Ticker

6/recent/ticker-posts

VIFAA VYA KUJIFUNGULIA(MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA) INDIVIDUAL BIRTH PREPAREDNESS-IBP



 VIFAA VYA KUJIFUNGULIA(MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA) INDIVIDUAL BIRTH PREPAREDNESS-IBP

Maandalizi ya kujifungua ikiwemo Vifaa vya Kujifungulia ni package muhimu sana ambayo mama mjamzito anatakiwa kuiyelewa vizuri sana, maandalizi haya ya kujifungua kwa kitaalam tunaita INDIVIDUAL BIRTH PREPAREDNESS-IBP

Moja ya maswali ambayo wakina mama wengi wajawazito wamekuwa wakiniuliza mara kwa mara ni kuhusu vifaa vya kujifungulia,

Wakiwa na maana ni vitu gani hutumika au vitu gani vyakuandaa wakati mama mjamzito anakwenda kujifungua.

Mbali na kwamba siku hizi mambo yamerahisishwa zaidi, unaweza kupewa kit au Begi ambalo linapackage ya vitu vyote muhimu vinavyohitajika wakati wa kujifungua.

lakini bado haitoshi, maana kiti hizi hazina vitu vyote, hivo bado kuna vitu utatakiwa kuvifahamu na kuandaa mwenyewe kabla ya kwenda kujifungua.

MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA NI YAPI?

Maandalizi ya kujifungua huhusisha vitu vingi ila watu wengi wamejikita kwenye vifaa peke yake, ila baadhi ya vitu hivo ni pamoja na;

• Fahamu mapema ni sehemu gani au hospital gan utakwenda kujifungua kabla ya muda kufika

• Unashauriwa kuweka mambo ya familia yako sawa ikiwemo nani atabaki na familia yako kipindi umeenda hospitalini

• Andaa Usafiri wako mapema ambao utakubeba kwenda hospitalini muda ukifika

• Weka akiba ya pesa kwa ajili ya Emergence yoyote ile

• Pia unatakiwa kufahamu kabsa endapo changamoto ya damu imetokea ni watu gani wa haraka wanaweza kukusaidia kupata damu ambayo inaendana na yakwako, ndyo maana ya kupima blood group mapema,

mbali na changamoto zingine kama mambo ya kutofautiana rhesus factor n.k ambayo yanahitaji mama mjamzito kuchomwa sindano ya anti-D pamoja na huduma zingine,

Pia ni lazima ufahamu watu wa karibu ambao wanauwezo wa kukupa damu kwa haraka zaidi pale ambapo changamoto ya kupata damu imetokea.

• Weka vitu vyako pamoja na karibu ambavyo utatakiwa kwenda navyo hospitalini, ikiwemo KADI YAKO YA MAHUDHURIO YA KLINIKI, NGUO n.k, ili kukusaidia kutokusahau kitu chochote wakati unakwenda hospitalini

• Vifaa vyote vya kujifungulia(maelezo zaidi hapo chini)

VIFAA VYA KUJIFUNGULIA NI PAMOJA NA;

- Andaa nguo zako za kuvaa ikiwemo dela au Gauni la kuvaa wakati unasubiria kwenda kujifungua, soks zako na za mtoto

- Andaa chupi safi za kuvaa, na hapa unashauriwa kuandaa chupi zenye material ya pamba ambazo huweza kufyoza damu au unyevu kwa haraka zaidi.

- Andaa nguo za kumfunika mtoto ambapo mara nyingi inakuwa ni kanga safi n.k

- Mpira ambao unasaidia kuzuia uchafu wakati unajifungua ambao kwa kitaalam hujulikana kama mackintosh

- Gloves za kuvaa mikononi angalau pair NNE, na hapa zinatumika aina ya Gloves inayojulikana kama Surgical gloves

- Nyembe za upasuaji maarufu kwa jina la Surgical blades

- Gauze pamoja na pamba

- Vibanio vya kubana kitovu cha mtoto ambavyo hujulikana kama umbilical cord clamp

- Nyuzi ambazo huweza kutumika kushona,wakati umeongezewa njia au upasuaji.

- Beseni la kuwekea vitu

- Syringe na needle zake

- mafuta laini kama vile mafuta ya nazi n.k

- Taulo za kike maalumu kwa ajili ya uzazi ambazo hujulikana kama maternanity pad

- Pia kunaweza kuwa na zile dawa muhimu kama vile; Oxyctocin,Misoprostol, magnessium sulphate n.k

Soma zaidi hapa: MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA

KWA USHAURI ZAIDI, ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Post a Comment

0 Comments