Chanzo cha Alama nyeusi kwapani na Jinsi ya kuondoa

 Chanzo cha Alama nyeusi kwapani na Jinsi ya kuondoa Alama nyeusi Kwapani(Ngozi kuwa nyeusi kwapani)

Je ngozi ya kwapani ni nyeusi sana au ina alama nyeusi?

Ni kweli kwamba tunaweza kutumia muda mwingi kwenye kunyoa nywele za kwapani,kuoga na kutumia vitu kama deodorant ili kuondoa harufu mbaya kwapani,

ila tunaweza tusizingatie sana alama nyeusi au ngozi kuwa nyeusi kwapani,

Japo kwa Wanawake wengi zaidi hujali sana muonekano wa kwapa hata wakati mwingine kukereka zaidi na hata kutafta msaada pale wanapoona weusi zaidi kwenye ngozi ya kwapani.

JE NI NINI CHANZO CHA NGOZI YA KWAPANI KUWA NYEUSI ZAIDI?

Hii inaweza kuhusishwa na maswala ya kigenetics, aina ya products unazotumia kama vile mafuta,sabuni,deodorant n.k,

Lakini wakati mwingine hizi zinaweza kuwa dalili na Ishara za tatizo kiafya,

• Jambo muhimu zaidi kujua kuhusu makwapa meusi ni kwamba wakati mwingine yanaweza kuhusiana na kisukari(diabetes),

Hiyo inaweza kuwa dalili ya kwanza kwa mgonjwa ambaye hapo awali hakuonyesha dalili zozote za Kisukari

• Tatizo la rangi ya ngozi(Skin pigmentation disorder) ambalo hujulikana kama Acanthosis nigricans,

Acanthosis nigracans ni tatizo ambalo huhusisha Hali ya ngozi kuwa na mabaka meusi au weusi kutokea kwenye maeneo ya ngozi yenye mikunjo mwilini pamoja na mistari.

• Sababu zingine ni kama vile;

-Za kiGenetics

- Tatizo la Polycystic ovarian syndrome (PCOS),

Kama unaona tatizo hili la ngozi ya kwapani kuwa nyeusi zaidi halafu inaambatana na matatizo mengine kama vile;

Hedhi kubadilika au kutokueleweka(irregular menstrual cycles), nywele kuwa nyingi zaidi kwenye maeneo mbali mbali mwilini, Uzito kuongezeka n.k,

basi kuna uwezekano mkubwa una tatizo la PCOS

- Tatizo la Allergy/Mzio kwenye ngozi(Allergic contact dermatitis)

- Kuwa na Tatizo la Upele au rashes kwenye ngozi

- Kuwa na tatizo la Post-inflammatory hyperpigmentation

- Tatizo la Psoriasis

- Tatizo la Kuvuja jasho kupita kiasi, hii pia huweza kupelekea weusi kwenye ngozi ya kwapani

- Ngozi kuwasha,kuvimba,kuwa na upele n.k baada ya kunyoa nywele eneo hili

- Kuwa na Hali ya msuguano mara kwa mara Kwapani kutokana na kuvaa nguo za kubana sana eneo hili

- Aina ya material kama vile Manukato, rangi na vihifadhi vinavyotumika kwenye deodorant, mafuta,Sabuni, shaving creams n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Tiba ya Kwanza kabsa ni Kujua chanzo cha tatizo, kama nilivyoeleza hapo juu baadhi ya Sababu,

hivo kuna umuhimu wa kuonana na wataalam wa afya kwanza ili kujua chanzo cha shida yako,kisha kupata Tiba Sahihi zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!