Ticker

6/recent/ticker-posts

Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito



Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito

Labor ni nini?

Kabla ya kufahamu kuhusu Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito,ni muhumu kufahamu maana ya labor kitaalam,

Labor Ni mchakato ambapo mtoto(fetus) aliyetumboni,kondo la nyuma(Placenta) pamoja na membranes hutolewa nje kupitia njia ya Uzazi yaani birth canal.

Hii ni kwa Mujibu wa Maelezo kutoka kwenye kitabu cha "Myle's textbook for midwives"

Huu ni mchakato asilia ambao mwili wako huupitia wakati mtoto anazaliwa,

Mchakato huu huanza toka unaanza kupata contractions za kwanza mpaka mtoto anapozaliwa pamoja na Kondo la Nyuma yaani placenta linapotoka.

Katika makala hii tutajadili kwa kina kuhusu Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito;

 HATUA ZAKE NI ZIPI?(STAGES OF NORMAL LABOUR)

Baada ya Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito kujitokeza, mwili wake hupitia mchakato maalum wa Labor,

Mchakato huu una Hatua kuu NNE(4) FOUR STAGES ambazo ni;

  • The first stage of labour
  • The Second stage of labour
  • The third stage of labour
  • The fourth stage of labour

1. Hatua ya kwanza(The first stage of labour) :

Ambapo huanza toka mama Mjamzito anaanza kupata painful regular rhythmic contraction mpaka mlango wa kizazi yaani Cervix unapofunguka vizuri yaani fully dilated Cervix,ambapo kwa kitaalam tunafamu inatakiwa kuwa Cm 10.

2. Hatua ya pili(The second stage of labour):

Inaanza toka mlango wa kizazi unapofunguka vizuri(Fully dilated) mpaka mtoto anapozaliwa kabsa-completely baby born

3. Hatua ya Tatu(The third stage of labour):

Inaanza toka mtoto anapozaliwa na kukamilika pale ambapo kondo la nyuma(placenta) pamoja na membranes zinapotoka au kutolewa nje.

4. Hatua ya nne(4TH Stage of labour):

Inaanza toka kondo la nyuma(placenta) pamoja na membrane kutolewa nje mpaka Saa Moja baada ya Kujifungua.

Maelezo kwa Kina kuhusu Hatua za Kujifungua,utayapata kwenye Category ya Midwifery Course Maalum kabsa kwa ajili ya Ukunga(Midwives)

Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito

Imekuwa ngumu kidogo kujua dalili za kujifungua za kweli kwa mama mjamzito,hali ambayo imepelekea baadhi ya wakina mama wajawazito kutokujua muda wa kupata uchungu na kujifungua(True labour), hasa kwa wakina mama wajawazito ambao ndyo mimba zao za kwanza.

Je dalili za mwanzo za kujifungua au dalili za uchungu kwa mama mjamzito ni zipi? soma hapa kujua baadhi ya Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito;

1. Kuongezeka sana kwa hisia za kukojoa mara kwa mara( increased urge to urinate),

Hali hii ya mama mjamzito kutaka kukojoa kila mara huongezeka sana akikaribia kujifungua kutokana na pressure au mgandamizo unaotokea kwenye kibofu cha mkojo wakati kichwa cha mtoto kikiingia kwenye Pelvis,

Hivo hii ni mojawapo ya Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito.

2. Mama mjamzito kuanza kutoa mlenda mlenda ukeni yaani(mucus plug), hii ni dalili kwamba labor ipo karibu sana.

Thick Mucus hii hutoka kwenye tezi za mlango wa kizazi yaani cervical glands ili kusaidia mlango wa kizazi au Cervix kuendelea kufunguka,

Mgandamizo au Pressure kubwa inayotokana na kichwa cha mtoto wakati kinashuka husababisha hii mucus plug kutolewa nje ya Uke na wakati mwingine huwa na mchanganyiko wa damu yaani kwa kitaalam “bloody show”.

3. Kichwa cha mtoto kushuka zaidi kuingia kwenye Pelvis, Hiki ni kiashiria kingine kwamba mtoto yupo karibu kuzaliwa.

4. Kufunguka kwa mlango wa kizazi yaani kwa kitaalam hujulikana kama Cervix dilation. Ili mtoto apite lazima mlango wa kizazi uanze kufunguka hapa ndyo utaanza kusikia maneno kama vile “njia yake imefunguka ni cm 2,4,5,6,8, au ipo full dilated yaani 10 cm”.

5. Kuanza kupata Contractions ambapo huhusisha tumbo kuvuta au kukaza sana(tightenings) mara kwa mara na kuachia.

Wakati mwingine tumbo hili huvuta kama lile la hedhi yaani Menstrual cramps na kadri contractions zinavyotokea karibu karibu ndivo na kujifungua hukaribia sana,

Hivo basi,hizi pia ni baadhi ya Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito.

6. Kupata maumivu makali ambayo huanzia mgongoni kwa mama mjamzito(backache),

Maumivu haya huweza kuanzia mgongoni kushuka chini ya kiuno na kwenda moja kwa moja tumboni.

7. Kujisikia kujisaidia haja kubwa na hata wengine kuharisha kabsa.

Kutokana na maumivu kwenye pelvic pamoja na pressure kubwa au mgandamizo mkubwa,Mama mjamzito huweza kujisikia kujisaidia haja kubwa.

8. Chupa ya Uzazi kupasuka ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Rupture of the amniotic membranes,

Chupa ya uzazi kupasuka ni Ishara kwamba Mtoto anataka kutoka sasa, Unashauriwa chupa yako ya uzazi ikipasuka usikae kimya na hata kama upo nyumbani haraka wahi hospitalini.

FAQs

Je, labor ni nini?

Labor Ni mchakato ambapo mtoto(fetus) aliyetumboni,kondo la nyuma(Placenta) pamoja na membranes hutolewa nje kupitia njia ya Uzazi yaani birth canal.

Zipi ni Dalili za kweli za kujifungua kwa mama mjamzito?

Dalili za kweli za kujifungua kwa mama mjamzito ni pamoja na; Kufunguka kwa mlango wa kizazi yaani kwa kitaalam hujulikana kama Cervix dilation. n.k

CONCLUSION(HITIMISHO)

Ni muhimu sana kwa mama mjamzito kufahamu Dalili za kujifungua kwa mama mjamzito ambazo ni za kweli(True labour), kwani hii itamsaidia kuwa makini zaidi na kupata msaada wa haraka pale anapohitaji kujifungua,

Ukiona dalili kama hizi;chupa ya Uzazi kupasuka,maumivu makali ambayo huanzia chini mgongoni kwenda tumboni ambayo hayaishi hata baada ya kutembea tembea n.k

hata kama Upo Nyumbani wahi Mapema Hospitalini ili kupata Msaada wa haraka zaidi, na kuhakikisha Unajifungua Salama.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments