Utosi wa mtoto kuvimba chanzo chake ni nini? Soma hapa kufahamu

Utosi wa mtoto kuvimba chanzo chake ni nini? Soma hapa kufahamu

Wakati mwingine Utosi wa mtoto kuvimba(bulging or swollen fontanelle) huweza kuwa dalili za matatizo makubwa kama vile;

  • Ugonjwa wa meningitis or encephalitis (maambukizi kwenye ubongo),
  • Tatizo la kuvuja damu kwenye ubongo(cerebral haemorrhage)
  • Tatizo la kichwa kujaa maji/vichwa vikubwa(hydrocephalus),
  • Kuwa na jipu au Sababu zingine ambazo huongeza mgandamizo(pressure) ndani ya ubongo wa mtoto.

Katika Makala hii tumechambua Sababu zinazoweza kupelekea Utosi wa mtoto kuvimba pamoja na maelekezo kwa kina kuhusu Utosi wa mtoto ulivyo.

Chanzo cha Utosi wa mtoto kuvimba

Zipo Sababu mbali mbali za Utosi wa mtoto kuvimba, na Sababu hizo ni pamoja na;
- Mtoto kuwa na tatizo la Hydrocephalus, Tatizo ambalo huhusisha kichwa kujaa maji na kuwa kikubwa zaidi.

Shinikizo la maji(fluid) hupanua ventrikali, hivyo basi kuweka shinikizo zaidi kwenye tishu za ubongo na kusababisha utosi kuvimba,

Hivo wakati mwingine mtoto kuvimba utosi huweza kuwa miongoni mwa dalili za tatizo hili.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha tatizo la hydrocephalus, Tatizo la hydrocephalus huweza kutokea wakati wa kuzaliwa, katika hali ambayo, madaktari huita hydrocephalus ya kuzaliwa "congenital hydrocephalus",

Au huweza kutokea baada ya kuzaliwa, ambapo hali hiyo baada ya kuzaliwa inaitwa "acquired hydrocephalus".

- Mtoto kupata maambukizi mbali mbali, mfano maambukizi kwenye Ubongo, maambukizi kwenye uti wa mgongo kama vile bacterial meningitis,maambukizi ya Rubella n.k

rubella, inaweza kuambukiza kutoka kwa mama mjamzito hadi kwa mtoto, ambapo inaweza kusababisha kuvimba kwa Utosi.

- Kupata tatizo la damu kuvuja kwenye Ubongo(cerebral haemorrhage),

Kuvuja damu kwenye ubongo,Tatizo hili huwatokea zaidi watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na wale wanaopata majeraha au kukosa oksijeni wakati wa kuzaa.

- Matatizo ya kuzaliwa nayo(Birth abnormalities):

Hapa nazungumzia matatizo ambayo huathiri ukuaji na maendeleo ya Ubongo wenyewe, fuvu la kichwa(skull),Uti wa mgongo(spinal cord), au sehemu zingine za mfumo wa fahamu,

ambapo matokeo yake ni kuongeza hatari ya mtoto kuzaliwa na tatizo la hydrocephalus(congenital hydrocephalus) pamoja Utosi kuvimba.

- Majeraha au kuumia(Injuries): Majeraha au kuumia ambako huhusisha ubongo pamoja na uti wa mgongo huweza kusababisha kuvimba ndani ya Ubongo au kuvimba kwa Utosi n.k

- kuwa na Uvimbe(Tumors): Uvimbe kwenye ubongo au uti wa mgongo unaweza kusababisha tatizo la hydrocephalus pamoja na Utosi kuvimba.

- Kiharusi(Stroke); Tatizo la stroke ni adimu sana kutokea kwa watoto lakini linaweza kutokea pia, endapo likatokea huweza kuongeza hatari ya watoto kupata tatizo la kichwa kujaa maji(hydrocephalus) pamoja na Utosi wa mtoto kuvimba.

- Sababu zingine ambazo huweza kuongeza hatari ya mtoto kupata tatizo la Kuvimba kwa Utosi ni pamoja na;

  • Mtoto kupata tatizo la Transient intracranial hypertension:Hali hii hutokea wakati mtoto anapata shinikizo la damu kwa muda katika ubongo, na kusababisha Kuvimba. Wakati mwingine hufuatana na maambukizi.
  • Mtoto kulia sana, Mtoto akilia hutengeneza mgandamizo kwa muda(temporary pressure) ndani ya ubongo wake, hii huweza kuongeza hatari ya utosi wa mtoto kuvimba, Ingawa hii sio sababu ya moja kwa moja ambayo husababisha tatizo hili,hivo mtoto achunguzwe kwanza.
  • Kutapika; Sawa na kulia,Mtoto akitapika hutengeneza pressure ndani ya ubongo au fuvu la kichwa, hali ambayo huweza kuongeza hatari ya Utosi wa Mtoto kuvimba.
  • Chanjo; Watoto mara kwa mara huweza kuvimba Utosi baada ya kupewa baadhi ya chanjo. Sababu kamili ya hii haijulikani, lakini watafiti wanaamini kuwa inahusiana na homa ambayo chanjo inaweza kusababisha kama athari ya Chanjo(side effects).
  • Matumizi ya baadhi ya Dawa pamoja na
  • Upungufu wa Virutubisho muhimu mwilini kama vile Vitamini huweza kuchangia pia tatizo la Utosi wa mtoto kuvimba.
  • Jinsi mwili wa mtoto ulivyowekwa(Body position): wakati mwingine mtoto akiwa amelala chini utosi wake huweza kuonekana kama umetuna au kuvimba, lakini kama baada ya kumuinua na kumsimamisha utosi hauonekani tena kama umevimba hilo sio tatizo ni kawaida.

FAHAMU UTOSI WA MTOTO KWA KINA NA MAMBO YAKUZINGATIA

Utosi wa mtoto mara nyingi watu huutambua kwa ulaini wake pamoja na kubonyea kwake kichwani. Huku asilimia kubwa ya watu wakijua utosi wa mtoto ni mmoja tu hapa mbele,kumbe hata nyuma pia kuna utosi tofauti yake tu ni kwamba utosi wa nyuma hufunga mapema hivo wengi hawaugundui.

-Utosi wa mbele kwa kitaalam hujulikana kama Anterior fontanel

- Na utosi wa nyuma kwa kitaalam hujulikana kama posterior fontanel

JE UTOSI WA MTOTO HUFUNGA BAADA YA MUDA GANI?

Kama nilivyosema hapo juu utosi wa nyuma huwahi kufunga kuliko utosi wa mbele hivo basi;

✓ Utosi wa mbele huweza kufunga kati ya kipindi cha miezi 18 mpaka 24.

✓ Na utosi wa nyuma huweza kufunga ndani ya miezi 3 baada ya mtoto kuzaliwa.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UTOSI WA MTOTO

• Zingatia jinsi unavyomlaza mtoto kuepusha kubonyeza utosi wa mtoto, ambapo wengi wao huona matokeo kama umbo la kichwa cha mtoto kubadilika.

• Epuka kubonyeza utosi wa mtoto kwa vidole vyako mara kwa mara

• Epuka kupitisha kitu chenye ncha kali kwenye utosi wa mtoto au karibu na utosi wa mtoto

• Zingatia kumpaka mtoto mafuta kichwani ikiwemo eneo la utosi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!