Ticker

6/recent/ticker-posts

Dalili za Ugonjwa wa Kaswende,chanzo chake(Syphilis)



Dalili za Ugonjwa wa Kaswende,chanzo chake(Syphilis)

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa ambao hutokana na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kwa jina la Treponema pallidum,

Unaweza kupata ugonjwa wa Kaswende kupitia mgusano(direct contact) kwenye michubuko au vidonda ambavyo tayari vimeathiriwa na bacteria hawa, michubuko au vidonda hivi huweza kuwepo maeneo kama vile;

- Mdomoni

- Kwenye Uume

- Kwenye Uke

- Sehemu ya haja kubwa n.k

Asilimia 99% ya maambukizi haya ya kaswende,watu huyapata wakati wakifanya mapenzi au tendo la ndoa.

KUMBUKA; Watoto wanaweza kupata ugonjwa wa kaswende kama mama zao wenye ugonjwa huu hawakutibiwa,hii hujulikana kama congenital syphilis.

HUWEZI KUPATA KASWENDE KWA;

- Kushare vyoo

- Kushare vijiko au vyombo vya kula

- Kuvaa nguo za mtu mwingine n.k

Na hii ni kwa sababu bacteria wanaosababisha ugonjwa wa kaswende hawawezi kuishi kwa Muda mrefu nje ya mwili wako.

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA UGONJWA HUU WA KASWENDE

• Wanaofanya mapenzi bila kinga/Condom(Ngono zembe)

• Wenye wapenzi wengi(multiple sexual partners)

• Wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao

•Wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile

• Wenye maambukizi ya UKIMWI

• Wenye wapenzi ambao tayari wana ugonjwa huu wa kaswende

DALILI ZA UGONJWA WA KASWENDE NI ZIPI?

Ugonjwa huu wa kaswende umegawanyika kwenye hatua Nne yaani;

- primary,secondary,latent na tertiary,

Kwenye hatua mbili za mwanzo(primary na secondary) kaswende huambukiza zaidi, kwenye hidden au latent stage kaswende hubaki kuwa active lakini mgonjwa anaweza asionyeshe dalili zozote, na kwenye Tertiary Stage hapa ugonjwa huleta madhara zaidi kwenye afya.

(1).Primary syphilis

Hapa huhusisha wiki 3 mpaka 4 toka Mgonjwa kuambukizwa bacteria wanaosababisha Kaswende,

Hapa dalili zinaanza kuonekana kama kidonda kidogo sana ambacho hata hakina maumivu yoyote kwa kitaalam huitwa chancre,

Kidonda hiki kidogo hakina maumivu yoyote ila kinakuwa na uwezo mkubwa sana wa kuambukiza, Mtu anaweza hata asijue kwamba ana kijidonda hiki(chancre),

Na kinatokea sehemu ambapo bacteria wemeingilia Mwilini kama vile Mdomoni,Sehemu za Siri au kwenye njia ya haja kubwa.

Wastani kidonda huweza kuonekana wiki 3 baada ya kuambukizwa, lakini huweza kuchukua siku 10 mpaka 90 kuonekana, na Wakati mwingine Mtu huweza kuwa na dalili Moja tu ya Kuvimba kwa tezi la Lymph(Swollen lymph nodes).

Na mtu mwingine huweza kuambukizwa kwa kugusana na kijidonda hicho(Direct contact) hasa wakati wa kufanya mapenzi.

(2).Secondary syphilis

Katika hatua hii Ngozi inaweza kuwa na Rashes,maumivu ya koo au mtu kuwa na sore throat,

Rashes hizi kwenye ngozi haziwashi na mara nyingi huonekana kwenye viganja vya mikono pamoja na kwenye miguu kwa chini(sole), japo pia zinaweza kuonekana maeneo mengine.

Na watu wengine wanaweza wasijue mpaka zinaisha zenyewe.

Dalili zingine kwenye secondary syphilis ni pamoja na;

- Kupata maumivu ya kichwa

- Kuvimba kwa lymph nodes

- Mwili kuchoka sana kuliko kawaida

- Kupata Homa

- Uzito wa mwili kushuka au kupungua

- Nywele kunyonyoka(hair loss)

- Maumivu kwenye joints n.k

KUMBUKA;Kuna umuhimu mkubwa wa kuwa makini kwa Mgonjwa mwenye shida hii,maana tafiti nyingi zinaonyesha ugonjwa wa kaswende unaweza kuwa na dalili ambazo hufanana kabsa na magonjwa mengine au Nonspecific symptoms, hali ambayo inaweza kuwa ngumu hata mtu kujua kama ana tatizo hili.

(3).Latent syphilis

Hatua ya tatu ya ugonjwa wa kaswende inajulikana kama latent au hidden, stage.

Dalili zote zilizoonekana kwenye hatua ya kwanza na ya pili zinapotea, hivo hakuna dalili yoyote inaonekana kwenye stage hii ndyo maana ya kupewa jina la hidden au latent stage.

Japokuwa dalili zimepotea ila Bacteria bado wapo mwilini na wakati mwingine huweza kuchukua muda kabla ya kwenda stage ya nne(tertiary stage of syphilis).

(4).Tertiary syphilis

Baadhi ya tafiti zinaonyesha ni asilimia 14% mpaka 40% ya watu wenye ugonjwa wa kaswende hufika stage hii,

Hatua hii ya ugonjwa wa kaswende inaweza kuchukua Muda mrefu sana(miaka) mpaka mtu kuingia kwenye stage hii toka siku ya kwanza ya maambukizi(initial infection).

Na madhara yake kwenye stage hii ni makubwa sana hata kuhatarisha maisha ya mgonjwa,

BAADHI YA MADHARA KWENYE HATUA HII YA UGONJWA WA KASWENDE NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kuwa kipofu au kutopoteza uwezo wa kuona(blindness)

- Mgonjwa kupoteza uwezo wa kusikia

- Kuathiriwa afya ya akili, kuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu n.k

- Kuharibiwa kwa soft tissue pamoja na mifupa

- Kupatwa na matatizo kwenye mfumo wa fahamu(neurosyphilis), ambapo bacteria wa kaswende hushambulia ubongo pamoja na uti wa mgongo.

- matatizo kama kiharusi(stroke), meningitis n.k

- Kupatwa na matatizo la Moyo n.k

KWA UPANDE WA MTOTO ALIYEZALIWA NA UGONJWA WA KASWENDE(congenital syphilis) ANAWEZA KUWA NA DALILI HIZI;

1. Kuchelewa hatua zake za ukuaji, kama kukaa,kusimama,kuongea n.k

2. Kuwa na dalili za kifafa au degedege

3. Kuwa na rashes kwenye ngozi

4. Kupandisha Homa

5. Ngozi na sehemu zingine kuwa na manjano(jaundice)

6. Kuwa na dalili za kuishiwa na damu(anemia)

7.Kuwa na vidonda ambazo vinaambukiza zaidi(infectious sores)n.k

MATIBABU YA UGONJWA WA KASWENDE

Moja ya tiba kubwa kwa ugonjwa wa kaswende kwa mama mjamzito na watu wengine ni pamoja na kupewa dawa ya Penicillin ambapo hutolewa kwa mfumo wa sindano(Penicillin Injection).

Lakini kwa mtu mwenye allergy na Penicillin huweza kupewa antibiotics zingine ikiwemo;doxycycline,ceftriaxone n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Post a Comment

0 Comments