Uzazi&Ujauzito
Dalili za hatari kwa mama mjamzito
Dalili za hatari kwa mama mjamzito ni zipi
Moja ya Vitu ambavyo Wakina mama Wajawazito hupewa ELIMU wanapohudhuria kliniki kuanzia Siku ya Kwanza ni Pamoja na kufundishwa Kuhusu Dalili za hatari wakati wa Ujauzito(Danger Signs),
Ukiwa unafahamu Dalili za hatari wakati wa Ujauzito itasaidia sana Kuchukua hatua Mapema Pale unapoona Viashiria vya hatari kwenye Ujauzito wako.
Kwa hali ya Kawaida,Asilimia kubwa ya Mahudhurio ya Kliniki huwa Manne,lakini mabadiliko hutokea kulingana na hali ya Ujauzito wako,
Hivo basi,Mahudhurio ya kliniki huweza kuzidi MANNE(4) kulingana na Hali ya Ujauzito wako
MAHUDHURIO MANNE YA KLINIKI
- Hudhurio la Kwanza:Ujauzito ukiwa na umri wa kabla ya wiki 16, Lakini kila hospital huweza kuweka utaratibu wao wa Muda wa kuanza Hudhurio la kwanza la kliniki, Ila Protocol,Baada tu ya kuwa Mjamzito unatakiwa kuanza kliniki
- Hudhurio la Pili: Ujauzito ukiwa na wiki 20 mpaka 24
- Hudhurio la Tatu: Ujauzito ukiwa na wiki 28 mpaka 32
- Hudhurio la Nne: Ujauzito ukiwa na wiki 36 Mpaka 40
Ziko dalili nyingi ambazo zinaweza kumpata mama mjamzito na iwapo utaona dalili hizi ni vyema ukafika katika kituo cha kutolea huduma mapema iwezekanavyo.
Ziko jamii za watu ambazo zimekuwa zikichukulia dalili hizi kama hali ya kawaida na wengine wamekuwa wakijitibia nyumbani pasipo kujua madhara yanayoweza kutokea iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa.
Chat Nasi Whatsapp
"Ungana na Wasomaji zaidi ya 12,000 wanaopata huduma ndani ya afyaclass, Kama unachangamoto yoyote ya kiafya; Kwa Ushauri&Tiba tuwasiliane hapa kupitia WhatsApp, Kama huna Whatsapp tuma SMS au Piga +255758286584."
Chat WhatSapp HapaDalili za hatari kwa mama mjamzito
Je Dalili za Hatari ni Zipi?
HIZI HAPA NI BAADHI YA DALILI ZA HATARI WAKATI WA UJAUZITO
1. Mama mjamzito Kuishiwa nguvu au kushindwa/kukosa nguvu za kutoka kitandani
2. Changamoto ya upumuaji (kuhema haraka haraka au kukosa pumzi)
3. Dalili zote za Degedege,Mwili kutetemeka au kupata convulsions/fits
4. Dalili zote za kifafa cha mimba kama vile;
- mjamzito kuona marue rue
- mjamzito kuvimba sana miguu,mikono na uso
- mjamzito kuumwa sana na kichwa
- presha kuwa juu sana pamoja na uwepo wa protein kwenye mkojo n.k
5. Homa kali au joto la mwili kuwa juu sana
6. Maumivu makali ya tumbo
7. Kupungua kwa kucheza kwa mtoto tumboni kusiko kwa kawaida. Au mtoto kuacha kucheza kabisa.
8.Chupa ya uzazi kupasuka kabla ya wakati yaani premature rupture of membrane
8. Maumivu makali ya kichwa na nuru hafifu
9. Kutokwa na damu ukeni
10. Kuvimba sana miguu,uso Pamoja na mikono.
11. Kutapika sana na kukosa hamu ya kula N.K
Kila mama mjamzito pamoja na mwenza wake wana haki ya kupata elimu juu ya dalili hizi na iwapo wataziona basi ni vyema wakafika katika kituo cha afya ili kuokoa maisha ya mtoto tumboni pamoja na maisha ya mama mjamzito.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REFERENCES;
- World Health Organization (WHO). Danger Signs in Pregnancy – Counselling for Maternal and Newborn Health Care.
https://www.who.int/tools/your-life-your-health/life-phase/pregnancy–birth-and-after-childbirth/keeping-well-during-pregnancy-and-after-childbirth - Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Urgent Maternal Warning Signs.
https://www.cdc.gov/hearher/hcp/toolkit/warning-signs-educational-materials.html - Office on Women’s Health. Pregnancy Complications – Warning Signs During Pregnancy.
https://womenshealth.gov/pregnancy/youre-pregnant-now-what/pregnancy-complications - World Health Organization (WHO). Care for Mother’s Health at Home – Danger Signs During Pregnancy.
https://applications.emro.who.int/docs/9789292743468-eng.pdf - National Institutes of Health (NIH). Danger Signs in Pregnancy.
https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304178/ - Knowledge of Danger Signs During Pregnancy and Subsequent Healthcare Seeking Actions Among Women in Urban Tanzania.
https://pmc.ncbi.nlm.nih.gov/articles/PMC5751870/
Ushauri,Elimu,Tiba
Medical Consultation: Karibu afyaclass Kwa Ushauri na Tiba, Kama una Tatizo lolote la kiafya, tafadhali Wasiliana na Daktari moja kwa moja hapa || Call au Sms(+255758286584) au Whatsapp.
Je, unahitaji ushauri binafsi au matibabu ya tatizo lolote?
💬 Wasiliana na Daktari Hapa(Whatsapp)

