Connect with us

magonjwa

UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU(MATUMBWITUMBWI-MUMPS)

Doctor Ombeni

Published

on

123 Views
0 Comments

UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU(MATUMBWITUMBWI-MUMPS)

Ugonjwa wa kuvimba mashavu maarufu kama Matumbwitumbwi,ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Mumps,

Ugonjwa huu huhusisha kuvimba kwa tezi la Mate yaani Salivary gland ambalo lipo karibu na sikio lako,

Ugonjwa wa kuvimba mashavu huweza kuhusisha mtu kuvimba shavu la upande mmoja au kuvimba mashavu yote mawili

CHANZO CHA UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU

Ugonjwa wa kuvimba mashavu au matumbwitumbwi, ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Mumps,hutokana na maambukizi ya Virusi yaani Viral infection ambayo hushambulia kwanza sehemu ya tezi la mate yaani Salivyary gland, ndipo baadae huweza kusambaa katika maeneo mengine.

Mtu huweza kupata virus hawa wa Mumps kutoka kwa mate ya mtu mwenye virusi akiwa anakohoa,kupiga chafya au kwa njia yoyote ile ambayo huweza kuhusisha mate kugusana.

DALILI ZA UGONJWA WA KUVIMBA MASHAVU

– Baadhi ya watu hawaonyeshi dalili zozote baada ya kuambukizwa na Virusi wa mumps, Lakini wengi wao huonyesha dalili ambazo huanza kuanzia wiki 2 mpaka 3 baada ya kupatwa na virusi hawa wa Mumps.

• Dalili ya kwanza kabsa ni mtu kuvimba shavu moja au mashavu yote mawili kutokana na kuvimba kwa tezi la mate(salivary gland)

• Mtu kupata maumivu ya shavu lililovimba

• Mtu kupata maumivu makali wakati wa kumeza kitu chochote au kupiga miayo

• Joto la mwili kuwa juu sana au mtu kuwa na homa

• Mtu kupata maumivu ya kichwa mara kwa mara

• Mtu kupata maumivu ya misuli,joints na viungo mbali mbali vya mwili

• Mwili kuchoka kupita kiasi

• Mtu kukosa kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote n.k

MADHARA YA UGONJWA HUU WA KUVIMBA MASHAVU AU MUMPS NI PAMOJA NA:

– Mtu kuvimba korodani moja au zote mbili hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Orchitis

– Mtu kuvimba ubongo,hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Encephalitis

– Kuvimba kwa ngozi pamoja na uwepo wa maji zaidi kwenye ubongo pamoja na uti wa mgongo,maambukizi ambayo hujulikana kama meningitis

– Mtu kuvimba kongosho,hali ambayo hujulikana kwa kitaalam kama pancreatitis

– Mtu kupoteza uwezo wake wa kusikia kwa sikio moja au yote mawili

– Mtu kupatwa na matatizo mengine ya moyo

– Mwanamke kupatwa na tatizo la mimba kutoka zenyewe hasa kwenye miezi mitatu ya mwanzoni n.k

JINSI YA KUZUIA UGONJWA HUU WA KUVIMBA KWA MASHAVU(MATUMBWITUMBWI AU MUMPS)

✓ Ugonjwa huu huzuiwa kwa njia ya chanjo, ambapo kwa kawaida chanjo yake hutolewa kwenye mfumo wa combined yaani, Measles-mumps-Rubella(MMR),

Dose zake hutolewa mbili yaani;
-Mtoto akiwa na mri wa kati ya miezi 12 na 15
– Pamoja na mtoto akiwa na umri wa kati ya miaka 4 na 6

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

123 Views
0 Comments

Medical Disclaimer

Medical Disclaimer: Taarifa kwenye makala hii ni kwa ajili ya Updates au elimu ya jumla tu na haichukui nafasi ya uchunguzi,Tiba au ushauri wa kitaalamu wa daktari kwa mtu mmoja mmoja. Kama una dharura au tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

LATEST POSTS

magonjwa1 year ago

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba

Ugonjwa wa genital warts,Chanzo,Dalili na Tiba Genital warts ni ugonjwa gani,Soma Zaidi hapa kufahamu Genital warts ni moja ya aina...

magonjwa2 years ago

Vipele Sehemu Ya Siri,Vipele Ukeni, Vipele Kwenye Uume

VIPELE SEHEMU YA SIRI,VIPELE UKENI, VIPELE KWENYE UUME Vipele kwenye Uume: Vipele Kwenye Uume: Chanzo, Dalili na Matibabu Tatizo la...

magonjwa ya wanawake5 years ago

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)

 PID • • • • • PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake) PID NI NINI?  PID...

afyatips1 day ago

Dalili za kidonda cha operation kupona

DALILI ZA KIDONDA CHA OPERATION KUPONA Baada ya kufanyiwa operation, mwili huanza mchakato wa kuponya kidonda mara moja. Mchakato huu...

Utafiti1 day ago

Desogestrel yahusishwa na Kuongezeka kwa Hatari ya uvimbe wa ubongo

Mamlaka ya Dawa na Bidhaa za Afya ya Ufaransa (ANSM) imewaonya wanawake wanaotumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango...

magonjwa5 years ago

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba)

UGONJWA WA BRUCELLA(chanzo,dalili na tiba) Huu ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama brucellosis na chanzo chake ni bacteria wanaojulikana...

magonjwa ya watoto2 years ago

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga

Ugonjwa wa Surua kwa Watoto: Sababu, Dalili, Matibabu na Kinga Ugonjwa wa Surua ni ugonjwa wa kuambukiza sana kwa watoto...

Afya News2 days ago

Vifo vya Watoto Wachanga Katika Mlipuko wa Surua Pennsylvania na Mjadala wa Afya ya Umma

Mlipuko wa ugonjwa wa surua (measles) unaoendelea katika jimbo la Pennsylvania, Marekani, umeendelea kuzua wasiwasi mkubwa baada ya watoto wawili...

Afya News2 days ago

Wauguzi Kenya Wasitisha Mgomo Baada ya Makubaliano na Serikali

Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao wa siku 43 baada ya kufikia makubaliano na serikali kupitia chama chao cha wafanyakazi....

WHO3 days ago

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba

Uvutaji Sigara Unaongeza Uwezekano wa Ugumba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuwa matumizi ya tumbaku yana athari kubwa kwa...

124
0