Ticker

6/recent/ticker-posts

WHO yataka uwekezaji zaidi kwenye chanjo ya kipindupindu



WHO yataka uwekezaji zaidi kwenye chanjo ya kipindupindu

Mkuu wa Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO ametoa wito wa kuongezwa uzalishaji wa chanjo ya kipindupindu, akiangazia kile alichokielezea kuwa upungufu mkubwa kabisa wa chanjo hiyo uliwenguni.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kupitia ukurasa wa X kwamba, visa 307,433 vya kipindupindu na vifo 2,326 vimeripotiwa katika mataifa 26 hadi Julai 28, ingawa udhibiti wake unazidi kuathiriwa na upungufu mkubwa wa chanjo.

Nchi 18 zimeagiza dozi milioni 105 tangu mwezi Januari, lakini ni dozi milioni 55 tu zilizotengenezwa.

Ghebreyesus amehimiza uwekezaji zaidi utakaosaidia kuongeza uzalishaji wa chanjo lakini pia kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na usafi kwa ujumla ili kuzuia milipuko zaidi ya kipindupindu.



Post a Comment

0 Comments