CHANZO CHA TATIZO LA FLAT FEET KWA WATOTO
Flat feet kwa mtoto ni tatizo ambalo huhusisha sehemu ya chini ya mguu kuwa sawasawa(flat) hali ambayo husababisha sole nzima ya mguu wa mtoto kugusa chini kwenye aridhi.
Sehemu ya chini ya mguu inakuwa sawa sawa au flat kama kwenye picha hapo.
Tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Flat feet au Pes planus pamoja na fallen arches,
CHANZO CHA TATIZO LA FLAT FEET KWA WATOTO
Tatizo hili huwapata watoto wengi kutokana na mifupa yao pamoja na Joints kuwa flexible sana,sehemu ya chini ya miguu iliyoingia ndani inayojulikana kama Foot's arch kutokutengenezwa au kupotea(collapses),
Kuchukua muda mrefu kwa Tendons kukaza na kutengeneza sehemu ya chini ya mguu iliyobonyea au Foot's arch.
Pia Vinasaba vya Tatizo hili huweza kurithiwa(Hereditary), na kwa jamii zenye tamaduni ya watu kutokuvaa viatu kabsa, Watoto wao huwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupatwa na tatizo hili la Flat Feet.
- Tatizo hili halisababishi maumivu ya aina yoyote kwa mtoto, japo huweza kusababisha mtoto kushindwa kutembea vizuri.
MATIBABU YA TATIZO HILI LA FLAT FEET KWA WATOTO
Endapo mtoto wako ana shida hii,mpeleke hosptal kwa ajili ya uchunguzi na matibabu stahiki.
Mtoto anaweza kupimwa uzito wake,pamoja na kufanyiwa vipimo vingine kama vile X-ray ya mguu n.k.
- Mtoto anaweza kuchongewa sole ambayo hujulikana kama Arch support insoles.(kama kwenye picha hapo juu)
- Kufanyiwa mazoezi ambayo hujulikana kama Stretching exercises.
- Pamoja na Kupewa viatu ambavyo ni Supportive shoes. Viatu hivi sio kwa ajili ya kurekebisha mguu lakini vitamsaidia mtoto kutokupata madhara zaidi.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!