Ticker

6/recent/ticker-posts

TABIA YA KULA KUCHA,MADHARA,DAWA NA JINSI YA KUACHA KULA KUCHA



 TABIA YA KULA KUCHA,MADHARA,DAWA NA JINSI YA KUACHA KULA KUCHA

Kwa vipindi tofauti watu wengi huwa na tabia ya kula kucha wakiwa watoto, japo kwa baadhi ya watu tabia hii huendelea hadi ukubwani,

Na kwa wengine inakuwa tabia ambayo kuacha kufanya hivo hawawezi kabsa,

KWANINI BAADHI YA WATU HULA AU KUTAFUNA KUCHA?

Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo hupelekea watu kuanza kutafuna kucha, japo wengi wanaanzia udogoni na kuacha inakuwa ngumu,

Zipo baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa Tabia hii kutokea, na sababu hizo ni kama vile;

- Kucha kuwa ndefu,hivo mtu huona njia rahsi na yaharaka popote alipo ni kuanza kuzing'ata kwa lengo la kuzipunguza

- Mtu kuwa na hali ya kukosa utulivu,Kuwa na frustration au kuwa bored, Baadhi ya watu wakiwa kwenye hali kama hizi huweza kula au kutafuna kucha kama njia ya kuendana(copy) au kukabiliana na hali hyo.

- Wakati mwingine ni akili yako kutokuwa mahali hapo(absentminded) wakati unatakiwa kuconcentrate sana kwenye kitu ambacho unafanya, ndipo unaanza kula kucha kama njia ya kukurudisha hapo bila wewe kujua.

- Kuwa na Msongo wa mawazo(Stress) au kuwa na wasi wasi(anxiety), Wakati upo kwenye hali hizi unaweza kuanza kula kucha kama njia ya kukusaidia kupata ahueni(relief) na hali hizo za Stress au Wasi wasi sana.

- Pia tabia hii huweza kuhusishwa na matatizo ya afya ya akili kama vile;

(i) attention deficit hyperactivity disorder (ADHD)

(ii) major depressive disorder (MDD)

(iii) obsessive-compulsive disorder (OCD)

(iv) oppositional defiant disorder

(v) separation anxiety disorder

Pamoja na Tourette syndrome, ila unachotakiwa kukijua ni kwamba sio kila mtu anayekula kucha basi ana matatizo kwenye afya ya akili.

MADHARA YA KULA KUCHA

kumbuka unavyokula kucha unaweza kuleta shida kwenye kucha ila wakati mwingine ni mpaka kwenye nyama au tissues za vidoleni,

- Unaweza kupata vidonda au michubuko kwenye kucha au kuzunguka ngozi ya vidole, Vidonda hivi huweza kupelekea maumivu, damu kuvuja kwenye kidole n.k

- Kula kucha kunasababisha kucha kutokuwa na muonekano mzuri(abnormal-looking nails)

- Kuwa kwenye hatari ya kupata fangasi(fungal Infections) hasa kwenye eneo la Nail Plate pamoja na kuzunguka ngozi

- Kupata magonjwa mengine kutokana na vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria pamoja na Virusi kutoka vidoleni kwenda mdomoni wakati unakula kucha.

- Unaweza kusababisha madhara mengine kwenye meno kama vile; meno kuchimba,mpangilio mbaya au tatizo la dental resorption

- Kupata maumivu kama vile temporomandibular joint pain pamoja na dysfunction

- Kusababisha michubuko mdomoni, kwenye fizi za meno n.k

- Pia tabia hii ya kula kucha inaweza kuongeza hatari ya wewe kupata maambukizi kama vile stomach and intestinal infections. N.K

JINSI YA KUACHA TABIA HII YA KULA KUCHA

Kama tunavyojua tabia sio kitu ambacho hutokea ndani ya siku moja,hivo hata kuacha kwake pia huweza kuwa ni mchakato endelevu. Ukiona njia ya kwanza haifanyi kazi jaribu ya pili, mpaka upate matokeo unayoyataka.

1. Hakikisha unakata kucha zako vizuri, moja ya sababu ambazo hupelekea kuanza kula kucha ni pale unapoona kucha zako ni ndefu, hivo hakikisha hukai na kucha ndefu zikate vizuri kila wakati zinapokua.

2. Jenga utaratibu wa kutunza kucha zako na kuhakikisha zinakuwa na muonekano mzuri,

Huwezi kung'ata kucha kama unatamani kucha zako ziwe na muonekano mzuri

3. Na kwa wale ambao wanapaka rangi kucha, hii inaweza kuzuia wewe kula kucha zako, kwa kuogopa kuharibu muonekano,

lakini pia kuogopa kula rangi mdomoni, na wakati mwingine mbali na kwamba rangi ina makemikali, pia huleta ladha mbaya mdomoni.

4. Dhibiti matatizo mengine kama vile Woga, wasi wasi, msongo wa mawazo n.k

5. Hakikisha mikono yako inakuwa bzy kwa kufanya vitu mbali mbali, moja ya vitu ambavyo huweza kukushawishi wewe kuanza kula kucha, ni mikono yako kukosa chakufanya.

6. Kama pia imekuwa too much,sio vibaya kufanya vipimo ikiwemo Vipimo vya afya ya akili

UKIONA MAMBO HAYA ONANA NA WATAALAM WA AFYA MAPEMA ZAIDI

- Kucha imeanza kuota pembeni au umepata tatizo la ingrown nails

- Maambukizi ya kwenye ngozi au kucha, kuwa na vidonda ambavyo haviponi n.k

- Kucha kupoteza rangi yake ya asili(nail discoloration)

- Kuvuja damu kuzunguka kwenye kucha ambayo inatoka mfululizo

- Kucha kuacha kuota tena au kuacha kukua, kucha kutoka kabsa n.k





Post a Comment

0 Comments