Chanzo Cha Tatizo La Miguu Kuvimba Wakati Wa Ujauzito Na Tiba Yake

 CHANZO CHA TATIZO LA MIGUU KUVIMBA WAKATI WA UJAUZITO NA TIBA YAKE

Miguu kuvimba,hii ni shida ambayo huwapata wanawake wengi pindi wakiwa Wajawazito,tatizo hili ni la kawaida kwa mama mjamzito,

japo endapo mama mjamzito anavimba miguu kupita kiasi,mikono na uso apimwe pia Presha pamoja na uwepo wa protein kwenye mkojo,endapo vyote hivi vipo hizo sio dalili njema,ni dalili za kifafa cha Mimba,hivo matibabu na huduma zaidi huhitajika kwa mama huyu.

CHANZO CHA TATIZO LA MIGUU KUVIMBA WAKATI WA UJAUZITO

Shida ya miguu kuvimba wakati wa ujauzito huweza kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo;

- Mabadiliko ya vichocheo mwilini hasa kuongezeka sana kwa kichocheo aina ya Progesterone kwenye miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito yaani First Trimester

- Mwili kukusanya kiwango zaidi cha Maji kipindi cha ujauzito kwa lengo la ulinzi na kusupport mtoto anayekuwa tumboni,

- Mara nyingi wakina mama wajawazito huvimba miguu hasa ujauzito ukiwa na umri mkubwa kutokana na uzito wa mtoto aliyetumboni kuongezeka pamoja na kuongeza mgandamizo au presha zaidi kwenye eneo la chini yaani miguuni,

- Mgandamizo huu au presha hii huweza kupunguza mzunguko wa damu pamoja na kuongeza kiwango cha maji kujikusanya mahali pamoja hasa eneo la chini yaani miguuni kisha kusababisha tatizo hili la kuvimba miguu wakati wa ujauzito,

KUMBUKA; Kiwango hiki cha maji kilichozidi(extra fluid) hujikusanya zaidi eneo la chini ya mwili kwenye miguu na kusababisha miguu kuvimba,na hali hii huzidi zaidi kipindi cha joto au Mama mjamzito akisimama kwa muda mrefu

MAMBO YAKUFANYA KAMA UNA TATIZO HILI LA KUVIMBA MIGUU KIPINDI CHA UJAUZITO

• Epuka tabia ya kusimama eneo moja kwa muda mrefu au epuka kusimama kwa muda mrefu

• Inua miguu yako na iweke kwenye sehemu iliyoinuka kama kwenye mito ukiwa umelala

• Punguza matumizi ya chumvi nyingi kwenye chakula chako cha kila sku

• Hakikisha unakunywa maji ya kutosha angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa siku

• Epuka matumizi ya vinywaji vyenye Caffeine

• Hakikisha unavaa nguo ambazo hazibani mwili,vaa nguo zinazoupa mwili nafasi kama Madira n.k

• Epuka kuvaa viatu virefu, epuka matumizi ya mkanda unaobana tumbo lako n.k

• Epuka kukaaa kwa muda mrefu

• Pendelea kulala ubavu hasa ubavu wako wa kushoto

• Fanya mazoezi mbali mbali ya mwili,usiwe mtu wa kukaa tu mda wote

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!