Tatizo la Allergy kwenye Dawa Zenye Sulphur,Dawa zipi zina Sulphur
Baadhi ya watu wana allergy na dawa zenye Sulphur,hivo baada ya kutumia dawa hizi hupata shida sana.
Ushauri; Kama unajijua una shida hii kabla ya kuondoka hospital na kwenda kutumia dawa unazoelekezwa na Daktari, Muulize kwanza zina Sulphur?
Na kama amesahau kukuuliza kuhusu allergy ya dawa ikiwemo hizi zenye sulphur,Mkumbushe kwamba wewe unapata shida ukitumia dawa zenye Sulphur.
Hii itakusaidia wewe, kwani watu wengi hupata madhara sana,ikiwemo kuungua ngozi n.k
HIZI HAPA CHINI NI BAADHI YA DALILI,IKIWA WEWE UNA ALLERGY NA DAWA ZENYE SULPHUR
Dalili za mzio wa salfa au Allergy kwenye dawa zenye sulphur huendana kabsa na zile za Allergic reaction kwenye dawa zingine.
Mara baada ya kutumia dawa zenye Sulphur utaanza kuona mabadiliko Mwilini, na Dalili zinaweza kujumuisha:
- Mtu kuanza kupata upele kwenye ngozi(skin rashes),
- Ngozi ya mwili kuungua, kuanza kutoa magamba n.k
- Shida ya macho kuwasha
- Kupata shida ya Ngozi kuwasha, kuanza kuvimba baada ya kujikuna n.k
- Kuvimba kwenye mdomo au Lips za mdomo
- Kupata uvimbe wa koo n.k
DAWA ZENYE SULPHUR NI ZIPI?
• Baadhi ya Dawa zenye sulfa ni pamoja na:
✓Baadhi ya Dawa jamii ya Antibiotics(Sulfonamide antibiotics) ikiwemo; sulfamethoxazole-trimethoprim (Bactrim, Septra), erythromycin-sulfisoxazole (Eryzole, Pediazole) n.k
✓ Baadhi ya dawa za Kisukari(diabetes medications) kama glyburide (Diabeta, Glynase PresTabs)
✓ Sulfasalazine (Azulfidine), ambazo hutumika kwa tatizo la rheumatoid arthritis, Crohn’s disease, na ulcerative colitis
✓ Dawa jamii ya dapsone ambazo hutumika kwa tatizo la dermatitis na baadhi ya aina za pneumonia
✓ Dawa jamii ya sumatriptan (Imitrex), kwa ajili ya tatizo la migraines
✓ Baadhi ya anti-inflammatory drugs kama vile celecoxib (Celebrex) n.k
✓ Baadhi ya dawa kwenye kundi la diuretics kama vile; hydrochlorothiazide (Microzide) pamoja na furosemide au kwa jina lingine hujulikana kama Lasix.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!