Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa amoeba kwa watoto,chanzo,dalili na Tiba



Ugonjwa wa amoeba kwa watoto,chanzo,dalili na Tiba

Mara nyingi kimelea cha amoeba kinaweza kuingia kwenye mfumo wa umeng’enyaji chakula na kuishi bila kusababisha dalili yoyote ile, isipokuwa kikivamia kuta za utumbo mpana.

Uvamizi kwenye utumbo mpana husababisha dalili za kuharisha damu, maumivu na kunyonga kwa tumbo, kichefuchefu, kukosa hamu ya kula na homa. Amoeba anaweza kusafiri kwenda pia sehemu nyingine ndani ya mwili na kusababisha maambukizi kwenye Ini, mapafu moyo na ubongo.

Dalili za Ugonjwa wa Amoeba kwa watoto

Watoto wenye maambukizi ya amoeba huwa hawaonyesi dalili kwa mara ya kwanza,Baadhi ya watoto hupata dalili ndani ya siku au wiki chache, lakini wapo baadhi pia hupata baada ya miezi kadhaa kupita.

Endapo dalili zitatokea zinajumuisha;

  • Maumivu ya tumbo yanayoanza taratibu na kuambatana na choo kilaini au cha majimaji
  • Kunyonga kwa tumbo
  • Kichefuchefu
  • Kupoteza hamu ya kula
  • Haja kubwa yenye kamasi

Dalili zingine zinazoweza kutokea kwa baadhi ya watoto ni;

  • Kupata Homa
  • Haja kubwa ilichonganyika na damu

Wakati gani uwasiliane na daktari haraka endapo mwanao ana dalili za ugonjwa wa amoeba?

Wasiliana na daktari haraka kwa matibabu endapo mwanao ana dalili zifuatazo;

- Kuharisha damu au kupata kinyesi chenye kamasi

- Maumivu ya tumbo ( ataonekana kwa kukunja sura au kujikunja mwili sehemu ya tumbo) kwa mtoto mkubwa atasema kuwa ana maumivu ya tumbo

- Kuchemka

- Kujaa kwa tumbo

- Maumivu sehemu ya kulia chini ya mbavu

Vihatarishi vya maambukizi ya ugonjwa wa amoeba kwa watoto

Maambukizi ya Ugonjwa wa amoeba hutokea mara nyingi kwenye maeneo yasiyo na mfumo mzuri wa utunzaji wa maji taka,

Maeneo hayo hujumuisha maeneo yenye mkusanyiko mkubwa wa watu na yasiyo na utunzaji mzuri wa kinyesi cha binadamu.

Hii ndio maana ugonjwa huu hutokea katika nchi masikini au zile zinazoendelea duniani. Mfano endapo shimo la choo limechimbwa karibu na vyanzo vya maji, maji yenye vimelea kutoka kwenye kinyesi hupenya kuingia kwenye vyanzo vya maji iwe kisima, mto au chanzo chochote kilicho karibu na makazi ya watu.

Maji haya yakitumiwa bila kutibiwa, hupelekea kutokea kwa maambukizi ya kujirudia rudia.

Endapo mtu atajisaidia karibu na chanzo cha maji au kumwaga kinyesi kwenye maji au kutumia kinyesi cha binadamu kama mbolea, au kumwagilia maji yaliyo na kinyesi kwenye mazao, hupelekea kusambaza kwa maambukizi kwa kula vyakula hivyo.

Mtoto kula mchanga au udongo wenye mayai ya kimelea pia huwa chanzo kingine cha kupata maambukizi kwa watoto wanaoanza kutambaa.

Namna gani mtoto anapata maambukizi ya ugonjwa wa amoeba?

Mtoto anaweza kupata maambukizi ya ugonjwa wa amoeba kwa kunywa maji au kula chakula kilichochanganyika na kinyesi chenye vimelea. Chakula kinaweza kuchanganyika na vimelea kwa njia mbalimbali kama vile;

Kuandaliwa chakula na mtu mwenye maambukizi pasipo kufanya usafi wa mikono kwa maji salama ( mtoto kula tunda lililoshikwa na mwenye maambukizi, au mtoto kula vidole vya mkono ulioshikwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hajanawa mikono kwa maji safi baada ya kujisadia.

Kutumia vyombo vya mtu mwenye maambukizi, mfano kutumia bilauri moja ya kunywea maji, au vyombo vilivyoshikwa na mtu mwenye maambukizi ambaye hazingatii usafi wa mikono,

Kutumia maji ya kunywa yasiyo salama, mfano yaliyochotwa mtoni au ambayo hayajachemshwa,

Kula matunda yaliyosafishwa kwa maji yasiyo salama,

Kunawa mikono kwa maji yasiyo salama,

Kula udongo au mchanga wenye mayai ya kimelea cha amiba,

Vipimo vya Ugonjwa wa amoeba kwa watoto

Baada ya kuchukuliwa historia ya dalili za mtoto na kufanyiwa vipimo vya awali vya mwili, daktari ataagiza mtoto afanyiwe vipimo mbalimbali. Kinyesi kitakusanywa kisha kupelekwa maabara kwa vipimo vya;

  • Kuchunguza uwepo wa vimelea vya amoeba kwa kutumia hadubini
  • Kupima antijeni za amoeba kwenye kinyesi n.k

Matibabu ya Ugonjwa wa amoeba kwa watoto

Matibabu ya ugonjwa wa amoeba hulenga katika kuondoa maambukizi na kuthibiti dalili zilizojitokeza. Dawa inayotumika sana kwa watoto ni metronidazole au Tinidazo (kwa watoto zaidi ya miaka 3) au dawa zingine zinazotumika kwa kuunganishwa zaidi ya moja kama;

  • Paromomycin (Humatin®)
  • Dehydroemetine
  • Tetracycline
  • Diloxanide Furoate
  • Diquinol

Matibabu mengine hutegemea hali ya mtoto, endapo mtoto anahara, utashauriwa kumpa maji ya kutosha au maji ya oral (ORS). Endapo mtoto ameharisha sana pia na ana hali mbaya anaweza kuongezewa maji hospitali.

Inachukua muda gani kupona ugonjwa wa amoeba baada ya kuanza kutumia dawa?

Kwa kawaida inachukua kati ya wiki 1 hadi 3 kwa maambukizi kuisha kabisa mwilini bada ya kuanza kutumia dawa. Hata hivyo dalili zinaweza kupotea kabisa kati ya wiki ya kwanza na pili tangia mtoto ameanza kutumia dawa. Amibiasis nje ya tumbo huweza kuchukua muda mrefu kupona.

Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa amoeba

Sio kila dalili za amoeba humaanisha amibiasis, hii inaongeza umuhimu wa kuonana na daktari kwa uchunguzi na vipimo kabla ya kuanza kutumia dawa. Magonjwa mengine yanayofanana sana dalili na maambukizi ya amoeba kwa watoto ni;

  • Shigellosis
  • Salmonellosis
  • Campylobacteriosis
  • Homa ya enterohemorrhagic
  • Escherichia coli,

Hata hivyo utofauti wa amibiasis na magonjwa haya ni dalili, dalili za magonjwa hayo huanza haraka zaidi ukiliganisha na amibiasis.

Madhara ya ugonjwa wa amoeba kwa watoto

Madhara yafuatayo yanaweza kutokea endapo mtoto hatapata matibabu mapema. Inakadiriwa asilimi 7 hadi 30 ya wagonjwa wanaweza kupta madhara haya wasipopata matibabu.

  • Kutoboka kwa utumbo
  • Kuoza kwa utumbo ( NEC)

Namna ya kumkinga mtoto kupata ugonjwa wa amoeba

Ili kumkinga mtoto na maaambukizi ya amiba, unaweza fanya mambo yafuatayo;

✓ Tenge vyombo vya mtoto na watu wazima mfano vyombo vya kuogea, vya kunywea maji n.k

✓ Nawa mikono wa maji safi baada ya kutoka chooni

✓ Safisha mboga za majani na matunda kwa maji safi kabla ya kuliwa au kupika.

✓ Tumia maji salama yaliyotiwa iodine au chlorine

✓ Jenga choo mbali na vyanzo vya maji

✓ Mfundishe mtoto kutokula mchanga au vidole bila kunawa. Au tumia viziba mdomo ili asile mikono akishika chini



>>>

Rejea za mada hii:

  1.  Amebiasis.https://pedsinreview.aappublications.org/content/23/8/293. Imechukuliwa 07.07.2021
  2.  Rashidul Haque, et al. Entamoeba histolytica Infection in Children and Protection from Subsequent Amebiasis.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1360358/#. Imechukuliwa 07.07.2021



Post a Comment

0 Comments