Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa kwashakoo,chanzo,dalili na Tiba



Ugonjwa wa kwashakoo,chanzo,dalili na Tiba

• Kwashakoo ni Ugonjwa gani?

Kwashakoo ni ugonjwa unaohusisha upungufu mkubwa wa protini mwilini,

Ugonjwa wa kwashakoo kwa kiasi kikubwa huathiri watoto wadogo, watoto ambao wapo kwenye mazingira ambayo hawapati mlo wenye virutubisho vya kutosha ikiwemo proteins,

Watu wenye kwashakoo wanaweza kuwa na chakula cha kula, lakini hakina protini ya kutosha.

Dalili za Ugonjwa wa Kwashakoo

Dalili za ugonjwa wa Kwashakoo ni Pamoja na;

1. Ukuaji duni kwa watoto au Mtoto kudumaa

2. Kuvimba kwenye vifundo vya miguu na miguu kwa ujumla

3. Kuvimba Tumbo au tumbo kujaa

4. Kuwa na mabadiliko mbali mbali kwenye nywele ikiwemo;

  • Nywele kukauka sana,
  • Nywele kunyonyoka au kupoteza nywele
  • Nywele kupoteza rangi yake. n.k

5. Kuwa na Ugonjwa wa ngozi(dermatitis)- tatizo ambalo huhusisha ngozi kuwa kavu,ngozi kubanduka, ngozi kuwa na magamba au mabaka mekundu.

6. Kuongezeka ukubwa au kuvimba kwa Ini, kama dalili ya ugonjwa ambao kitaalam hujulikana kama "fatty liver disease".

7. Misuli kupungua na kuwa dhaifu lakini mafuta huhifadhiwa chini ya ngozi (subcutaneous fat).

8. Kuwa na dalili za tatizo la Upungufu wa maji mwilini(Dehydration).

9. Kukosa hamu ya chakula(anorexia).

10. Mwili kuchoka kuliko kawaida n.k

Madhara ya Ugonjwa wa Kwashakoo

Madhara ya Ugonjwa wa Kwashakoo ni pamoja na;

- Kusababisha udumavu kwenye ukuaji wa watoto(watoto kudumaa)

- Kusababisha tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha sukari kwenye damu(Hypoglycemia).

- Kusababisha tatizo la joto la mwili kushuka zaidi-Hypothermia (low body temperature).

- Kusababisha kiwango cha ujazo wa damu kuwa chini-Hypovolemia (low blood volume), kisha kupelekea matatizo kama vile hypovolemic shock.

- kusababisha tatizo la Electrolyte imbalances hasa kutokana na upungufu wa maji mwilini.

- Kusababisha kinga ya mwili kuwa dhaifu sana, hali ambayo husababisha mwili kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara pamoja na vidonda kuchelewa kupona pale unapopata vidonda.

- Kupata Matatizo kweye Ini ikiwemo;

  • tatizo la Cirrhosis
  • Au Ini kushindwa kufanya kazi(liver failure).

- Kudhoofika  kwa kongosho, hali ambayo huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye umeng'enyaji wa chakula

- Na Wakati mwingine kusababisha Kifo

Chanzo cha Ugonjwa wa Kwashakoo

Kwashakoo ni ugonjwa unaohusisha upungufu mkubwa wa protini mwilini, hivo chanzo kikubwa cha Ugonjwa wa kwashakoo ni upungufu wa Protini mwilini,

Sababu za msingi zinazohusiana na kwashiorkor ni pamoja na:

• Mtu kula vyakula vyenye Wanga nyingi, Katika idadi ya watu ambayo inachukuliwa kuwa kwenye hatari zaidi, haswa maeneo ya Afrika, Amerika ya Kati na Asia ya Kusini-Mashariki, mara nyingi chakula kinachopatikana ni aina ya wanga kama vile:

  • mchele,
  • mahindi
  • au mboga za wanga.

Mazao haya yanaelekea kuwa ya bei nafuu na hupatikana kwa wingi kuliko vyakula vyenye protini nyingi, hasa katika maeneo ya vijijini ambako wengi ni wakulima. Akina mama ambao hawana protini ya kutosha mwilini wanaweza kupitisha tatizo hili la upungufu wa protini kwa watoto wao.

• Kuachishwa kunyonya na kusababisha mtoto kukosa virutubisho vya kutosha. Jina "kwashiorkor" linatokana na lugha ya Ga ya Ghana-Afrika, Ikimaanisha "Ugonjwa ambao mtoto anapata wakati mtoto mpya(mwingine) anakuja."

Hii inaelezea hali ya kawaida ambayo mtoto anayenyonyeshwa anaachishwa haraka ili mtoto mchanga aanze kunyonyeshwa.

Kwa sababu ya uhaba wa rasilimali au kutojua lishe vizuri, au vyote viwli, mtoto anayeachishwa kunyonya hapati lishe ya kutosha, hali ambayo huathiri afya yake,kupelekea ukosefu mkubwa wa virutubisho muhimu kama vile Proteins,kisha kupata magonjwa kama vile Kwashakoo.

• Sababu zingine zinazoweza kuchangia kuwepo kwa Ugonjwa wa kwashakoo ni pamoja na;

  1. Ukosefu wa Virutubisho muhimu kama vile vitamins na madini mwilini
  2. Ukosefu wa Lishe yenye antioxidants.
  3. Aflatoxins - sumu kutoka kwa ukungu ambayo kwa kawaida hukua kwenye mazao katika hali ya hewa ya joto na unyevunyevu.
  4. Uwepo wa vimelea vya magonjwa aina ya Parasites pamoja na magonjwa kama vile; surua, malaria na HIV.
  5. Pamoja na Matatizo mengine mbali mbali ya kimaisha, ikiwa ni pamoja na njaa, vita na majanga ya asili pia huweza kuchangia uwepo wa Ugonjwa wa Kwashakoo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments