Chembechembe nyekundu za damu,Seli nyekundu
Fahamu kuhusu chembe chembe nyekundu za damu au Seli nyekundu za damu yaani Red blood cells(RBCs) Pamoja na Protein maarufu kama Hemoglobin,
Hesabu za kawaida za seli nyekundu za damu hutofautiana kulingana na mtu binafsi: Mfano:
• Wanaume: seli nyekundu za damu huweza kuwa kati ya milioni 4.7 hadi 6.1 kwa kila microlita moja ya damu.
• Wanawake: seli nyekundu za damu milioni 4.2 hadi 5.4 kwa kila mikrolita moja ya damu.
• Na Watoto: seli nyekundu za damu milioni 4.0 hadi 5.5 kwa kila microlita moja ya damu.
[sc_fs_faq html="true" headline="h3" img="" question="Je Hemoglobini ni nini?" img_alt="" css_class=""]Hemoglobini ni protini ambayo hubeba oksijeni na iko ndani ya kila seli nyekundu ya damu,kazi yake kubwa ni kuchukua oksijeni kwenye mapafu na kuipeleka kwenda kwenye tishu katika mwili wako wote. [/sc_fs_faq]
SELI NYEKUNDU ZA DAMU ZINAFANYA KAZI GANI?
Moja ya kazi kubwa inayofanywa na Seli nyekundu za damu(Red blood cells) ni kusafirisha Oxygen kutoka kwenye Mapafu kwenda kwenye tisu mbali mbali za mwili wako,
Hapo ndipo Tisu zako hufanya mchakato na kuzalisha energy kwa Kutumia hyo oxygen, Kisha kutoa Carbiondioxide kama uchafu au taka mwili,
Seli hizi nyekundu za damu huipeleka hii carbiondioxide kutoka kwenye tisu mbali mbali za mwili kwenda kwenye Mapafu kwa ajili ya kutolewa nje kama taka mwili(wastes).
SELI NYEKUNDU ZA DAMU HUTENGENEZWA WAPI?
Seli nyekundu za damu hukua katika tishu laini za mfupa wa mwili wako maarufu kama Uboho(bone marrow)na kutolewa kwenye mfumo wako wa damu baada ya kukomaa kabisa, ambayo huchukua takribani muda wa siku saba.
JE, SELI NYEKUNDU ZA DAMU ZINAONEKANAJE?
Seli nyekundu za damu hupata rangi nyekundu kutoka kwa protini inayojulikana kama hemoglobin, inayoziruhusu kubeba oksijeni kutoka kwa mapafu yako na kuipeleka kwa tishu zingine za mwili wako (hemoglobin).
Seli nyekundu za damu hazionekani sana na zina umbo la diski bapa au donati, ambayo ni ya mviringo yenye ujongezaji katikati, lakini haina mashimo. Seli nyekundu za damu hazina kiini kama chembe nyeupe za damu, na kuziruhusu kubadilisha umbo na kusonga kwa urahisi katika mwili wako.
SELI NYEKUNDU ZA DAMU ZIMEUNDWA NA NINI?
Seli nyekundu za damu hukua kwenye uboho wako. Uboho huunda karibu seli zote za mwili wako. Seli nyekundu za damu zina protini inayoitwa hemoglobin, ambayo inawajibika kwa kubeba oksijeni.
NI HALI GANI ZA KAWAIDA ZINAZOATHIRI SELI NYEKUNDU ZA DAMU?
Baadhi ya Sababu huweza kusababisha Seli nyekundu za damu kuwa nyingi au kidogo mwilini,
Na Sababu hizo ni pamoja na:
1. Tatizo la damu kupungua Mwilini- Anemia
2. Kupoteza damu mwilini kwa Sababu mbali mbali kama vile Ajali,Kuumia n.k,
Kitu chochote kinachopelekea Damu kuvuja mwilini basi huweza kusababisha Upungufu wa Seli nyekundu za Damu
3. Ugonjwa wa uboho: Unapopata uharibifu kwenye uboho wako, ambapo ndipo chembe chembe nyekundu za damu huundwa basi huweza kuathiri kiwango cha Seli hizi na kusababisha Upungufu wake,
Matatizo kama vile Leukemia pamoja na lymphoma, huweza kusababisha shida hii.
4. Kuwa na tatizo la Saratani, Saratani mbali mbali kama vile saratani ya Damu n.k pamoja na matibabu ya chemotherapy kwa saratani yanaweza kuathiri idadi ya seli nyekundu za damu ambazo mwili wako hutoa.
5. Ugonjwa wa moyo ambao umezaliwa Nao(Congenital heart diseases)
6. Ugonjwa wa mapafu: Tatizo la Tishu kwenye mapafu yako kuwa na makovu kutokana na shida kama vile emphysema, COPD au pulmonary fibrosis.
7. Tatizo la Hypoxia: ambapo Kiwango cha oksijeni katika damu yako kinakuwa cha chini zaidi.
8. Kuwa na tatizo la Upungufu wa vitamini kama vile Vitamin B9 na B12
9. Kuwa na tatizo la Upungufu wa Madini chuma(Iron) n.k
NI DALILI ZIPI HUWEZA KUJITOKEZA ENDAPO KUNA SHIDA KWENYE HALI YA SELI NYEKUNDU ZA DAMU?
- Mtu kupata Uchovu sana
- Kupata Udhaifu wa misuli.
- Ukosefu wa Nguvu mwilini.
- Maumivu ya kichwa au kizunguzungu.
- Macho kuona Marue rue (blurry vission)
- Mikono na miguu kuwa yabaridi n.k
NI MATIBABU GANI KWA MTU MWENYE SHIDA YA KUPUNGUA SELI NYEKUNDU ZA DAMU?
Zingatia mambo haya,yatakusaidia sana kupambana na tatizo hili;
✓ Kula chakula chenye uwiano mzuri wa virutubisho,
ili Kupata Virutubisho vya Kutosha kama vile vitamini mfano; Vitamin B9 na B12 au kupata Madini chuma(Iron) n.k
Kula vitu kama vile;
- Nyama ya ng'ombe,
- Samaki,
- Mboga za majani, kama vile kale,Tembele na mchicha
- Dengu, maharagwe na mbaazi.
- Karanga na matunda
✓ Hakikisha unapata matibabu kutokana na chanzo cha tatizo lako, kama nilivyokwisha kueleza baadhi ya Vyanzo
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!