Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa Gumboro ( Infectious Bursal Diseases) katika ufugaji wa kuku



 Ugonjwa wa Gumboro ( Infectious Bursal Diseases) katika ufugaji wa kuku

Ufahamu ugonjwa wa Gumboro ( Infectious Bursal Diseases) katika ufugaji wa kuku.

Ni ugonjwa utokanao na virusi  viitwavyo ”BIRNAVIRUS" . Ugonjwa huu huwashambulia kuku na ndege wengine wafugwao.

Kuenea/kusambaa kwa ugonjwa;

Kuenea au kusambaa kwa ugonjwa huu wa Gumboro Kutoka banda moja kwenda linginge asilimia kubwa ni Kupitia kinyesi cha kuku anayeumwa.

Dalili za Ugonjwa wa Gumboro

Dalili za Ugonjwa wa Gumboro kwa Kuku ni pamoja na;

  1. Kuku kutapika na kuharisha majimaji.
  2. Manyoya husimama.
  3. Kuku kusinzia na kukosa hamu ya kula.
  4. Kuku kufa sana,Vifo hufikia hadi asilimia thelathini (30%).
  5. Kuku kujidokoadokoa sehemu ya haja kubwa.
  6. Cloaca kuvimba.
  7. Kutokea Vidonda, Chini ya ngozi hasa mapajani vidonda hutokea hasa kwa vifaranga.

Namna ya kukinga na kuzuia ugonjwa wa Gumboro

✓ Safisha banda kwa dawa za kuua vijidudu (Disinfectants).

✓ Wapatie chanjo ya Gumboro vifaranga wakiwa na umri wa wiki 2 na rudia tena wakiwa na umri wa wiki 3 (yaan siku ya 14 na 21)

Tiba za ugonjwa wa Gumboro

Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila kwa msaada zaidi wasiliana na mtaalam au daktari wa mifugo. Asante.!!!





Post a Comment

0 Comments