Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa Wa Homa Ya Ini(Hepatitis): Sababu, Dalili, Matibabu, na Kinga



Ugonjwa Wa Homa Ya Ini(Hepatitis): Sababu, Dalili, Matibabu, na Kinga

Ugonjwa wa homa ya ini ni ugonjwa hatari wa ini ambao husababisha uvimbe na uharibifu wa ini. Ugonjwa huu husababishwa na virusi, kemikali, na magonjwa mengine. Katika makala hii, tutajifunza zaidi kuhusu sababu, dalili, matibabu, na kinga ya ugonjwa wa homa ya ini.

Wakati Ini linapovimba au kuharibiwa huathirika kiutandaji pia,hivo kazi zote zinazofanywa na kiungo hiki muhimu huathiriwa pia, Matumizi ya Pombe kupita kiasi,Sumu(toxins),baadhi ya dawa au matatizo kadhaa ya kiafya huweza kusababisha tatizo la Ini kuvimba(hepatitis).  Soma zaidi hapa.!!

Sababu ya Ugonjwa Wa Homa Ya Ini:

Ugonjwa wa homa ya ini husababishwa Zaidi na virusi wa aina tatu:

  1. virusi vya hepatitis A,
  2. hepatitis B,
  3. Pamoja na hepatitis C. Ingawa kuna aina nyingine kama vile
  4. hepatitis D
  5. na hepatitis E

Vilevile, kemikali, pombe, na baadhi ya dawa zinaweza kusababisha ugonjwa huu wa kuvimba kwa Ini(hepatitis).

Sababu nyingine ambazo huongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa wa homa ya Ini ni pamoja na:

  • Kuchora tatoo au kupasua mwili kwa vifaa visivyo visafi
  • Kupokea damu au viungo vya mwili visivyo safi
  • Kufanya mapenzi bila kinga/condom
  • Kugusana na damu,jasho au maji maji yoyote ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu
  • Kutumia sindano zisizo safi au vifaa vingine vyenye ncha kali n.k

Kwa Ujumla,Njia nyingi ambazo unaweza kupata ugonjwa wa homa ya Ini, zinafanana kabsa na njia ambazo unaweza kupata Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Dalili za Ugonjwa Wa Homa Ya Ini:

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na:

  1. Kupata Homa kali
  2. Kuhisi uchovu sana
  3. Kuhisi Kichefuchefu na kutapika
  4. Kupata Maumivu ya tumbo
  5. Viungo kuuma au kupata muwasho
  6. Kuharisha
  7. Kupoteza hamu ya kula
  8. Ngozi na macho kuwa na rangi ya njano
  9. Mkojo kuwa mweusi n.k

Matibabu ya Ugonjwa Wa Homa Ya Ini (Hepatitis):

Matibabu ya ugonjwa wa homa ya ini hutofautiana kulingana na aina ya virusi vya hepatitis.

• Kwa hepatitis A, hakuna tiba maalum, lakini dalili hupungua kwa muda wa wiki nne hadi sita.

• Kwa hepatitis B na hepatitis C, tiba inapatikana, lakini kadri unavyochelewa kupata Tiba ndivo inavyokuwa ngumu zaidi kupona.

Kinga ya Ugonjwa Wa Homa Ya Ini:

Kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua ili kujikinga na ugonjwa wa homa ya ini, na hatua hizo ni pamoja na:

✓ kupata Chanjo ya Kuzuia ugonjwa wa homa ya Ini,

•Soma Zaidi hapa Kuhusu Chanjo ya ugonjwa wa Homa ya ini

✓ Kuepuka kugusana na damu,jasho,mate au maji maji yoyote ya mwili kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu

✓ Kuepuka ngono isiyo salama au Kutumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi

✓ Kupata chanjo ya hepatitis A na hepatitis B

✓ Kuhakikisha kwamba vifaa vya tiba na vipimo vya damu ni safi

✓ Kuepuka kutumia dawa bila ushauri wa daktari

✓ Kuepuka matumizi ya pombe kabsa au kutumia kwa kiasi kidogo

FAQs:

Je! Ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis) ni hatari kwa afya yangu?

Ndio, ugonjwa wa homa ya ini ni hatari kwa afya yako na unaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa ini ikiwa haikutibiwa.

Je! Ni njia zipi za kujikinga na ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis)?

Kujikinga na ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na kupata chanjo, kuepuka kugusana na damu,jasho, mate au maji maji ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu, kutumia kondomu wakati wa tendo la ndoa, na kuepuka matumizi ya pombe au kutumia kwa kiasi kidogo.

Je! Ni dalili zipi za ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis)?

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na homa kali, kuhisi uchovu sana, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo,ngozi na macho kuwa na rangi ya njano,kukojoa mkojo mweusi n.k.

SOMA ZAIDI HAPA kuhusu Ugonjwa huu wa Homa ya Ini

Ugonjwa Wa Homa Ya Ini(Hepatitis)

Ugonjwa wa Homa ya Ini ni Ugonjwa unaoshambulia kiungo muhimu mwilini kinachojulikana kama INI, ambapo WANAWAKE wakiwa miongoni mwa kundi linaloshambuliwa sana na Ugonjwa huu. Ifahamike kwamba Ini linafanya kazi zaidi ya 500 katika miili yetu ikiwa ile ya kupambana na sumu yaani Untoxification,na kuchuja damu mwilini.

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kufanya ini lisifanye kazi vizuri,au livimbe ambapo hii ndyo huitwa Hepatitis kitaalam,Mfano; Unywaji wa pombe kupita kiasi,maambukizi ya magonjwa, VIRUSI au uwepo wa sumu kwenye damu,vitu hivi vinaweza kuathiri utendaji kazi wa Ini.

MAKUNDI YA VIRUSI VINAVYOLETA HOMA YA INI (HEPATITIS)

Tafiti zinaonyesha kwamba,kwa AFRIKA,Maambukizi ya Homa ya Ini,ndiyo shida kubwa inayosumbua ini kuliko matatizo mengine kwenye Ini.

Kuna Aina Tano;
(1) HEPATITIS A

(2) HEPATITIS B✔️

(3) HEPATITIS C

(4) HEPATITIS D

(5) HEPATITIS E

Ambapo hepatitis B na C zikiongoza kwa kuwa sababu kuu za kusambaa ugonjwa wa homa ya ini na husambaaa kwa njia kuu ya Damu pamoja na majimaji yanayotoka mwilini mwa mgonjwa, mfano jasho,mate,mkojo,machozi,Mbegu za kiume n.k

Hepatitis B peke yake,inakadiriwa kuwa, husababisha vifo kwa Takiribani watu 600,000 hivi kwa kila mwaka kutokana na Takwimu za Vifo DUNIANI. Na zaidi ya watu billion mbili sawa na asilimia 33% ya watu wote Duniani wameshaambukizwa virusi hivi vya Homa ya ini (Hepatitis B)

VIRUSI HIVI HUSAMBAA KWA NJIA GANI (HEPATITIS B NAC)?

Chanzo kikubwa cha kusambaa kwa maambukizi haya ni kwa Njia ya Damu,au majimaji kutoka kwa mgonjwa mfano; jasho lake,mate,mkojo,machozi,mbegu za kiume n.k na Hatari ya virusi hivi ni kwamba vina nguvu ya kuathiri au kushambulia mtu mara 100 zaidi ya virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI.

NJIA AMBAZO MTU ANAWEZA KUPATA VIRUSI HIVI

NB; Njia zote ambazo virusi vya ukimwi husambaa,ndyo njia hizo hizo virusi vya Homa ya Ini Husambaaa.

(1) Mama mwenye virusi hivi anaweza kuvisambaza kutoka kwake kwenda kwa mtoto wakati wa Kujifungua ambapo uwezekano ni mkubwa zaidi ya asilimia 90% kama kusipochukuliwa tahadhari thabiti

(2) Kushiriki tendo la Ndoa na Mtu mwenye virusi hivi vya Homa ya Ini

(3) Kushare vifaa vyenye ncha kali kama wembe,sindano,miswaki n.k

(4) Kuongezewa damu ya Mtu mwenye virusi vya Ugonjwa huu wa Homa ya Ini

MDA AMBAO VIRUSI VYA HOMA YA INI HUWEZA KUISHI VIKIWA NJE YA MWILI

Virusi vya Homa ya Ini vinauwezo wa kukaa Nje ya mwili hadi siku 7 na bado vikawa na uwezo wa kuangia kwa mtu na kumuambukiza ugonjwa huu.

KUNDI LA WATU AMBAO WAPO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU

(1) Watu wanaofanya Ngono zembe na pia wanashiriki kitendo hiki na watu wengi

(2) Watoto wanaozaliwa na mama mwenye ugonjwa huu wa Homa ya Ini

(3) Watu wanaotumia madawa ya kulevyia hasa aina ya Sindano

(4) Watu wanaoshiriki mapenzi ya Jinsia moja hasa wanaume

(5) Mtu mwenye mpenzi au mke mwenye virusi hivi

(6) Wagonjwa wenye magonjwa ya vigo ambao wanapata huduma ya kusafisha damu au kitaalam Dialysis

(7) Watumishi wote wa Afya

DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA INI

✓ kukojoa mkojo wenye rangi kama ya COCACOLA

✓Kupata rangi ya manjano katika maeneo tofauti ya mwili kama macho,mikono au mwili mzima ngozi hubalika rangi na kuleta rangi ya manjano

✓Hali ya kichefuchefu,kutapika,mwili kuchoka sana, na kukosa hamu kabsa ya kula chakula

Kumbuka; Maambukizi ya Ugonjwa wa Homa ya Ini,huweza kuwa chanzo kikubwa cha kuleta Ugonjwa wa Saratani ya Ini.

Ni muhimu sana kupima kwa Ugonjwa huu ili kuwa salama zaidi, hasa kwa makundi hatarishi niliyoyataja hapo juu.

Hitimisho:

Ugonjwa wa homa ya ini ni ugonjwa hatari wa ini ambao husababisha uvimbe na uharibifu wa ini,Ugonjwa huu husababishwa na virusi, kemikali, na magonjwa mengine.

Ni muhimu kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja na kupata chanjo, kuepuka kugusana na damu,mate,jasho au maji maji yoyote ya mwili kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu, na kutumia kondomu wakati wa tendo la ndoa.

Kwa wale walio na dalili za ugonjwa wa homa ya ini, ni muhimu kutafuta matibabu haraka ili kuzuia uharibifu mkubwa wa ini.

KWA USHAURI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KUPITIA NAMBA +255758286584





Post a Comment

0 Comments