Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA BANDAMA KUVIMBA AU KUJAA MAJI,CHANZO,DALILI NA TIBA



 TATIZO LA BANDAMA KUVIMBA AU KUJAA MAJI,CHANZO,DALILI NA TIBA

Watu wengi kwa hivi sasa hupatwa na tatizo hili la bandama kuvimba huku wengine wakiambiwa bandama zimejaa maji baada ya kufanyiwa vipimo mbali mbali, tatizo la bandama kuvimba kwa kitaalam hujulikana kama Splenomegaly, je chanzo cha matatizo ya bandama kuvimba au kujaa maji ni nini?

CHANZO CHA TATIZO LA BANDAMA KUVIMBA NI PAMOJA NA;

- Maambukizi mbali mbali ya vimelea vya magonjwa kama vile;

1. Maambukizi ya bacteria mfano bacteria wanaosababisha ugonjwa wa kaswende au syphilis,maambukizi ya bacteria kwenye kuta za ndani ya moyo na kusababisha matatizo kama endocarditis n.k

2. Maambukizi ya virusi kama vile mononucleosis n.k

3. Maambukizi ya Parasites kama vile kwenye ugonjwa wa Malaria

4. Magonjwa ya ini kama Cirrhosis pamoja na magonjwa mengine yanayoshambulia Ini

5. Aina mbali mbali za anemia(upungufu wa damu mwilini), hasa anemia inayohusu uvunjaji wa seli nyekundu za damu yaani RED BLOOD CELLS(RBCs) kwenye hatua ya mwanzo kabsa kabla ya kukomaa

6. Uwepo wa tatizo la kansa kwenye damu kama vile: shida ya Leukemia,Lmyphomas,myeloproliferative neoplasms n.k

7. Magonjwa au matatizo mbali mbali kwenye mfumo wa uvunjaji chakula kwenye seli yaani metabolic disorders kama vile tatizo la Gaucher,Niemann n.k

8. Tatizo la presha kwenye mishipa ya Veins ndani ya Bandama au Ini au mtu kupatwa na shida ya damu kuganda au kutengeneza clots kwenye mishipa hii ya veins

9. Magonjwa kwenye mfumo wa kinga ya mwili yaani autoimmune conditions kama vile shida ya Lupus,Sarcoidosis n.k

DALILI ZA MTU MWENYE MATATIZO HAYA YA BANDAMA NI PAMOJA NA;

- Mtu kupata maumivu makali upande wa kushoto karibu na mbavu

- Mtu kuhisi uzito kwenye eneo la karibu na mbavu kushoto juu kidogo ya kitovu

- Hali ya mtu kuhisi kushiba hata kama umekula kidogo sana au hujala kitu,hii ni kwasababu bandama hugandamiza tumbo la chakula hivo kufanya chakula kiingie kidogo sana au mtu kuhisi kushiba muda wote

- Mtu kuanza kuonyesha dalili mbali mbali za upungufu wa damu yaani anemia kwenye mwili wake

- Mtu kupata shida ya kuvuja damu kwa urahisi zaidi,kushambuliwa na magonjwa mbali mbali mara kwa mara n.k

VIPIMO MBALI MBALI KUFANYIKA KAMA VILE

• Vipimo vya kuchukua Sample ya damu yaani blood tests

• Kufanya physical examination

• Kufanya ultrasound,Ct Scan au MRI n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA BANDAMA

Tiba ya matatizo ya bandama kama vile bandama kuvimba au bandama kujaa maji hutegemea na chanzo chake,hivo kama chanzo ni maambukizi ya bacteria basi mgonjwa atapewa antibiotics mbali mbali kutibu shida hii n.k

Kama matibabu ya dawa yameshindikana huduma ya upasuaji huweza kufanyika kwa mgonjwa

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments