Dalili za ukomo wa hedhi ni zipi
Asilimia Kubwa tunasema Mwanamke kafikia Ukomo wa Hedhi pale ambapo amekaa kwa kipindi cha zaidi ya Miezi 12 Pasipo kupata Period yake ya mwezi,
hapo tunazungumzia Mwanamke mwenye Miaka 40s, 50s na kuendelea, na pia hana tatizo lolote la kiafya ambalo huweza kuzuia hedhi yake .
CHANZO CHA UKOMO WA HEDHI,
kipindi cha Ukomo wa hedhi huja kutokana na matokeo ya Mabadiliko mbali mbali Mwilini,ikiwemo;
1. Mabadiliko ya vichocheo mwilini,
Hasa pale mwili wako(Ovaries) unapoanza Kupunguza Uzalishaji wa kichocheo cha estrogen pamoja na progesterone,
Hormones ambazo zinarekebisha mzunguko wako wa hedhi,
Katika miaka ya 40, hedhi yako inaweza kuanza kutokea kwa muda mrefu zaidi au kwa muda fupi, nzito au nyepesi, mara kwa mara au mara chache zaidi.
Kwa wastani, kufikia umri wa miaka 51 - ovari zako zitaacha kutoa mayai, na hapo utakuwa hupati hedhi tena.
2. Upasuaji wa kuondoa ovari (oophorectomy). Ovari zako huzalisha hormones,
Na hapa tunazungumzia hasa vichocheo vya estrojeni na progesterone, ambavyo hudhibiti mzunguko wa hedhi.
Upasuaji wa kuondoa ovari zako husababisha kukoma kwa hedhi mara moja.
3. Upasuaji wa Kuondoa Kizazi bila Kugusa Ovaries zako (hysterectomy),
kwa kawaida huweza kusababisha kukoma hedhi mara moja. Ingawa hupati hedhi tena, lakini ovari zako bado hutoa mayai na kutoa kichocheo cha estrojeni na progesterone.
4. Huduma ya Chemotherapy na tiba ya mionzi,
Tiba hizi za saratani zinaweza kusababisha kukoma kwa hedhi.
Ingawa sio kila Mara ukipata huduma hizi basi utapata tatizo la Hedhi Kukoma au kupoteza uwezo wa kuzaa,
Tiba ya mionzi huathiri tu kazi ya ovari ikiwa mionzi inaelekezwa kwenye ovari.
Tiba ya mionzi kwa sehemu zingine za mwili, kama vile kwenye tishu za matiti, kichwani na shingoni, haitaathiri kukoma hedhi.
5. Tatizo la Primary ovarian insufficiency,
ambapo Takriban asilimia 1% ya wanawake wanakuwa wamemaliza kuzaa kabla ya umri wa miaka 40 (kukoma hedhi mapema).
Kukoma hedhi kabla ya wakati kunaweza kutokana na tatizo la kushindwa kwa ovari zako kutoa viwango vya kawaida vya homoni za uzazi, tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Primary ovarian insufficiency
ambayo inaweza kutokana na sababu za kigenetics au magonjwa ya mfumo kinga yaani autoimmune diseases. N.k
DALILI ZA UKOMO WA HEDHI(Menopause)
Mwanamke ambaye amekaribia ukomo wa hedhi(perimenopause), anaweza kupata dalili mbali mbali na dalili hizo ni kama vile:
- Blid kuanza kutokueleweka kama mwanzoni
- Kuanza kupata tatizo la Ukavu wa uke
- Mwili Kuwaka moto au kuwa na joto sana kuliko kawaida
- Kuhisi Baridi sana mara kwa mara
- Mwili Kutoa sana Jasho wakati wa usiku
- Kuanza kukosa usingizi au kupata Shida ya kulala
- Mood hubadilika
- Kuongezeka kwa uzito wa mwili na kupungua kwa mchakato wa kimetaboliki
- Kuwa na Nywele nyembamba na ngozi kavu
- Kupoteza umbo la matiti,matiti kusinyaa zaidi n.k
- Ishara na dalili, pamoja na mabadiliko katika hedhi vinaweza kutofautiana kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
- Vipindi vya kuanza kukosa hedhi mara kwa mara kuliko ilivyokawaida vinatarajiwa kutokea.
- Mara nyingi, vipindi vya hedhi vitaruka mwezi na kurudi, au kuruka miezi kadhaa na kisha kuanza mizunguko ya kila mwezi tena kwa miezi michache.
Vipindi hivi pia huweza kuhusisha kutokea kwa mizunguko mifupi, Licha ya vipindi visivyo vya kawaida, ujauzito pia unawezekana katika kipindi hiki.
Hivo ni muhimu pia kuchukua tahadhari kwani uwezo wa mwanamke kutokubeba mimba huanza baada ya kuingia kipindi cha ukomo wa hedhi na sio karibu na ukomo wa hedhi.
Kwa maana nyingine,mwanamke ambaye amekaribia ukomo wa hedhi anaweza kubeba mimba pia.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!