UGONJWA WA SCABIES,CHANZO,DALILI NA TIBA

 UGONJWA WA SCABIES,CHANZO,DALILI NA TIBA

Scabies, ni ugonjwa wa ngozi unaohusishwa na kuwasha na madoa madogo mekundu kwenye ngozi, yanayosababishwa na utitiri wa kuwasha(itchy mite).

Aina ya Utitiri huu yaani tiny burrowing mite hujulikana kwa kitaalam kama Sarcoptes scabiei.

DALILI ZA UGONJWA WA SCABIES NI PAMOJA NA;

- Mtu kupata muwasho sana kwenye ngozi yake, na sana sana muwasho huu huzidi sana wakati wa usiku

- Kuanza kupata upele kwenye ngozi

- Ngozi kuanza kuwa na madoa doa mekundu

- Na maeneo ya ngozi ambayo huweza kuathiriwa zaidi ni pamoja na;

• Kati kati ya vidole

• Eneo la kwapani

• Kuzunguka kiuno

• Kwenye mikono

• Chini ya miguu kwenye sole

• Kuzunguka maziwa au matiti

• Kwenye sehemu za siri za Mwanaume(Around the male genital area)

• Eneo la matakoni

• Kwenye magoti

• Na kwa upande wa watoto wadogo, sana sana hutokea kwenye kichwa(Scalp), viganja vya mikono pamoja na miguuni.

MATIBABU YA SCABIES

- Zipo njia mbali mbali za kutibu Ugonjwa huu wa Scabies pamoja na vitu vya kuzingatia na kufanya ukiwa nyumbani, ikiwemo swala la usafi wa mwili pamoja nguo zako,

Na kwa upande wa tiba huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali zikiwemo vidonge vya kunywa na Cream za kupaka

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!