TATIZO LA KUPATA HEDHI KIDOGO(chanzo chake)
Tatizo la mwanamke kupata hedhi ndogo sana(light period) au matone matone na wakati mwingine kutokutoka kabsa husababishwa na nini? Soma hapa baadhi ya sababu za tatizo hili
1. Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango hasa zile zenye vichocheo ndani yake(hormonal birth control),
Tatizo la kupata hedhi ndogo,matone matone au kutokupata kabsa huweza kutokea baada ya kutumia njia za uzazi wa mpango zenye vichocheo,kwani husababisha mabadiliko makubwa kwenye vichocheo mwilini
2. Tatizo la Mwanamke kushindwa kutoa yai(Anovulation) au tatizo la Ovaries kutokufanya kazi vizuri hasa mwanamke akikaribia ukomo wa hedhi(menopause).
3. Tatizo la Mwanamke kuwa na uzito mdogo sana wa Mwili(underweight) au Mwanamke kupungua uzito wake wa Mwili kwa kasi sana,
hii huweza kusababisha period kuanza kutoka kidogo sana na wakati mwingine kuacha kabsa kutoka.
Chanzo: Mabadiliko haya ya uzito wa mwili husababisha kiwango cha mafuta mwilini(Body fat level) kuwa kidogo sana hali ambayo huweza kuathiri utokaji wa yai(ovulation) na wakati mwingine yai kutokutoka kabsa.
4. Kufanya mazoezi kupita kiasi(Excessive exercise) pamoja na kuwa na matatizo kwenye ulaji wako(eating disorder), vyote hivi huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili
5. Ujauzito, Kwa kawaida kipindi cha Ujauzito period(hedhi) huacha kabsa kutoka, Lakini Mwanamke huweza kuendelea kuona vidamu damu(light period) wakati mtoto akijishikiza kwenye mji wa mimba yaani kwa kitaalam hujulikana kama implantation bleeding
6. Tatizo la Msongo wa Mawazo au STRESS, Fahamu kwamba ukiwa na Stress mzunguko wako wa hedhi unaweza kubadilika kabsa, na moja ya mabadiliko ambayo unaweza kuyapata ni pamoja na hedhi kuacha kabsa kutoka au kutoka kidogo sana.
Ukiwa na stress mara kwa mara na kwa muda mrefu, huweza kuleta mabadiliko kwenye vichocheo mwilini(hormones changes) hali ambayo huweza kuathiri mzunguko wako wa hedhi.
7. Matatizo mengine ya kiafya(Medical conditions) kama vile;
- thyroid dysfunction
- polycystic ovary syndrome (PCOS)
- perimenopause
- Cushing’s syndrome N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!