Tatizo la macho kuona ukungu,chanzo chake ni nini?
Kwa asilimia kubwa,chanzo cha tatizo la macho kuona ukungu,au mawingu mawingu mbele chanzo chake ni Mtoto wa Jicho.
Mtoto wa jicho ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama CATARACT, tatizo hili huhusisha kutokea kwa Wingu kwenye lens za jicho lako. Hali ambayo husababisha mtu kutokuona vizuri,kuona wingu mbele(Clouded vision) n.k.
DALILI ZA MTOTO WA JICHO NI PAMOJA NA;
- Mtu kutokuona vizuri,kuona marue rue,kuona wingu mbele(Clouded vision) n.k
- Kupata shida ya kuona sana hasa wakati wa Usiku
- Jicho kuwa na Mwanga hafifu sana(Dim vision)
- Kushindwa kufanya chochote kama vile kusoma n.k pasipokuwa na Mwanga wa kutosha(brighter light)
- Mtu kuanza kuona kila rangi imefifia(Fading) au kuona unjano kwenye rangi(yellowing of colors)
- Kuona mara mbili kwenye jicho moja(Double vision in a single eye) n.k
AINA ZA MTOTO WA JICHO(CATARACT)
1. Aina ya mtoto wa jicho ambayo huathiri katikati(center) ya Lens, aina hii hujulikana kama NUCLEAR CATARACTS.
2. Aina ya mtoto wa jicho ambayo huathiri kwenye Kingo(edges) za Lens, aina hii hujulikana kama CORTICAL CATARACTS.
3. Aina ya mtoto wa jicho ambayo huathiri nyuma ya Lens, aina hii hujulikana kama POSTERIOR SUBCAPSULAR CATARACTS.
4. Aina ya mtoto wa jicho yakuzaliwa nayo, aina hii hujulikana kama CONGENITAL CATARACTS.
CHANZO CHA MTOTO WA JICHO NI NINI?
• Kwa asilimia kubwa tatizo la mtoto wa jicho hutokea baada ya mtu kuzeeka(aging) au kuumia kwenye jicho ambako huweza kuleta mabadiliko makubwa ya tissues zinazounda LENS za macho.
Nyuzi nyuzi(Fibers) pamoja na Proteins kwenye Lens huanza kuvunjika na kusababisha hali ya kuona ukungu au mawingu kwenye macho(Clouded vision).
• Baadhi ya matatizo ya kurithi(inherited genetic disorders) huweza kuongeza uwezakano wa mtu kupata tatizo la Mtoto wa jicho.
• Sababu zingine ni pamoja na;
- jicho ambalo hapo nyuma lilifanyiwa upasuaji yaani Past eye Surgery huwa kwenye hatari ya kupata mtoto wa jicho(Cataract)
- Mtu Kuwa na matatizo mengine kama vile Ugonjwa wa kisukari(diabetes) n.k
- Matumizi ya dawa jamii ya STEROIDS au corticosteroid kwa muda mrefu sana huweza kusababisha tatizo la Mtoto wa jicho.
WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA TATIZO LA MTOTO WA JICHO NI PAMOJA NA;
1. Watu wenye umri mkubwa au Wazee
2. Watu wenye ugonjwa wa Kisukari
3. Watu ambao hukaa kwenye Mwanga mkali kama wa jua n.k kwa muda mrefu
4. Watu ambao huvuta Sigara
5. Watu ambao wana shida ya uzito mkubwa(Overweight/Obesity)
6. Watu wenye ugonjwa wa Presha ya kupanda(High blood pressure)
7. Watu ambao wameshawahi kuumia kwenye macho,kupata uvimbe wa macho au kuwahi kufanyiwa upasuaji wa macho(past eye surgery)
8. Watu ambao wametumia dawa jamii ya STEROIDS au corticosteroid kwa muda mrefu
9. Watu ambao wanakunywa Pombe kupita kiasi n.k
MATIBABU YA TATIZO LA MTOTO WA JICHO,
Kama mgonjwa kapewa miwani(prescription glasses) lakini hazikumsaidia chochote,Tiba kubwa ya tatizo hili ni UPASUAJI(Surgery).
ZINGATIA MAMBO HAYA;
- Jenga utaratibu wa kufanya checkup ya macho mara kwa mara hasa pale unapoona hali yoyote ya tofauti kwenye macho yako
- Acha kabsa uvutaji wa Sigara
- Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi
- Dhibiti magonjwa mengine kama vile ugonjwa wa Sukari,Presha n.k
- Pata mlo kamili kila siku(Balance diet)
- Vaa protective eye glasses kama unafanya kazi zinazohusisha mwanga mkali kama vile kuchomelea n.k
- Dhibiti tatizo la Uzito mkubwa(overweight/Obesity)
- Epuka matumizi ya muda mrefu ya dawa jamii ya STEROIDS au corticosteroid N.K
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!