Chanzo Cha Macho Kupoteza Nguvu Ya Kuona

 CHANZO CHA MACHO KUPOTEZA NGUVU YA KUONA

Zipo sababu nyingi ambazo huweza kuchangia macho kupoteza nguvu ya kuona na sababu hizo ni kama vile;

- Tatizo la Diabetic Retinopathy, shida hii hutokana na ugonjwa wa kisukari, ambapo ugonjwa huu wa kisukari huleta madhara makubwa hadi kwenye mishipa ya damu ndani ya Retina,

hali ambayo huchangia macho kupoteza uwezo wake wa kuona

Na ndyo maana baadhi ya wagonjwa wa kisukari wanapatwa na tatizo la macho kutokuona vizuri pia.

- Kuumia kwenye macho(Injury), Sababu hii huweza kusababisha macho kupoteza uwezo wake wa kuona kwa gafla kulingana na jinsi mtu alivyoumia kwenye macho.

- Kuvimba kwa Conjunctiva yaani Conjunctivitis, kuvimba kwa Cornea yaani Keratitis n.k vyote hivi huweza kusababisha macho yako kupoteza nguvu au uwezo wa kuona.

- Tatizo la Age-Related Macular Degeneration, ambapo tatizo hili la macho kupoteza nguvu au uwezo wake wa kuona hutokana na umri mkubwa au uzee,

Mtu mwenye umri mkubwa au mzee huweza kupata shida ya macho kutokuona vizuri

- Tatizo la Refractive Errors, ambapo huhusisha shida ya kuona karibu yaani myopia (near-sightedness), shida ya kuona mbali yaani hyperopia (farsightedness), pamoja na tatizo la macho kutokuona vizuri mbali wala karibu yaani astigmatism (distorted vision at all distances).

- Tatizo la Amblyopia au kwa lugha nyingine hujulikana kama Lazy Eye, Tatizo hili la macho huaathiri zaidi uwezo wa kuona kwa watoto wadogo,

Na tatizo hili hutokana na macho pamoja na Ubongo kutokufanya kazi vizuri kwa kushirikiana hali ambayo hupelekea uwezo wa kuona kwa jicho moja kupungua sana,

- Ugonjwa wa Presha ya macho ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Glaucoma.

SOMA HAPA ZAIDI: Ugonjwa huu wa presha ya macho(Glaucoma)

Lakini pia hata presha yakawaida(high blood pressure) mbali na hii ya macho huweza kuathiri pia uwezo wa macho kuona vizuri.

- Ugonjwa wa mtoto wa jicho au kwa kitaalam hujulikana kama Cataract.

Ugonjwa huu huhusisha uwepo wa kitu kama wingu kwenye lensi za macho, na ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza duniani kwa kusababisha Upofu wa macho.

SOMA HAPA ZAIDI: Ugonjwa huu wa mtoto wa jicho(Cataract)

- Tatizo la Eye strain, ambapo huhusisha misuli ya macho kuvuta zaidi kutokana na sababu mbali mbali kama vile; kuangalia kwenye SCREEN kwa muda mrefu sana, hali ambayo huweza kusababisha macho kupoteza nguvu ya kuona.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!