UGONJWA WA MASUNDO SUNDO-warts KWA UJUMLA WAKE(soma hapa)

 UGONJWA WA MASUNDO SUNDO-warts KWA UJUMLA WAKE(soma hapa)

UGONJWA WA MASUNDO SUNDO (WARTS)

Huu ni ugonjwa wa Ngozi ambao unasababishwa na virusi waitwao Human papillomaviruses (HPVs).

Virusi hawa wapo wa aina nyingi sana na wanasababisha madhara au ugonjwa katika sehemu husika katika mwili na Mpaka sasa kuna aina Zaidi ya 220 ya virusi hawa wa HPV. Mfano masundosundo yatokeayo maeneo ya haya kubwa na maeneo ya via vya uzazi husababishwa na HPV aina ya 6 na 11, masundosundo ya kwenye kanyagio na kisigino ni HPV aina ya 1.

Masundo sundo ya Ngozi inawapata sana Watoto na vijana,kwa watu wa makamo,wazee wnapata masundosundo kama hayo lakini masundosundo ya maeneo ya njia ya haja kubwa na maeneo ya uzazi wa mwanamke na mwanaume.

Masundosundo kwa Watoto na vijana hua yanaweza kuisha menyewe hata bila dawa na ikumbukwe kwamba kuisha kwa masundosundo hutegemea na uimara wa kinga ya mwili wa muhusika na umri wa mtu husika;hata kwa kwa upande wa kutokea kwa dalili Watoto na vijana wenye kinga nzuri hua inachukua takribani wiki 2 hadi 6 kwa dalili za awali kuonekana;

lakini kwa wazee na watu wenye upungufu wa kinga mwilini kutokana na sababu yeyote inaweza kuchukua miezi kadhaa hata miaka kadhaa kwa dalili kuanza kuonekana.

Maambukizi ya virusi wa HPV ni kutoka mtu kwa mt una inasadikika kwamba ni kwa njia ya migusano au ngono baina ya mgonjwa na mtu asie mgonjwa na virusi hao humuingia mtu kupitia mikatiko midogo midogo ambayo itakuwepo kwa Ngozi au maeneo ya uzazi.

DALILI ZA UGONJWA WA MASUNDOSUNDO

Ugonjwa huu hupelekea mtu kupata vipele au vinundu vigumu vingumu katika Ngozi.masundo sundo haya hutegemea na sehemu yaliyipo na yamepewa na majina kutokana na sehemu vilivyotokea. Kuwepo kwa majina tofauti tofauti hakubadilishi dalili,makali au matibabu yake bali ni katika kuvielezea tu. Matibabu ya aina zote yanafanana kabisa.

Kuna aina kadhaa ya masundosudo kutokana na mionekano yao na sehemu yaliyopo mfano kuna masundosundo ya kawaida ambayo hutokea mikonon,kifuani,tumboni,usoni nk (verruca vulgaris),masundo sundo yatokeayo kwenye viiganja vya miguu na mikono (verruca plantaris),masundosundo yasokua na vinundu au vipele (verruca plana) na masundosundo ya maeneo ya haja kubwa na maeneo ya uzazi (condylomata acuminata).masundosundo tofauti na vinundu au vipele pele vinauaga vinawasha washa mwingine

MATIBABU YA MASUNDOSUNDO

Ugonjwa huu kama yalivyo magonjwa mengine hutibika vizuri sana ,aidha masundo sundo sio lazima yatibiwe kwa dawa kwani mengine yanaweza kuisha menyewe bila hata dawa. Matibabu ya masundosundo kabla ya kufanyika mambo kadhaa hutizamwa kwani madawa au tiba zingine hua ni za gharama na kuna madhara yake pia.

Matibabu ya masundo sundo yapo ya aina mbalimbali kama vile kwa kutumia dawa za kupaka na za kuchoma,kufanya operesheni ya kuvikata,kuviunguza kwa baridi au kuvikata kwa umeme.

Ikumbukwe kwamba tunatoa matibabu ya masundo sundo kama mgonjwa ana mojawapo ya mambo yafuatayo.

1)Kama yamekaa kwa muda mrefu sana (Persistent warts)

2)Kama mgonjwa anataka kuyaondoa kwa sababu za muonekano au kuogopa kusemwa au kunyanyapaliwa (Patient concern for cosmesis or social stigma)

3)Kama  mtu ana upungufu wa kinga mwilini (Immunosuppression)

4)Kama yanamletea maumivu  mgonjwa (Associated pain)

5) Kama yanamkera kera mtu au kumzuia mtu kufanya majukumu yake (Associated with discomfort/functional impairment)

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!