Dalili za Ugonjwa wa malaria kwa mjamzito

Dalili za malaria kwa mjamzito(Dalili za ugonjwa wa Malaria Kwa Mama mjamzito)

Miongoni Mwa watu ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Ugonjwa wa Malaria ni pamoja na;

• Watoto wenye umri wa chini ya miaka 5

• Wajawazito

• Wazee

• Wageni wanaotoka maeneo ambayo hayana ugonjwa wa Malaria

• Watu wenye tatizo la upungufu wa Kinga Mwilini kama Wagonjwa wa UKIMWI n.k

FAHAMU: Wanawake wajawazito wapo kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa Malaria kwa Urahisi zaidi kutokana na kushuka kwa Kinga ya Mwili kipindi hiki cha Ujauzito.

Dalili za Mara kwa Mara za Malaria katika Ujauzito;

Hizi hapa ni dalili ambazo Mara nyingi hutokea kwa Mama Mjamzito mwenye Malaria,

- Kupata Homa

- Kuhisi Kichefuchefu pamoja na kutapika

- Kupata Maumivu ya kichwa

- Kupata Maumivu ya Viungo

- Kupungua kwa hamu ya kula n.k

Hivo ni vizuri zaidi Mama mjamzito kwenda hosptal kufanya vipimo baada ya kuona dalili kama hizi,

Epuka dhana ya kusema hii ni UTI,hivo unaanza dawa za UTI,fanya vipimo kwanza, wakati mwingine unaweza kuwa na ugonjwa wa Malaria.

Wakina mama wajawazito LAZIMA watafute matibabu kutoka katika kituo cha afya ndani ya kipindi cha chini ya saa 24 baada ya dalili za Malaria kuanza.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!