Ukweli ni kwamba watu wengi hawanywi maji ya kutosha kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya, mbali na kuelimishwa kuhusu madhara mbali mbali ya kutokunywa maji ya kutosha,
Unashauriwa kunywa maji angalau wastani wa Lita 2.5 mpaka 3 kwa siku, Ingawa kiwango hiki hutegemea pia umri,uzito,aina ya kazi unayofanya,hali ya hewa n.k
Swali; je zipi ni dalili za mtu ambaye hanywi maji ya kutosha?
DALILI ZA KUTOKUNYWA MAJI YA KUTOSHA
Zipo dalili ambapo huonekana ndani ya muda mfupi sana kwa mtu ambaye hanywi maji ya kutosha na zipo dalili ambazo huchukua muda kidgo kuanza kujionyesha, Kwa ujumla wake hizi hapa chini ni baadhi ya dalili ambazo huweza kutokea au kujionyesha kwa mtu ambaye hanywi maji ya kutosha;
1. Ngozi ya mwili kukauka kupita kiasi hata kama unapaka mafuta, baadhi ya watu ngozi hukauka na wengine hufikia hatua ya ngozi kuanza kutengeneza cracks au kupasuka
2. Mdomo kukauka sana hasa kwenye lips za mdomo, hadi kufikia hatua ya lips za mdomo kupauka au kupasuka
3. Kupatwa na kiu ya maji kupita kiasi kila mara
4. Kupatwa na maumivu makali ya kichwa cha mara kwa mara
5. Mwili kuchoka kupita kawaida au kupata uchovu usio wa kawaida hata kama hukufanya kazi yoyote ngumu
6. Kupatwa na tatizo la kujisaidia choo kigumu sana mara kwa mara yaani Constipation
7. Kupata shida sana ya kukojoa,kutoa mkojo mdogo sana,kutoa mkojo wenye rangi iliyokolea sana,nyeusi n.k
8. Kupatwa na maambukizi ya UTI za mara kwa mara
9. Kupatwa na tatizo la kukakamaa kwa misuli ya mwili yaani muscle cramps
10. Kupatwa na tatizo la kizunguzungu mara kwa mara
11. Mwili kutokutoa jasho kabsa hata kama hali ni ya joto sana
12. Kuanza kupatwa na matatizo ya moyo,matatizo ya presha au shinikizo la damu n.k
13. Kuanza kusumbuliwa na matatizo ya figo,maumivu ya kiuno,mgongo,nyonga,magoti,miguu yote n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!