Connect with us

afyatips

Ukimeza Big G,inakaa tumboni kwa Miaka 7, Madhara yake ni nini?

Doctor Ombeni

Published

on

 Ukimeza Big G,inakaa tumboni kwa Miaka 7, Madhara yake ni nini?

Baadhi ya Watu wamekuwa wakiamini kwamba,kama ukimeza Big G basi inauwezo wa kukaa tumboni kwako kwa kipindi cha Miaka 7, Je ni kweli?

Ukweli ni kwamba hushauriwi Kumeza Big G baada ya kuona utamu umeisha au umemaliza kuitumia,

Lakini je nini kinaweza kutokea pale ambapo umemeza kipande kidogo cha Big G, Maana watu wanasema Big G huwa haimeng’enywi kabsa tumboni.

SOMA HAPA;

kwanza Big G(Gum) inaweza kutoka kwenye miti yaani tree resin au kutengenezwa na gum base, ambapo kwa asilimia kubwa vitu hivi havifanyiwi umeng’enyaji tumboni kama ilivyo kwa vyakula vya kawaida unavyokula.

Sasa basi kama ilivyo utaratibu wa kawaida wa Mwili, Kama vitu hivi havifanyiwi umeng’enyaji basi husubiri wakati wa Kutolewa Nje kwa Njia ya Haja Kubwa,

Baadhi ya Tafiti zinaonyesha”Endapo umemeza kipande cha Big G(Gum) kitatoka ndani ya Masaa 40 kupitia Njia ya Haja Kubwa, na kwa vile hakimeng’enywi basi kitatoka kama kilivyo” Anasema Mtaalam Mmoja anayejulikana kama Czerwony.

Hivo basi unashauriwa kutokumeza vitu kama hivi, japo vinaweza visikusababishie madhara yoyote Mwilini,

Kumeza kipande Kimoja cha Big G kwa bahati mbaya sio tatizo Ila endapo unameza vipande vingi mara kwa mara ndani ya kipindi kifupi cha Muda,huweza kuleta athari kwenye mfumo wako wa Umeng’enyaji chakula.

Kama unafanya hivi kila siku na mara nyingi zaidi ndani ya siku Moja,inaweza kusababisha tatizo la kuziba kwa Utumbo yaani intestinal blockage,

NENDA HOSPITAL HARAKA KAMA UMEMEZA BIG G(GUM) HALAFU UNAPATA DALILI HIZI HAPA;

1. Unapata Maumivu makali ya Tumbo

2. Kuanza kupata tatizo la choo kigumu pamoja na kujisaidia kwa shida sana(Constipation)

3. Kujihisi Umeshiba Muda wote

4. Tumbo lako kujaa au Kuvimba

5. Kuanza kupata shida ya Kutapika n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

✚

Ushauri,Elimu,Tiba

Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.

Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?

💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

🏆Certified| Doctor from Afyaclass. Maudhui haya ni kwa ajili ya elimu ya jumla ya afya. Unapohitaji ushauri wa kina, uchunguzi, au matibabu binafsi, wasiliana na daktari kupitia namba:+255758286584.Pia tufwatilie kupitia: @Facebook | @Instagram | @YouTube.

2 Comments

2 Comments

  1. Guest Avatar

    Peter

    July 31, 2026 at 10:48 am

    Asante kwa kutoa elimu kwa watu nikiwemo namimi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Guest Avatar

LATEST POSTS

Utafiti24 hours ago

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka

Chumvi yenye Potasiamu Inaweza Kuzuia Vifo Karibu Milioni 3 Kila Mwaka Vinavyosababishwa na Magonjwa ya Moyo na Kiharusi – Utafiti...

Afya News1 day ago

Mtoto Afariki Dunia kwa Surua Marekani, Vifo 3 Vyaripotiwa Wiki Hii

Mtoto mchanga afariki dunia kutokana na surua nchini Marekani, vifo vitatu vyaripotiwa wiki hii Mtoto mchanga nchini Marekani amefariki dunia...

CHANJO1 day ago

Chanjo Mbili Mpya za Ebola Kuongezwa kwenye Majaribio ya Kitabibu Huku Utafiti wa Tiba Ukiendelea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa chanjo mbili mpya zinazofanyiwa utafiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola zinatarajiwa kuongezwa kwenye...

Afya News2 days ago

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke

Bodi ya Dawa nchini Kenya yaonya dhidi ya matumizi ya cetirizine kukaza au kukausha uke. Bodi ya Dawa na Sumu...

magonjwa2 days ago

Sababu ya mikono kufa ganzi

Sababu 12 Za Mikono Kufa Ganzi: DALILI HII INASABABISHWA NA NINI? Mikono kufa ganzi ni hali ambayo mtu hupoteza hisia...

Uzazi&Ujauzito3 days ago

Kubeba mimba baada ya kujifungua

Kubeba mimba baada ya kujifungua JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano...

Uzazi&Ujauzito6 years ago

Je,ninaweza Kupata Mimba baada ya kujifungua na kabla ya kupata hedhi tena?

JE,NINAWEZA KUPATA MIMBA BAADA YA KUJIFUNGUA NA KABLA YA KUPATA HEDHI TENA? Ndiyo, kuna uwezekano wa kupata ujauzito mara baada...

magonjwa2 years ago

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE

TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO,CHANZO NA MATIBABU YAKE Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio...

Utafiti5 days ago

Afya Kidijitali nchini Kenya: Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyobadilisha Huduma Za Uuguzi

Teknolojia ya Akili Bandia (AI) inazidi kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha huduma za afya nchini Kenya, ikiwasaidia wauguzi na...

afyatips5 days ago

Upungufu wa Vitamini D,Dalili Zake, Visababishi na Madhara Ambayo Unaweza Usiyatambue Mapema

Patient Story Via BBC;Sikujua nilikuwa na upungufu wa vitamini D hadi nilipozirai kazini’ Msichana mwenye umri wa miaka 23, Saskia...