Dalili za Uchungu kwa Mama Mjamzito Anayetaka kujifungua

 Dalili za Uchungu kwa Mama Mjamzito Anayetaka kujifungua

DALILI ZA MWANZO ZA KUJIFUNGUA(dalili za uchungu kwa mama mjamzito ni zipi)

Imekuwa ngumu kujua dalili za kweli kwa mama mjamzito kupata uchungu na kujifungua(True labour), hasa kwa wakina mama wajawazito ambao ndyo mimba zao za kwanza.

Je dalili za mwanzo za kujifungua au dalili za uchungu kwa mama mjamzito ni zipi? soma hapa kujua baadhi ya dalili za kujifungua...!!!

1. Kuongezeka sana kwa hisia za kukojoa mara kwa mara( increased urge to urinate),

Hali hii ya mama mjamzito kutaka kukojoa kila mara huongezeka sana akikaribia kujifungua kutokana na pressure au mgandamizo unaotokea kwenye kibofu cha mkojo wakati kichwa cha mtoto kikiingia kwenye Pelvis.

2. Mama mjamzito kuanza kutoa mlenda mlenda ukeni yaani(mucus plug), hii ni dalili kwamba labor ipo karibu sana.

Thick Mucus hii hutoka kwenye tezi za mlango wa kizazi yaani cervical glands ili kusaidia mlango wa kizazi au Cervix kuendelea kufunguka,

Mgandamizo au Pressure kubwa inayotokana na kichwa cha mtoto wakati kinashuka husababisha hii mucus plug kutolewa nje ya Uke na wakati mwingine huwa na mchanganyiko wa damu yaani kwa kitaalam "bloody show".

3. Kichwa cha mtoto kushuka zaidi kuingia kwenye Pelvis, Hiki ni kiashiria kingine kwamba mtoto yupo karibu kuzaliwa.

4. Kufunguka kwa mlango wa kizazi yaani kwa kitaalam hujulikana kama Cervix dilation. Ili mtoto apite lazima mlango wa kizazi uanze kufunguka hapa ndyo utaanza kusikia maneno kama vile "njia yake imefunguka ni cm 2,4,5,6,8, au ipo full dilated yaani 10 cm".

5. Kuanza kupata Contractions ambapo huhusisha tumbo kuvuta au kukaza sana(tightenings) mara kwa mara na kuachia.

Wakati mwingine tumbo hili huvuta kama lile la hedhi yaani Menstrual cramps na kadri contractions zinavyotokea karibu karibu ndivo na kujifungua hukaribia sana.

6. Kupata maumivu makali ambayo huanzia mgongoni kwa mama mjamzito(backache),

Maumivu haya huweza kuanzia mgongoni kushuka chini ya kiuno na kwenda moja kwa moja tumboni.

7. Kujisikia kujisaidia haja kubwa na hata wengine kuharisha kabsa.

Kutokana na maumivu kwenye pelvic pamoja na pressure kubwa au mgandamizo mkubwa,Mama mjamzito huweza kujisikia kujisaidia haja kubwa.

8. Chupa ya Uzazi kupasuka ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Rupture of the amniotic membranes,

Chupa ya uzazi kupasuka ni Ishara kwamba Mtoto anataka kutoka sasa, Unashauriwa chupa yako ya uzazi ikipasuka usikae kimya na hata kama upo nyumbani haraka wahi hospitalini.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!