TATIZO LA USONJI(AUTISM),CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE
Tatizo la usonji(autism) ni tatizo ambalo huhusisha hitilafu kwenye maendeleo ya ubongo wa mtoto ambayo huleta shida zingine kama vile; tatizo la mtoto kutokuongea,kujitenga n.k,na tatizo hili huanzia utotoni na kusababisha matatizo makubwa mpaka utu uzima.
Tatizo hili la Usonji ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Autism hutokea kwa baadhi ya watoto na tafiti zinaonyesha kwa wazazi wengi huchelewa kugundua kama watoto wao wana shida hiyo mpaka watoto wakiwa na umri wa miaka 2-3 na kuendelea.
Mtoto mwenye tatizo la Usonji hupatwa na tatizo la kutokuongea,hupenda kujitenga sana na wenzake au watu wengine, na pia tafiti zinaonyesha kwamba tatizo hili la Usonji huwapata watoto wa jinsia ya KIUME zaidi kuliko ya KIKE.
CHANZO CHA TATIZO LA USONJI
- Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa tatizo la Usonji au Autism,japo kuna baadhi ya sababu ambazo zimeonekana kuweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa tatizo hili la Usonji,na sababu hizo ni kama vile;
1. Tatizo la vinasaba(genetics) ambapo hujulikana kwa kitaalam kama vile neurodevelopmental disorders, hapa tunazungumzia matatizo mbali mbali kama vile Rett syndrome,Fragile X syndrome n.k
2. Sababu za kimazingira kama vile; Kupatwa na maambukizi ya (Virusi) ugonjwa wa RUBELLA n.k
3. Matumizi ya baadhi ya dawa kipindi cha ujauzito
4. Complications mbali mbali ambazo huweza kumpata mama wakati wa ujauzito
5. Mama mjamzito kutumia vilevyi mbali mbali kama vile pombe,madawa ya kulevyia kama Coccaine n.k
6. Uchafuzi wa hewa hivo kusababisha watu kuvuta hewa chafu n.k
7. Kuwa na mtoto mwenye tatizo hili la usonji kwenye familia au koo flani huweza kuongeza uwezekano wa watoto wengine kuzaliwa na tatizo hili
8. Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati hasa kama imetokea kabla ya wiki 26 za ujauzito, na kwa hapa kwetu Tanzania ni ngumu sana kwa mtoto huyu kuishi,angalau kuanzia wiki 28 na kuendelea uwezekano wa kuishi ni mkubwa.
9. Wazazi kujifungua watoto wakiwa na umri mkubwa sana,japo tafiti zinaendelea kufanyika juu ya hili,ila baadhi ya tafiti zinasema mwanamke kuchelewa kuzaa au kuzaa akiwa na umri mkubwa sana huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili la Usonji
NJIA ZA UTAMBUZI WA TATIZO HILI KWA MTOTO
• Wataalam wa afya watataka kujua kuhusu hatua za ukuaji wa mtoto,uwezo wake wa akili pamoja na kufanya vipimo mbali mbali kama vile genetic testing n.k
DALILI ZA TATIZO LA USONJI NI PAMOJA NA;
- Mtoto kushindwa kuitika baada ya kuitwa jina lake au mtoto kuonekana kutokusikia kabsa wakati akiitwa jina lake
- Mtoto kushindwa kutazama watu usoni(eye contacts), kutokucheka,n.k
- Mtoto kutokuongea kabsa au kuchelewa sana kuongea kuliko kawaida
- Kupoteza uwezo wa kutamka maneno au sentensi ambazo mwanzoni alikuwa anaweza kutamka
- Mtoto kushindwa kabsa kuanzisha mazungumzo
- Mtoto kuongea huku akitoa sauti zisizozakawaida
- Mtoto kushindwa kuelewa maswali rahisi akiulizwa na watu
- Mtoto kufanya vitu vya kujidhuru mwenyewe kama vile; kujipiga mwenyewe,kujibamiza kichwa n.k
- Mtoto kutokutaka mwanga,kushtuka sana akiguswa au kusikia sauti yoyote
- Mtoto kutokutamka maneno ya kitoto mpaka afikishe umri wa mwaka mmoja na kuendelea
- Mtoto kutokuongea neno lolote mpaka afikishe kipindi cha umri wa miezi kumi na sita
- Mtoto kupoteza kabsa uwezo wake wa kuongea
- Mtoto kushindwa kufanya vitu mbali mbali kama kupunga mkono kwa wazazi au mtu yoyote kama ishara ya kumsalimia au kumuaga mpaka anapofikisha kipindi cha umri wa miezi kumi na mbili
- Mtoto kushindwa kuongea maneno zaidi ya mawili au sentensi ya maneno mpaka anapofikisha umri wa miezi 24
- Mtoto kuwa na tabia ya kukaa peke yake pamoja na kujitenga na watu N.k
MADHARA YA TATIZO LA USONJI KWA WATOTO NI PAMOJA NA;
• Mtoto kushindwa kuongea kabsa,kuchelewa sana kuongea au kuongea maneno ambayo hayaeleweki
• Mtoto kushindwa kuchangamana na watu wengine(kujitenga muda wote)
• Mtoto kuwa na matatizo ya kutokuelewa akiwa shuleni
• Tatizo la kupewa ajira au kuajiriwa
• Kusababisha msongo wa mawazo na hali ya huzuni katika familia N.k
MATIBABU YA TATIZO LA USONJI
Tatizo hili halitibiki au hakuna tiba ya kuondoa kabsa tatizo hili,ila kuna tiba ya kudhibiti dalili mbali mbali ambazo husababishwa na tatizo hili la Usonji, na kwa ujumla wake zipo tiba mbali mbali kama vile;
✓ Matumizi ya dawa za kudhibiti dalili za tatizo la Usonji
✓ Huduma ya kimawasiliano pamoja na ufundishwaji wa tabia mbali mbali kwa mtoto yaani Behavior and Communication therapy
✓ Huduma ya uelimishwaji yaani educational therapy n.k
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!