Chanzo cha Tatizo la Macho kuwa na Makengeza(squint eyes)
Tatizo la MaKengeza huhusisha hali ya macho kutokulingana vizuri, Na tatizo hili hujulikana kama Squint au Strabismus,
Hii kwa kawaida hutokea kwa sababu misuli inayodhibiti mwendo wa jicho na kope,pamoja na misuli ya nje ya macho, haifanyi kazi kwa pamoja,
matokeo yake, macho yote mawili hayawezi kutazama sehemu moja kwa wakati mmoja.
Inaweza pia kutokea kutokana na jeraha au shida kwenye ubongo, Hali ambayo huathiri uwezo wa macho kufanya kazi kwa pamoja n.k.
AINA ZA TATIZO HILI LA MAKENGEZA
1.Hypertropia: Wakati jicho linageuka juu
2. Hypotropia: wakati jicho linageuka Chini
3. Esotropia: wakati jicho linageuka ndani
4. Exotropia: Wakati jicho linapoelekea nje
DALILI ZA MAKENGEZA KWA WATOTO
Dalili na Ishara ya tatizo la Makengeza inaonekana wazi tangu utotoni.
- Jicho moja haliangalii moja kwa moja mbele.
- Kukodolea macho kidogo kunaweza kutoonekana sana
- Macho yote mawili kushindwa kutazama Sehemu Moja kwa Wakati mmoja.
KUMBUKA; wakati mwingine uchovu kwa Mtoto,Kuumwa,au Usingizi huweza kuonekana kama macho ya mtoto yana Kengeza,Hivo ni vizuri kuchunguzwa zaidi.
- Ikiwa mtoto amefumba jicho moja huku lingine kafumbua, au anainamisha kichwa chake anapotazama vitu, hii inaweza kuwa ishara ya kuona vitu mara mbili na uwezekano wa kuwa na shida ya makengeza ni Mkubwa. Hivo ni nzuri zaidi kuonana na daktari.
Kwa kawaida Tatizo hili la MAKENGEZA,hutokea tangu mtoto anazaliwa, na huonekana Zaidi kwa mtoto baada ya kufikisha Umri wa miezi 3 na kuendelea.
- Kuwa na Jicho kama La kukonyeza au Kutazama kama mtu ambaye kachoka Sana au mvivu(Lazy eye)
CHANZO CHA SHIDA HII YA MAKENGEZA
Tatizo la Makengeza Mtoto huzaliwa nalo, Ila kwa Ujumla zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kupelekea mtu kupata shida hii, kama Vile;
• Shida ya kurithi au kuwa kwenye Familia yenye tatizo hili
• Kupata jeraha au Ajali yoyote,
• Kupata Ugonjwa ambao huweza kuathiri macho,Ubongo n.k
• Kuwa na shida ya kutokuona kwa muda mrefu
• Jeraha kwenye mishipa ya fuvu.
• Tatizo la Hydrocephalus pia huweza kuathiri mpaka macho ya mtoto na kupelekea shida hii ya Kengeza
Hydrocephalus ni hali ambayo huhusisha uwepo wa maji mengi(cerebrospinal fluid) ambayo hujilimbikiza ndani na karibu ya ubongo.
• Baadhi ya maambukizi ya virusi, kama vile vya surua, yanaweza kusababisha shida hii. N.K
MATIBABU YA TATIZO HILI,
Tatizo hili huweza kuhusisha Tiba zaidi ya Moja,kulingana na chanzo husika na hali ya Tatizo ilivyo;Mfano;
✓ Kutumia Miwani maalum kama Mtu anapata shida ya Uono
✓ Kuchoma sindano yaani Botulinum toxin injection, au botox:
Sindano hii huchomwa kwenye Misuli eneo la Surface ya jicho
✓ Vision therapy: Ili kusaidia kuongeza Ushirikiano kati ya macho na Ubongo,Kuongeza uwezo wa kudhibiti Misuli na kuboresha focus ya Macho.
✓ Huduma ya Upasuaji n.k
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!