Dalili za Ugonjwa wa Surua,chanzo na Tiba yake

Dalili za Ugonjwa wa Surua,chanzo na Tiba yake

UGONJWA WA SURUA(MEASLES),CHANZO,DALILI NA MATIBABU YAKE

Ugonjwa huu huhusisha Mfumo wa hewa na husababishwa na virusi aina ya Paramyxovirus na pia uenezwaji wa virusi hawa ni kwa njia ya mtu kupumua, kupiga chafya, kukohoa au wakati mwingine mtu akiongea.

Licha ya chanjo ambazo watoto hupewa kliniki lakini bado Ugonjwa huu wa Surua huendelea kusababisha Vifo kwa watoto wengi wenye umri wa chini ya Miaka 5.

DALILI ZA UGONJWA WA SURUA NI PAMOJA NA;

- Kuwa na mapele katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo Usoni

- Mgojwa kupatwa na hali ya kukohoa

- Mgonjwa Kupatwa na mafua mepesi

- Joto la mwili la Mgonjwa kupanda

- Mgonjwa kubadilika rangi ya macho na kuwa mekundu

MADHARA YA UGONJWA WA SURUA NI PAMOJA NA;

  1. Mgonjwa kupatwa na tatizo la masikio
  2. Kuathiriwa utoaji wa sauti kwa Mgonjwa kwani ugonjwa huu huhusisha mfumo mzima wa hewa
  3. Athari katika ubongo wa binadamu
  4. Kuchangia tatizo la Pneumonia au Homa ya mapafu
  5. Kuchangia kuwepo kwa matatizo ya moyo
  6. Huathiri utengenezaji wa seli za Damu

MATIBABU YA UGONJWA WA SURUA

Hakuna tiba au dawa ya moja kwa moja mpaka sasa kwa ajili ya kutibu surua, Japo mgonjwa atashauriwa kupata mda wa kutosha kupumzika,kupata hewa ya kutosha na kunywa maji kwa kiasi kikubwa.

Hivo basi matibabu ya surua yataangalia sana dalili za Mgonjwa na singinevyo.

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!