dhaifu)

Tatizo hili huhusisha Misuli kuwa legevu na hii inaweza kusababisha mtoto kushindwa kushikilia kichwa vizuri. Hypotonia inaweza kutokana na matatizo ya ubongo, mishipa, misuli au sehemu inayounganisha mishipa na misuli.

5.Matatizo ya Ubongo au mfumo mkuu wa neva
Mfano ni madhara ya ukosefu wa oksijeni wakati wa kuzaliwa (hypoxic-ischaemic encephalopathy) au baadhi ya matatizo ya ukuaji wa ubongo.

6.Tatizo la Mtindio wa Ubongo au Cerebral palsy
Baadhi ya watoto wenye tatizo la Mtindio wa Ubongo au cerebral palsy wanaweza kuwa na tatizo la misuli kuwa legevu au dhaifu (hypotonia), pamoja na kuchelewa kwa hatua za ukuaji kama;

  • kukaa,
  • kutambaa
  • au kutembea.

7.Kuwa na Magonjwa ya misuli au mishipa
Mfano ni spinal muscular atrophy (SMA), baadhi ya muscular dystrophies na congenital myopathies. Haya yanaweza kuambatana na udhaifu wa mikono/miguu au mtoto kutosogea sana.

8.Kuwa na Magonjwa ya kurithi/kijenetiki
Baadhi ya syndromes za kijenetiki, ikiwemo Down syndrome, zinaweza kusababisha hypotonia pia.

9.Maambukizi au ugonjwa mkali
Kwa mtoto ambaye ghafla amekuwa mlegevu au dhaifu sana, maambukizi makali kama sepsis yanaweza kuwa miongoni mwa sababu.

Ni wakati gani mtoto apelekwe hospitali haraka?

Pamoja na Dalili hiyo ya Shingo kulegea au kutokukaza kwa muda unaotakiwa,Mpeleke mtoto haraka kwa daktari/kitengo cha watoto ikiwa kulegea kwa shingo kumeanza ghafla, au kunaambatana na dalili hizi:

  • kushindwa kunyonya/kula,
  • kupumua kwa shida,
  • mtoto kuwa na usingizi kupita kiasi
  • udhaifu mkubwa wa mikono au miguu,
  • kupungua kwa harakati(movement),
  • homa au kuonekana mgonjwa sana.

NICE inapendekeza mtoto chini ya mwaka mmoja mwenye hypotonia iliyoanza ghafla apimwe haraka, na hypotonia inayoambatana na udhaifu, matatizo ya kula au kupumua inahitaji rufaa ya haraka.

Muhimu: Umri wa mtoto ni muhimu sana katika kutafsiri hali hii.

References;

  1. NICE – Suspected neurological conditions: recognition and referral.
  2. StatPearls/NCBI Bookshelf – Hypotonia.
  3. NICE – Suspected neurological conditions, Hypotonia in children.
  4. NHS – Cerebral palsy: Symptoms.
  5. Taverna et al. – Evidence-Based Clinical Algorithm for Hypotonia Assessment. BioMed Research International, 2018.
  6. Ahmed et al. – Genetic evaluation of the pediatric patient with hypotonia. Developmental Medicine & Child Neurology.
254 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo,...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician.  PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali...

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

🩺Medically reviewed by Dr.Elizabeth,A pediatrician. Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya...

255
0