CHANZO CHA TATIZO LA MASHAVU YA UKE KUWA MAREFU KULIKO KAWAIDA

 CHANZO CHA TATIZO LA MASHAVU YA UKE KUWA MAREFU KULIKO KAWAIDA

Hili ni tatizo ambalo huhusisha mashavu ya uke kuwa makubwa zaidi kuliko kawaida au kuongezeka ukubwa, na huwapata baadhi ya Wanawake,kwa kitaalam tatizo hili hujulikana kama Labial Hypertrophy,

ambapo huhusisha mashavu ya uke kukuwa na kuongezeka ukubwa,hapa nina maana ya Labia majora,na labial Minora,vyote kwa pamoja.

DALILI ZA TATIZO HILI LA MASHAVU YA UKE KUWA MAREFU KULIKO KAWAIDA

- Kama hakuna ukuaji mkubwa zaidi au ongezeko kubwa zaidi,ni vigumu sana mwanamke kupata dalili zozote za tofauti, ila kama mashavu ya uke yamekuwa makubwa zaidi,mwanamke huweza kupata dalili kama hizi hapa chini;

• Mwanamke Kuona hali ya kutuna kuliko kawaida kwa nguo akiwa amevaa hasa nguo zake za ndani

• Kupata shida ya kujisafisha maeneo ya ukeni, hii hutokea baada ya mwanamke kupata hisia kali akishika maeneo haya,hivo kuyakwepa,

hali ambayo hupelekea uchafu kujificha kwenye mikunjo hasa wakati wa period au hedhi,hali ambayo huweza kusababisha mwanamke kupatwa na maambukizi ya magonjwa yasioisha

• Hali ya kutekenywa ukeni, hii hutokea endapo mashavu ya uke yamekuwa makubwa zaidi, ambapo hupelekea msuguano mpaka kwenye nguo yako ya ndani hasa wakati wa kutembea,na wakati mwingine hupelekea hali ya miwasho pia

• Mwanamke kutokuwa comfortable wakati wa shughuli mbali mbali kama vile wakati wa kuendesha baiskeli,kupanda farasi n.k pamoja na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

CHANZO CHA TATIZO HILI LA MASHAVU YA UKE KUONGEZEKA UKUBWA

Mpaka sasa Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo hujulikana ya kutokea kwa shida hii,ila kuna baadhi ya sababu zimeonekana kuongeza uwezekano wa kutokea kwa tatizo hili kwa baadhi ya Wanawake kama vile;

1. Tatizo la kigenetics,ambapo mwanamke huzaliwa tayari akiwa na shida hii

2. Hali ya vichocheo vya Estrogen pamoja na vichocheo vingine au hormones zingine za kike ambazo huzalishwa kwa kiwango kikubwa zaidi wakati wa balehe

3. Wakati wa Ujauzito,ambapo Mtiririko wa Damu(Blood flow) huwa mkubwa zaidi kuelekea maeneo ya via vya uzazi ikiwemo ukeni,

Hii huweza kuongeza presha na kusababisha shida hii

4. Mwanamke kupatwa na majeraha au ajali ambazo huhusisha kuumia kwenye mashavu ya ukeni

5. Na wakati mwingine baadhi ya maambukizi ya magonjwa sehemu za siri kama vile Fangasi,Magonjwa ya zinaa n.k huweza kuchangia Mwanamke kupatwa na tatizo hili la Mashavu ya uke kuwa makubwa kuliko kawaida.

MATIBABU YA TATIZO LA MASHAVU YA UKE KUWA MAKUBWA KULIKO KAWAIDA

- Matibabu hutegemea na chanzo husika Pamoja na ukubwa wa tatizo hili,ila kwa ujumla wake kuna matibabu ambayo huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali Pamoja na huduma ya upasuaji ambayo kwa kitaalam hujulikana kama LABIOPLASTY.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!