Chanzo cha tatizo la Mtoto mchanga Kukosa Choo na Tiba Yake
Kama huoni mtoto wako akijisaidia kabsa,hiki ndyo chanzo cha Mtoto mchanga kukosa choo.
Chanzo cha tatizo la Mtoto mchanga Kukosa Choo na Tiba Yake
Baada ya mtoto kuzaliwa huanza kunyonya maziwa ya mama yake, na baada ya muda huanza kujisaidia haja ndogo na haja kubwa pia. Lakini kukaa kwa muda mrefu bila mtoto kupata choo huweza kuleta mashaka hata kwa mama wa mtoto pia.
Swala la mtoto kukosa choo kwa muda mrefu huweza kusababisha mtoto kulia lia mara kwa mara, Mtoto kupata maumivu ya tumbo,tumbo kujaa n.k
CHANZO CHA TATIZO LA KUKOSA CHOO KWA WATOTO
Wengine tatizo la kukosa choo kabsa, huanza na haja kubwa kuwa ngumu sana wakati wa kujisaidia, Kujisaidia kinyesi kama cha mbuzi na baadae hali ya kukosa choo kabsa hujitokeza.
Watoto wadogo sana huweza kupatwa na shida hii, Watoto ambao ni kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka mitano pia huweza kusumbuliwa na shida hii.
Maziwa ya mama yanavirutubisho vingi zaidi(So nutritious), hali ambayo huweza kupelekea muda mwingine mwili wa mtoto kufyonza Kila kitu na kuacha kiasi kdogo sana kupita kwenye mfumo wa umeng'enyaji chakula,
Hii pia huweza kusababisha mtoto wako kukosa Choo,
Pia wakati mwingine hunyonyeshi mtoto vizuri akashiba, hawezi kujisaidia maana hana cha kutoa Nje.
Lakini pia Wakati mwingine inaweza kuwa tatizo kubwa kama kuziba Njia ya haja kubwa,ambayo hii huweza kutokea toka mtoto anazaliwa hapati choo, kuambatana na tumbo la mtoto kuvimba n.k
DAWA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO
- Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutatua tatizo hili kulingana na Umri wa mtoto, Mfano;
Kwa watoto ambao tayari wanakula vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama pekee, hushauriwa ;
• kula matunda ambayo yana nyuzi nyuzi kama maembe,machungwa na matunda yenye kiwango kikubwa cha maji kama matikiti maji,
• Watoto kunywa kiwango kikubwa cha maji kwa siku
• Watoto kuepuka kubana kinyesi kila mara wanapohisi haja kubwa
• Lakini pia kuna njia ya kumassage tumbo la mtoto, hali ambayo itamsaidia mtoto kujisaidia kwa haraka zaidi.
Kama Mtoto hapatu choo Kabsa unaweza kuonana na wataalam wa afya hasa wa mambo ya Watoto kwa ajili ya Msaada zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!