UTANDO MWEUPE KWENYE MDOMO
Kuna baadhi ya watu hupatwa na shida hii ya kuwa na utando mweupe mdomoni na Utando huu mweupe huweza kuwa kwa pembeni mwa Lips za mdomo,kuzunguka lips zote,ndani ya mdomo au kwenye Ulimi, je chanzo chake ni nini?
CHANZO CHA UTANDO MWEUPE KWENYE MDOMO NI PAMOJA NA;
1. Maambulizi ya fangasi kwenye mdomo ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Oral candidiasis,
Baadhi ya watu hupata shida hii baada ya kupatwa na mashambulizi ya fangasi mdomoni kwa njia mbali mbali ikiwemo ile ya kufanya mapenzi kwa kunyonya sehemu za siri za mwanamke ambaye ana mashambulizi ya mara kwa mara ya fangasi wa ukeni,
Baada ya kuhamisha maambukizi ya fangasi kutoka ukeni kwenda kwenye mdomo,mwanaume huanza kukauka lips za mdomo, au kupatwa na shida hii ya utando mweupe mdomoni
2. Wakati mwingine utando mweupe mdomoni hutokea kama Povu jeupe,ambapo mate yako mwenyewe ndyo hutengeneza hilo povu kama dalili mojawapo ya Mdomo kuwa mkavu sana(dry mouth),
Hivo hapa unashauriwa kutumia maji ya kutosha angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa sku,kwani kukauka mdomo sana ni mojawapo ya dalili za upungufu wa maji mwilini
3. Kuoverdose baadhi ya dawa, watu wengi hawajui kwamba mtu huweza kuoverdose baadhi ya dawa na kupata shida hii,soma hapa;
Baada ya mtu kuoverdose baadhi ya dawa huweza kupata tatizo la Seizures,ambapo matokeo yake ni mtu kutoa mate mdomoni hadi nje ya Lips zake za mdomo kwa pembeni
4. Mtu kuwa na tatizo la Kifafa yaani epilepsy pamoja na matatizo mengine yanayoshabihiana na kifafa yaani seiziures disorders,
Kama nilivyokwisha kueleza hapo juu, tatizo la Seizures pamoja na matatizo mengine kama Kifafa huweza kupelekea mtu kutoa mate mdomoni hadi nje ya Lips zake za mdomo kwa pembeni na kisha kusababisha hali hii ya kuwa na utando mweupe mdomoni
5. Mashambulizi ya vimelea vya magonjwa mbali mbali kama vile virusi jamii ya RABIES,ambao hutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu,
Moja ya dalili kubwa ya mashambulizi ya virusi jamii ya Rabies ni pamoja na; mtu kupooza misuli ya kwenye koo yaani throat paralysis,hali ambayo hupelekea mtu kushindwa kumeza kitu lakini pia kuongeza uzalishwaji wa mate mdomoni,
Uzalishwaji wa kiwango kikubwa cha mate mdomoni ndyo hupelekea mate kutoka nje ya mdomo kisha kuchanganyika na hewa ya oxygen kwani mtu hawezi kuyameza,mwisho wa siku hutengeneza utando mweupe mdomoni
6. Upungufu wa kinga mwilini au Mtu kukosa uwiano sahihi mwilini kati ya kinga yake ya mwili pamoja na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Bacteria,
Hivo watu wenye magonjwa yanayohusu upungufu wa kinga mwilini kama vile, Saratani,kisukari,Maambukizi ya Ukimwi, au Mama mjamzito huweza kupatwa na shida hii pia ya mdomo kutengeneza utando mweupe.
KUMBUKA; Matibabu ya shida hii ya utando mweupe kwenye Mdomo hutegemea na chanzo chake,hivo kama unashida hii ongea na wataalam wa afya kwanza,ili kupata msaada
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI NA MENGINE PIA,TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!