Dalili za mtoto kulawitiwa,ukatili wa kijinsia kwa watoto
Fahamu kuhusu Dalili za mtoto kulawitiwa kupitia makala hii,ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Ukatili wa kijinsia kwa watoto ikiwemo Mtoto kulawitiwa ni moja ya swala kubwa kwenye Jamii kwa hivi sasa, Na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha tunakomesha kabsa vitendo hivi kwa watoto wetu.
Dalili za mtoto kulawitiwa
Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za mtoto kulawitiwa, kwa msaada wa Shirika la Sema Tanzania,
Dalili za mtoto kulawitiwa huweza kutofautiana kulingana na umri na tabia za mtoto,
Mtoto aliyefanyiwa ukatili wa kingono anaweza kuwa na dalili kama hizi;
- kujitenga na wenzake,
- kuwa mpweke,
- na ghafla hubadilika kuwa muoga sana isivyo kawaida yake.
- Baadhi ya watoto waliofanyiwa ukatili wa kingono hujaribu kadiri ya uwezo wao kuzuia watu kuona sehemu zao za siri, kama bado wanaogeshwa. Yaani mtoto atakataa usimnawishe/kumgusa sehemu za siri,
- au ataonekana kuumia pale unapojaribu kumnawisha na huenda akakataa kuogeshwa kabisa.
- Mara nyingi, mtoto aliyefanyiwa ukatili hushtuka ama kufedheheka kila akimuona mtu aliyemfanyia ukatili hata kama alikua amemzoea sana.
- Dalili nyingine ni kuogopa giza,
- kushtuka usingizini,
- mara nyingine anakuwa na jina jipya la sehemu za siri.
- Pia kukojoa kitandani kama alikuwa hakojoi na wengine hunyonya kidole.
- Kwa watoto wakubwa zaidi, huweza kujaribu kujinyonga,
- kukimbia nyumbani,
- kupata msongo wa mawazo na mengine mengi.
Silaha kubwa dhidi ya ukatili kwa mtoto ni ukaribu na mzazi/mlezi. Kama anaweza kuongea, zungumza nae; mdadisi kwa maswali ili kujua kama ametendewa chochote bila wewe kujua.
Mtoto akiwa huru/karibu na wewe atakueleza kila kitu kinachomtatiza kwa kuwa wewe ni zaidi ya mzazi na ni rafiki yake,
Fahamu kuwa watu wanaowakatili watoto ni wajanja sana na wanajua kuwa wanachokifanya sio sahihi na hivyo huwatishia watoto kuwa wakisema watawaua au kuwadhuru wapendwa wao,
Wengine pia huwafanya watoto wajisikie kuwa wao ndio wamefanya kosa.
Soma zaidi hapa kuhusu Dalili za mtoto kulawitiwa
Hizi ndio dalili 10 za mwanzo ambazo mtoto anayenyanyaswa kingono huwa anazionesha mara nyingi.
1. Mtoto anapata shida wakati wa kukaa au kutembea. (Dalili hizi ni kuanzia watoto wa miaka Miwili hadi 10)
2. Mtoto anaogopa kupita kiasi baadhi ya watu, mahali au vitu. (Hii ni kuanzia mwaka mmoja hadi mitano)
3. Mtoto anapenda kujishika sehemu za siri mara kwa mara na hali hii humtokea hadi usiku akiwa amelala.
4. Mtoto anakaa chooni muda mrefu au kuhitaji kujisaidia mara kwa mara. (Hii huwatokea watoto wenye umri kuanzia mwaka 1-5)
5. Usiku anapatwa na marue marue au anaweweseka usiku. (miaka 1-5)
6. Mtoto anakataa/kusumbua kula na muda mwingine kutapika bila ugonjwa. (Miaka 0-5)
7. Mtoto analia sana. (Miaka 0-3 )
8. Mtoto anaona aibu na kujitenga. (umri wote 0-17)
9. Mtoto anashindwa kuzuia haja kubwa. (Umri kati ya miaka 4-7)
10. Mtoto anakuwa mkimya isivyo kawaida (Umri wa balehe).
11. Dalili zingine ni kama vile;
- Mtoto kushuka kielimu gafla. (Miaka 6-17)
- Mtoto kuwa na kiburi, maamuzi ya kukinzana na maagizo. (Umri wa balehe)
- Mimba (Miaka 11-17)
- Majaribio ya kujiua. (Miaka 8- 17)
- mtoto kukimbia nyumbani mara kwa mara (Miaka 8-17)
- Mtoto kukataa kushiriki shughuli za nyumbani, za shule, za kiroho. (7-17) n.k
Credits: Sema Tanzania&Bongo5
Hitimisho
Ni muhimu sana kufahamu kuhusu Dalili za mtoto kulawitiwa, Kisha kujenga tabia ya kuwachunguza watoto mara kwa mara, ili ukiona dalili zozote za mtoto kulawitiwa au kufanyiwa vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia uchukue hatua mapema.
Ukatili wa kijinsia kwa watoto ikiwemo Mtoto kulawitiwa ni moja ya swala kubwa kwenye Jamii kwa hivi sasa, Na ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha tunakomesha kabsa vitendo hivi kwa watoto wetu.
Silaha kubwa dhidi ya ukatili kwa mtoto ikiwemo mtoto kulawitiwa ni ukaribu na mzazi/mlezi. Kama anaweza kuongea, zungumza nae; mdadisi kwa maswali ili kujua kama ametendewa chochote bila wewe kujua.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!