Staili za kulala kwa mama mjamzito,Soma hapa kufahamu
Inaweza isiwe mara ya kwanza kwako kusikia kwamba,si kila staili ya kulala ni nzuri kwa mama mjamzito,
huenda ukawa umesikia mama mjamzito akilala sana chali atagandamiza mshipa mkubwa wa damu uonapita eneo la mgongoni na kusababisha mzunguko mbaya wa damu, mtoto kukosa hewa,chakula na hata kupoteza maisha.
Ni kweli kabsa sio kila staili ya kulala ni nzuri na salama kwa mama mjamzito, na Leo tunakuchambulia baadhi ya staili za kulala kwa mama mjamzito;
Staili za kulala kwa mama mjamzito
✓ Ulale ubavu wa Kushoto Au Kulia?
Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.
Ukweli ni kwamba, Kulala upande wa kushoto wakati wa ujauzito huwezesha mtiririko mzuri wa damu na kuhakikisha kwamba viungo muhimu na mtoto hupokea virutubisho na oksijeni.
Sleeping on the left side during pregnancy facilitates blood flow, ensuring that vital organs and the baby receive the nutrients and oxygen.
Pengine wajiuliza namna gani sahihi ya kulala kwa mjamzito? Wakati wa ujauzito madaktari wanapendekeza zaidi ulae kwa ubavu hasa kama mimba yako imeshakuwa kubwa. Hii ni kwasababu ya kuepuka kubonyeza mshipa mkubwa wa damu na kuzuia mtiririko mzuri wa damu inayozunguka kuelekea kwenye kizazi.
Kulala Kwa Ubavu wa Kushoto
Kulala kwa ubavu wa kushoto ni mkao sahihi zaidi kwa mama mjamzito ikilinganishwa na staili zingine za kulala kwa mjamzito. Kwasababu mkao huu unaruhusu mzunguko mzuri wa damu kutoka kwenye moyo wa mama kuelekea kwa mtoto.
Kulala kwa ubavu wa kushoto pia kunapunguza mgandamizo kwenye ini na figo. Hii itasaidia kupunguza kuvimba kwa vidole vya mikono , miguu na kwenye enka.
Je ni kweli Kulala Upande flani Ni kigezo cha Jinsia ya Mtoto?
Unaweza kuwa umesikia tetesi kwamba mwanamke akipenda kulalia upande flani basi ni jinsia fulani ya mtoto. Hii ni tetesi tu haina ukweli wowote. Hakuna utafiti wowote unaoonesha ukweli wa jambo hili.
Miezi Mitatu Ya Kwanza Ya Ujauzito(First Trimester)
Kipindi hiki unaruhusiwa kulala kwa namna yoyote, aidha kwa ubavu wa kushoto, kulia, kulalia tumbo au hata mgongo. Lakini kama unataka kujizoesha mapema kwa ajili ya baadae basi anza kulala kwa kuweka mto katikati ya miguu yako. Hii itakusaidia ufurahie usingizi na usipate kashkashi zozote.
Miezi Mitatu Ya katikati ya ujauzito(Second trimester)
Kadiri tumbo linavoongezeka utahitaji kupata godoro imara ambalo halibonyei sana kujizuia mgongo kujikunja sana unapolala. Endelea kutumia mto katikati ya miguu.
Miezi mitatu ya mwisho(Third trimester)
Endelea kutumia mto kukupa sapoti katika miezi hii ya mwisho kuelekea kujifungua. Katika kipindi hiki pendelea zaidi kulala kwa ubavu wa kushoto. Na mara chache lala kwa ubavu wa kulia, hakikisha pia unaweka mto mwingine eneo la kichwa liwe juu kidogo.
✓ Kulala Chali je ni Sahihi na Salama?
Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali wapo kwenye hatari ya kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi. Katika utafiti uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito walikuwa kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.
Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu. Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya watoto wafu wanaozaliwa katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.
✓ Kulala kwa Tumbo ni Salama?
Pengine umekuwa ukijiuliza vipi naweza kulala kwa tumbo nikiwa na mimba na isilete madhara yoyote? Jibu ni ndio unaweza kulala kwa tumbo kwa week 16 za kwanza za mimba. Kadiri mimba inavokuwa kubwa wewe mwenyewe itakushinda kulala na tumbo na itabidi ubadili mkao.
Usiwe na hofu kwamba mimba itaharibika pengine ikitokea kwa bahati mbaya umelala na tumbo. Mtoto analindwa na majimaji ya amniotic fluid kwenye chupa yake.
✓ Kulala kwa Mgongo
Kulala kwa mgongo ni salama ukiwa kwenye miezi mitatu ya mwanzo. Baada ya hapo kulala kwa mgongo itakuwa siyo salama kwani itasababisha upate matatizo ya maumivu chini ya mgongo, bawasili, matatizo ya tumbo na pia damu kutozunguka vizuri inavotakiwa.
Ikitokea mara chache usiku ukajisahau na kulala kwa mgongo basi usiwe na hofu badilisha tu mkao na maisha yaendelee vizuri mpaka ukishajifungua.
Ni matumaini yangu umejifunza na kuelewa vizuri kuhusu Staili za kulala kwa mama mjamzito.... Mungu akujalie Uzazi Salama, na Ujifungue salama katika Safari hii....!!!!!!!
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!