Ticker

6/recent/ticker-posts

Dalili za Saratani ya Matiti kwa Wanawake na Wanaume



Dalili za Saratani ya Matiti kwa Wanawake na Wanaume

SARATANI NI NINI?

Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au ulizidi kiwango,Kwahyo basi, Saratani ya matiti ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la titi au matiti.

DALILI ZA SARATANI ZA MATITI

(1) Dalili ya awali inayoweza kutambulisha saratani ya matiti ni kuwepo kwa uvimbe kwenye titi ambao huwa na hali tofauti na sehemu nyingine za titi.

Hata hivyo, si kila uvimbe kwenye titi unaashiria uwepo wa saratani ya matiti. Uvimbe huu huwa mgumu, unaochezacheza kwenye titi, ambapo wakati mwingine unaweza kuwa na maumivu makali au kusiwe na maumivu yeyote.

Uvimbe huu huwepo zaidi ya mzunguko mmoja wa hedhi kwa wale ambao hawajaacha kupata hedhi.

Dalili nyingine ni pamoja na

(2) Kuwepo kwa uvimbe kwenye sehemu za kwapa

(3) Sehemu ya titi kuingia ndani inayoashiria uvimbe usioonekana au usioweza kuhisiwa

(4) Mabadiliko kwenye chuchu, kama vile chuchu kuzama ndani au kuwa na nundu ndogo ndogo, chuchu kuwasha, kuhisi kama kuchoma, kidonda kwenye chuchu au chuchu kuwa na kovu ambalo huashiria saratani ya sehemu hiyo

(5) Kubadilika kwa umbo la titi, ngozi ya titi kuwa kama ganda la chungwa (peu de orange), ngozi kuwa na rangi nyekundu, na kuongezeka kwa joto kwenye titi. Dalili hizi huashiria kusambaa kwa saratani mwilini.

(6) Dalili nyingine ni chuchu kutoa maji yasiyo ya kawaida ambayo hayana rangi. Aidha wakati mwingine, chuchu hutokwa damu au majimaji yenye rangi nyingine tofauti.

MAMBO YANAYOONGEZA HATARI YA KUPATA SARATANI YA MATITI

(1) Jinsi ya kike,wapo kwenye hatari zaidi

(2) Kuanza hedhi katika umri mdogo.

(3) Kukoma siku katika umri mkubwa

(4) Kutozaa kabisa.

(5) Kutonyonyesha kabisa au kunyonyesha kwa muda mfupi.

(6) Utumiaji mafuta mengi katika chakula.

(7) Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.

(8) Unene kupita kiasi

(9) Uvutaji sigara.

(10) Utumiaji wa pombe kupita kiasi.

(11) Historia ya saratani ya matiti katika familia.

JINSI YAKUJILINDA NA SARATANI YA MATITI

Kujichunguza mwenyewe mara kwa mara kwa mara.

Uchunguzi wa kitabibu wa matiti kila mwaka.

Uchunguzi wa matiti kwa njia ya mashine ya mionzi (mara moja kwa mwaka kwa wenye miaka zaidi ya 40).

Wanawake wote wenye umri kuanzia miaka 21 wajichunguze matiti yao siku ya 5-7 baada ya kumaliza hedhi mbele ya kioo

Madhara ya saratani ya Matiti

- Titi kuoza na kukatwa kabsa

- Titi kuuma sana na kutoa damu au usaha kila wakati

- Mwanamke kupoteza maisha pia

- Kushindwa kabsa kunyonyesha kama mama ananyonyesha

Kumbuka

Kutokana na tafiti nyingi zilizofanywa,Hizi hapa ni kansa mbili zinazoongoza kuwatesa wanawake

SARATANI YA MATITI KWA WANAUME,CHANZO,DALILI NA TIBA

Asilimia kubwa ya watu hawajui kwamba kuna saratani au kansa ya ziwa kwa wanaume,wengi wao wanajua kwamba kuna kansa/saratani ya matiti kwa wanawake tu.

Ila ukweli ni kwamba,hata wanaume huweza kupatwa na aina hii ya saratani japo namba yao sio kubwa kama wanawake.

CHANZO CHA SARATANI YA MATITI KWA WANAUME

- Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo hujulikana kama chanzo cha Kansa hii japo kuna baadhi ya vitu ambavyo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata aina hii ya saratani kama vile;

✓ Umri kuwa mkubwa

✓ Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huhusisha kuongeza vichocheo vya mwilini kwa muda mrefu

✓ Kuwa na historia ya tatizo hili katika famili yenu

✓ Mwanaume kufanyiwa upasuaji wa korodani

✓ Unene kupita kiasi

N.K

Pia kuna utafiti ambao umefanywa "according to new research funded by the charity Breast Cancer Now and published in Breast Cancer Research"

Utafiti huu unasema kwamba " Wanaume ambao hawana uwezo wa kuzalisha yaani Infertile men wapo kwenye hatari mara mbili ya kupata kansa hii ya matiti kuliko wale ambao hawana matatizo yoyote ya uzazi(fertility issues)"

DALILI ZA SARATANI YA MATITI KWA WANAUME NI PAMOJA NA;

- Mwanaume kupata maumivu makali kwenye ziwa

- Mwanaume kuanza kutoa usaha au damu kwenye ziwa

- Ziwa moja kuanza kuwa kubwa kuliko lingine

- Sehemu ya ziwa kubadilika rangi na kuwa nyekundu sana

- N.K

MATIBABU YA SARATANI YA MATITI KWA WANAUME

-Mojawapo ya matibabu ya kansa hii ni pamoja na mgonjwa kufanyiwa upasuaji, huduma ya Chemotherapy, dawa za vichocheo mwilini, huduma ya mionzi(Radiation therapy) N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments