Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa pid kwa mwanaume,Je wanaume wanaweza kuwa na PID?



 Ugonjwa wa pid kwa mwanaume,Je wanaume wanaweza kuwa na PID?

Moja ya Maswali ambayo watu wengi wamekuwa wakiuliza ni kuhusu mwanaume kupata Ugonjwa wa Pid, je inawezekana?

Hapana, Mwanaume hawezi kuwa na Ugonjwa wa PID(Pelvic inflammatory disease),

Hii n kwa Sababu PID ni ugonjwa ambayo huhusisha maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile bacteria kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke,

Kwa Ujumla,Ugonjwa huu wa PID hushambulia mfumo wa Uzazi kwa mwanamke, ikiwa ni Pamoja na;

  • Kizazi(Uterus)
  • Mirija ya uzazi(fallopian tubes)
  • au Vifuko vya Mayai(Ovaries)

PID hutokea wakati bacteria wakipanda kutoka Ukeni kwenda kwenye viungo vya juu vya uzazi, au tunasema upper reproductive organs.

Mara nyingi, bakteria hawa huambukizwa kwa ngono, na magonjwa ya zinaa kama kisonono na chlamydia yanaweza kusababisha PID.

Fahamu pia, inawezekana kwa wanaume kuwa na magonjwa hayo ya Zinaa(Kisonono,chlamydia), na wanaweza kueneza bakteria wanaohusika kuyaeneza kwa mwanamke,

Hivo kumuweka mwanamke kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa haya ya zinaa ambayo pia huweza kupelekea Mwanamke kupata PID.

Hata hivyo, haiwezekani kwa Magonjwa haya ya Zinaa  kusababisha PID kwa wanaume kama inavyoweza kutokea kwa wanawake.

Vitu vya Kuzingatia ni pamoja na;

• Mwanaume kupata Tiba endapo ana magonjwa haya ya Zinaa

• Mwanaume kupata Tiba hata kama haumwi,pale ambapo Mke wake au mwezi wake amagendulika ana Ugonjwa wa PID.

• Mwanamke,Wapenzi wowote ambao umekuwa nao kwa muda wa miezi 6 kabla ya dalili zako kuanza wanapaswa kupimwa na kutibiwa ili kuzuia maambukizi kujirudia au kuenea kwa wengine.

Dalili za Ugonjwa wa PID

Dalili za Ugonjwa wa PID ni Pamoja na;

1. Kupata maumivu karibu na eneo la nyonga au tumbo chini ya kitovu

2. Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

3. Kupata maumivu wakati wa kukojoa

4. kutokwa na damu katikati ya mwezi kabla hedhi na baada ya tendo la ndoa

5. Kupata damu nzito au nyingi wakati wa hedhi(heavy periods)

6. Kupata maumivu makali sana wakati wa hedhi

7. Kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya njano au kijani ambao huambatana na harufu mbaya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments