Chanzo cha tatizo la Penile Vascular Insuffiency Kwa WANAUME,Pamoja na Dalili Zake
Chanzo cha tatizo la Penile Vascular Insuffiency Kwa WANAUME,Pamoja na Dalili Zake
Tatizo hili hujulikana pia kama Venous leak, venogenic erectile dysfunction au penile venous insufficiency,
Tatizo hili huhusisha vimishipa vidogo vya damu hasa aina ya Veins kwenye uume, ambapo ni pamoja na Kuvuja kwa vena, vena kutokufanya kazi vizuri au upungufu wa vena kwenye uume,
Na asilimia kubwa,madhara ya tatizo hili huhusisha uume kushindwa kusimama vizuri, upungufu wa nguvu za kiume(Erectyle dysfunction) n.k
CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?
Shida ya mishipa hii huweza kuchangiwa na Sababu mbali mbali kama vile kuumia(trauma), kuwa na tatizo la Varicose Veins kwenye eneo hili, au sababu za kigenetics.
Baadhi ya Takwimu huonyesha kwamba shida hii huweza kuhusisha pia mishipa ya arteries(Arterial insufficiency):
ambapo Asilimia 12% hutokea kwa Wanaume wenye umri wa chini ya miaka 45, na asilimia 19.6%(mild) hutokea kwa wanaume wenye zaidi ya miaka 45,
Na Asilimia 5.9% ya Wanaume ambayo hupata Venous leakage hali yao huwa mbaya Zaidi(Severe).
DALILI ZA TATIZO HILI LA Penile Vascular Insuffiency
- Kwa Wanaume wengi wenye tatizo hili hupata tatizo la Uume kushindwa kusimama vizuri hata kwenye Umri mdogo
- Uume kushindwa kusimama vizuri,Uume kushindwa kusimama kabsa, uume kusimama lakini kwa muda mfupi tu mpaka ufanyiwe constant manual stimulation ndyo huendelea kusimama
- Uume kupungua zaidi tofauti na hapo awali
- Uume kushindwa kusimama vizuri wakati wa asubuhi(Loss of quality Morning erections)
- Uume kushindwa kusimama vizuri hata kama umetumia dawa mbali mbali kama vile sildenafil n.k
- Wakati mwingine kwa baadhi ya Wanaume hutoa Mbegu za kiume au Maji maji kama mbegu ambayo hutoka mara kwa mara kwenye Uume hata wakiwa katika hali ya kawaida ambayo sio ya kufanya Mapenzi.
MATIBABU YA TATIZO HILI
• Kama shida ni vimishipa hivi vimepasuka, lazima viunganishwe au kufanyiwa Ligation, ambapo hapa matibabu ya Upasuaji yatahusika,
Lakini pia unashauriwa kubadilisha mtindo wako wa Maisha ikiwemo;
- Kuacha kabsa Tabia ya Kufanya Punyeto(Masturbation)
- Epuka matumizi ya Pombe
- Epuka Uvutaji wa Sigara
- Punguza Uzito kama una tatizo la Uzito Mkubwa
- Pia dhibiti magonjwa kama presha,Kisukari,magonjwa ya Moyo n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!